Bukondamoyo
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 458
- 487
.
Monday .February 18,2019
Walimu wa Shule ya Sekondari Magu mkoani Mwanza, wameweka Historia mpya katika shule hiyo na wilaya ya Magu, kwa kuchangia takribani Milioni 14 kwa ya ajili ya ujenzi wa chumba cha Darasa shuleni hapo, ikiwa ni jitihada za Walimu kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa. Haya yamesemwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Magu Mwalimu Sahani Bilaazah amebainisha kuwa Wazo hilo lilitokana na ongezeko la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2019 kufikia 500 ukilinganisha na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka jana walikuwa 220. Hivyo kwa hivi sasa shule ina Wanafunzi 1320 na vyumba vya madarasa vilivyopo ni 14 kwa O-Level badala ya 27 kwa hiyo upungufu hadi hivi sasa ni vyumba 13, Sisi Walimu tumeamua na kwa imani tuliyonayo kwa Serikali yetu ya awamu ya tano ya Mhe: Rais John Magufuli tunaonesha njia kwa vitendo ili jamii ijitoe kuachangia shughuli za maendeleo hasa kwa ujenzi wa miundo mbinu hapa shuleni kwetu.
Mwalimu Mwandu Michael(Makamu mkuu wa Shule) yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ameeleza kuwa wazo hilo lilipoibuliwa na kujadiliwa katika kikao cha Walimu liliungwa mkono kwa asilimia 71, Kamati iliundwa na Katibu akiwa ni Mwalimu Arthur Simkonda na Mtunza fedha ni Mwalimu Adam Matemu, Hivyo hadi sasa Walimu 34 kati ya 48 ndiyo waliojitolea kujenga chumba cha darasa hiki. Mwandu amefafanua kuwa zoezi hili ni shirikishi na silazimishi hivyo walimu walioridhia ndiyo wanachangia Kiasi cha Tshs 35,000/- kila mwezi wakati huo Mkuu wa Shule amechangia Tshs 1,000,000.00 kufikia mwezi Augost 2019 watakuwa wanakamilisha ujenzi na mwezi wa Septemba watakabidhi Jengo hilo Serikalini likiwa tayari kwa matumizi. Akizungumzia mafanikio ya mradi Mwandu amesema kwa fedha waliyochanga kwa mwezi Januari imefanikisha kusomba mawe, kujenga msingi na kumwaga jamvi hivyo mchango wa mwezi Februari wataanza kujenga boma. Mwandu ametoa wito kwa jamii kuitikia wito wa kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ili kutatua changamoto ya upungufu miundo mbinu , Walimu ni sehemu ya jamii tunafanya hili kama jamii tunaomba na wadau wengine wajitokeze kuunga mkono jitihada hizi. Alilisitiza Mwandu Michael
Kwa upande wa Serikali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba ameridhishwa na uzalendo wa Walimu hao, na kwamba tayari alishamwagiza Mhandisi wa Ujenzi kufanya kazi bega kwa bega na Kamati ya Walimu inayosimamia ujenzi wa mradi huo. Hali kadhalika Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza kupitia barua yake Kumb. Na. DA.2/186/01/67 ya 28.01.2019 amewapongeza Walimu waliojitolea na kwamba ni mfano wa kuigwa katika kuchochea shughuli za maendeleo na Serikali inatambua na kuthamini juhudi na michango yao. Pia jamii iendelee kuhamasishwa kushiriki kikamilifu katika utatuzi wa changamoto za kimaendeleo katika sekta ya elimu kwa Kuzingatia ongezeko la wanafunzi wanaochaguliwa kila Mwaka.
Magu Kazi na Maendeleo = Kusema na kutenda
Imeletwa kwenu na
Dominique NghonelaBubeshi(Luhegangulu)
Afisa habari, Mawasiliano na Itifaki wa Mbunge Jimbo la Magu.
email: dbubeshi@gmail.com
+255 716 094 601
Sent using Jamii Forums mobile app