Walimu wacharazwa bakora tena, mbele ya wanafunzi wao!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu wacharazwa bakora tena, mbele ya wanafunzi wao!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Dark City, Apr 21, 2010.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Habari zilizorushwa na TBC1 saa 2 usiku zinaeleza kuwa baadhi ya walimu wa shule ya msingi Sakasaka iliyoko wilaya ya Meatu, Shinyanga wamechapwa viboko na Sungusungu kwa kosa la kutohudhuria mkutano wa kijiji. Pia mke wa mwalimu mkuu amechapwa viboko baada ya kuvuliwa nguo hadharani. Na kuna mmojawapo wa hao walimu alikuwa mjamzito. Walimu waliocharazwa bakora na baadhi ya wanafunzi walioshuhudia walihojiwa na mwandishi wa habari Richard Leo, kutoka Mwanza.

  Hili ni tukio la pili baada ya lile lilotokea mwaka jana katika kijiji cha Katerero, Bukoba vijijini ambapo mkuu wa wilaya wa wakati huo Mnari alimwamuru askari kuwachapa viboko walimu waliokuwa wamechelewa kufika shuleni. Pamoja na Mnari kufukuzwa kazi ya ukuu wa wilaya, hakuna taarifa kama alichukuliwa hatua zaidi. Pia walimu walifungua kesi kudai fidia ingawa haijulikani hiyo kesi inaendeleaje.

  Je nini kifanyike walimu waache kudhalilishwa?
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Haya mambo bwana, lakini kisheria ukiondoa madenti si viboko kwa watu wazima hadi hakimu aruhusu? Hawa sungusungu wanao uwezo kweli kiutaratibu kuchapa viboko?
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa nchi yetu kila mtu mwenye madaraka hata yakiwa madogo kiasi gani anaweza kuchapa mtu bakora. Huko vijijini hata Mjumbe wa nyumba kumi (tena akiwa wa CCM) anaweza kutembeza bakora atakavyo. Lakini walimu ndio wamejishushia dhamani yao kwa kukubali kuwa mawakala wa CCM. Kwa wingi wao na jinsi ambavyo wamesambaa kila kona ya nchi wangeamua kutotumika wangeheshimika sana.
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hiyoni kwa wasukuma tu. Mwalimu mzima mpaka unalazwa chini bado upo tu!!!! Ndio maana mnatishiwa amani na upendo mpaka mnakufa wakavuuu, acha wachapwe kama hata mwalimu hajui haki yake hao wanakijiji je?:angry:
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Aisee, hii ni aibu kwa nchi inayojigamba kuwa ina utawala bora na unaofuata sheria. JK upo wapi?
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sio waalimu tu, things are now going out of proportions, jumamosi mkuu wa mkoa
  ( RC) katuma mapolisi na maafisa usalama kumtoa ndani ya ofisi mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba Kigoma eti kwa sababu hafuati maelekezo yake.

  Inaelekea rule of law inaanza kupuuzwa, ukifanya kosa naamua adhabu ya kukupa papo hapo ndio maana yake.

  Tunakwenda wapi????
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu. Siyo tatizo la wasukuma tu. Albert Mnari alichapa walimu wa Bukoba. Na hao walikuwa wasukuma? Kuna tatizo kubwa zaidi ya Wasukuma au Wahaya.
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Kutojua haki yako ni tatizo kwa Watanzaniawengi.
  kule kanda ya ziwa sungusungu ndiye askari wa usalama barabarani, kutuliza gasia, na pia ndiyo jeshi la ulinzi, kwa hiyo pale kilichotokea ni ugaidi tu wa kuwavamia walimu na kuwapiga, sidhani kama kulikuwa na jinsi ya wanawake hao kujikinga (angalau wanaume) hasa kwa vile walichukuliwa kama wahalifu kwa kutohudhuria vikao vya serikali ya kijiji (sungusungu). Zamani ilikuwepo tabia ya kuwatenga watu wanaohisiwa kuwa wahalifu, pamoja na wale wasioshiriki shughuli za kijamii, ukikutwa hata unamsalimia mtu aliyetengwa na wewe pia unatengwa!
  Tusiwalaumu walimu hawa, kwani mambo haya yapo kila sehemu, hata askari wetu wanawakwida watu na kuwapiga bila hatia. sioni tofauti kati ya sungusungu na wanausalama wetu.
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Walimu wakilipwa mshahara mzuri na kuwekewa mazingira mazuri ya kufanyia kazi, uzalilishwaji na upuuzi wote huu utakwisha.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
   
