Walimu wa Tanzania mmekombolewa!

Radio Producer

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
724
295
SERIKALI imeamua kuwa kuanzia sasa walimu nchini, kama ilivyo kwa madaktari, wataajiriwa na kupangiwa moja kwa moja vituo vya kazi bila kufanya usaili ama kucheleweshwa na michakato na taratibu nyingine za kirasimu, ili mradi wawe wameshinda mitihani yao.
Ili kutekeleza uamuzi huo wa Serikali, imeamuliwa kuwa walimu watapangiwa vituo vya kazi katika miezi ya mwisho ya mafunzo yao ili kuwawesha kuripoti moja kwa moja kwenye vituo vyao baada ya kumaliza masomo na mafunzo yao.
Uamuzi huo wa Serikali ulifikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika wiki iliyopita, Alhamisi, Februari 3, 2011, mjini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Baraza limefikia uamuzi huo kwa kutilia maanani uhaba wa walimu, kama walivyo madaktari nchini na, kwa nia ya kupanua na kuboresha kiwango cha huduma elimu.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI
07 FEBRUARI, 2011
 
Sasa huo ndio ukombozi kwa walimu?Badala ya kuwaongezea mshahara waweze kujikimu wanawaharakisha kazini!
 
Mie nilifikiri kuanzia sasa tutaanza kulipwa kama wabunge aagh! kumbe ni kuwahishwa tu kazini, anyway!
 
''walimu wa Tanzania mmekombolewa''
Hii title hii!... Huo ndo ukombozi kweli?.. Au ulikua unataka kuatrack attention ya JF?
 
Sasa huo ndio ukombozi kwa walimu?Badala ya kuwaongezea mshahara waweze kujikimu wanawaharakisha kazini!

maslah ndio ukomboz c kupata ajira fast,mazngra mazuri ya kaz na nyenzo za kufundishia,kwa sasa kufundisha serikalin ni adhabu
 
Tangu tumehitimu july 2011 hadi leo hamna tetesi za kuajiriw, hizi ni siasa tu na mpango wameshindwa kuutekeleza. TZ too much politics,,, damn
 
jamaani habari nzuri ni ankara hlo la kupangiwa direct kwa mwl. hasa tz ni wajibu wa serikali
 
Back
Top Bottom