 11. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hili jambo lilikuwepo vijijini siku nyingi ambapo mtendaji wa kijiji anatoa adhabu kwa kuwacharaza bakora wananchi. Tatizo huko vyombo vya habari hakuna ndo maana taarifa hazijulikani. Kipindi kile nikiwa kijijini, nilishuhudia hiyo hali, na watu waliikubali kwasababu ya uelewa wao, kipato chao na mazingira. Ndo maana hii inaipa CCM company ya kupeta, maana licha ya kuchapwa wale watu hawaelewi zaidi ya thi-thi-e-mu. WACHA WAPATE BAKORA NDO ZITAWAZINDUA.
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nchi inapokosa utawala wa sheria matokeo yake ni hayo...Kila mtu anajiona ana uwezo wa kuamua chochote!...Adhabu ya mtu aliyekosa kuhudhuria kikaon ni kiboko?...Idont think so!...huu ni udhalilishaji!
   
 13. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Watoto siku zote huiga toka kwa wakubwa zao, walichofanya sungusungu wa shinyanga ni zao tu la wanachofanya wakubwa wengine, na hii ni wazi kuwa hapa TZ hakuna kitu kama utawala wa sheria. lakini mimi niwakumbushe tu hapa"wakubwa" wao wako ndani ya nyumba za vioo na wanawaudhi waponda kokoto, usiku utakokucha waponda kokoto wakagundua kuwa hao wanaowaudhi wanaishi kwenye nyumba za vioo.....
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni kwa upande mmoja kwa upande wa pili ni kudharau utawala wa sheria, mtu unapata wapi haki ya kumhukumu mwenzio na kumchapa viboko? Mijini ndio zaidi haki zetu zinapokwa sie tunacheka tu eti maborn town. Amoeba, Umeunderestimate hawawakwidi bali wanawapiga risasi na kuwauwa watu eti majambazi na sisi badala ya kusimama na kulaani tunaunga mkono tuu. Tangu polisi wameanza hakuna inquiry hata moja ilitumwa kuangalia kama ni kweli au la.
  .
   
 15. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  naagree mkuu,
  hata huo utawala wa sheria wenyewe hupo hapa Tanzania. ni wanausalama na vigogo wangapi walio na kesi mahakamani?....kati ya hao ni asilimia finyu sana wanaohukumiwa kwa kuvunja haki za raia, wengi wanapiga risasi raia, kuwacharaza bakora, na kuwatukana matusi ya kuwadharirisha hadharani (unakumbuka waalimu wanafunzi wa chuo kimoja walivyoitwa WAPUMBAVU na kigogo wa kike?). Hao ndiyo wenye dhamana ya kusimamia utawala wa sheria, hebu nambie watawezaje wakati wenyeewe ndy wako mstari wa mbele katika kuzibaka hizo sheria?!

  Signature yako inaongea jambo la msingi kabisa mkuu.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na kitendo hiki pale nilipokuwa naangalia habari jana ..na hii si mara ya kwanza kutokea
  Kuna mtu mwenye mamlaka ya kwachapa walimu viboko??
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,995
  Trophy Points: 280
  Nyerere alipewa na nani mamlaka ya kuwachapa wanachuo cha udsm?
   
 18. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Jamani hiki kitendo ni cha kulaaniwa kwa nguvu zote, na hao sungusungu pamoja na mwenyekiti wao wawekwe ndani na wao wacharazwe viboko.

  Leo imeanza kwa walimu tunachekelea kesho itakuwa wafanyakazi wa maofisini wanatolewa nje na kuchapwa na sisi tunaendelea kuchekelea.

  Masikini walimu wamekosa nini? Ndio waliotutoa kwenye ujinga leo hii ndio fadhila yao! POLENI SANA WALIMU KWA UDHALILISHAJI HUO
   
 19. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kwa mwendendo huu, itafika mahali waalimu washinde kuwafundisha wanafunzi, kwani wanafunzi watajichukulia hatua na kuwachraza viboko waalimu.
  Hivi viongozi wa juu serikalini wanaliona hili? na kama wanaliona, wanasemaje?

  Ningewashauri hao waalimu wawachukulie hatua za kishari ahao watu waliowacharaza viboko, ikiwa ni pamoja na waalimu wote kugoma kufunfudisha katika shule hiyo.
   
 20. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah hii kali tena, richad leo wa TBC anabahati sana ya kupata habari za kuchekesha flani hivi na oia kuripot kwake ndo huwa nacheka zaidi.
   
Loading...