Walimu wa Shule ya Sekondari Magu wajitolea kujenga chumba kimoja cha darasa

Bukondamoyo

JF-Expert Member
May 11, 2017
319
500
.

Monday .February 18,2019

Walimu wa Shule ya Sekondari Magu mkoani Mwanza, wameweka Historia mpya katika shule hiyo na wilaya ya Magu, kwa kuchangia takribani Milioni 14 kwa ya ajili ya ujenzi wa chumba cha Darasa shuleni hapo, ikiwa ni jitihada za Walimu kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa. Haya yamesemwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Magu Mwalimu Sahani Bilaazah amebainisha kuwa Wazo hilo lilitokana na ongezeko la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2019 kufikia 500 ukilinganisha na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka jana walikuwa 220. Hivyo kwa hivi sasa shule ina Wanafunzi 1320 na vyumba vya madarasa vilivyopo ni 14 kwa O-Level badala ya 27 kwa hiyo upungufu hadi hivi sasa ni vyumba 13, Sisi Walimu tumeamua na kwa imani tuliyonayo kwa Serikali yetu ya awamu ya tano ya Mhe: Rais John Magufuli tunaonesha njia kwa vitendo ili jamii ijitoe kuachangia shughuli za maendeleo hasa kwa ujenzi wa miundo mbinu hapa shuleni kwetu.

Mwalimu Mwandu Michael(Makamu mkuu wa Shule) yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ameeleza kuwa wazo hilo lilipoibuliwa na kujadiliwa katika kikao cha Walimu liliungwa mkono kwa asilimia 71, Kamati iliundwa na Katibu akiwa ni Mwalimu Arthur Simkonda na Mtunza fedha ni Mwalimu Adam Matemu, Hivyo hadi sasa Walimu 34 kati ya 48 ndiyo waliojitolea kujenga chumba cha darasa hiki. Mwandu amefafanua kuwa zoezi hili ni shirikishi na silazimishi hivyo walimu walioridhia ndiyo wanachangia Kiasi cha Tshs 35,000/- kila mwezi wakati huo Mkuu wa Shule amechangia Tshs 1,000,000.00 kufikia mwezi Augost 2019 watakuwa wanakamilisha ujenzi na mwezi wa Septemba watakabidhi Jengo hilo Serikalini likiwa tayari kwa matumizi. Akizungumzia mafanikio ya mradi Mwandu amesema kwa fedha waliyochanga kwa mwezi Januari imefanikisha kusomba mawe, kujenga msingi na kumwaga jamvi hivyo mchango wa mwezi Februari wataanza kujenga boma. Mwandu ametoa wito kwa jamii kuitikia wito wa kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ili kutatua changamoto ya upungufu miundo mbinu , Walimu ni sehemu ya jamii tunafanya hili kama jamii tunaomba na wadau wengine wajitokeze kuunga mkono jitihada hizi. Alilisitiza Mwandu Michael

Kwa upande wa Serikali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba ameridhishwa na uzalendo wa Walimu hao, na kwamba tayari alishamwagiza Mhandisi wa Ujenzi kufanya kazi bega kwa bega na Kamati ya Walimu inayosimamia ujenzi wa mradi huo. Hali kadhalika Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza kupitia barua yake Kumb. Na. DA.2/186/01/67 ya 28.01.2019 amewapongeza Walimu waliojitolea na kwamba ni mfano wa kuigwa katika kuchochea shughuli za maendeleo na Serikali inatambua na kuthamini juhudi na michango yao. Pia jamii iendelee kuhamasishwa kushiriki kikamilifu katika utatuzi wa changamoto za kimaendeleo katika sekta ya elimu kwa Kuzingatia ongezeko la wanafunzi wanaochaguliwa kila Mwaka.

Magu Kazi na Maendeleo = Kusema na kutenda

Imeletwa kwenu na

Dominique NghonelaBubeshi(Luhegangulu)
Afisa habari, Mawasiliano na Itifaki wa Mbunge Jimbo la Magu.
email: dbubeshi@gmail.com
+255 716 094 601

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,770
2,000
Yaani Hawa walimu natamani kuwa Osama mwaka juzi juzi kipindi Cha mbio za mwenge walichangiswa madawani, vyoo, maabara alafu bado mishahara yenu miduchu bado mnaisaidia serekale kwenye wajibu wake

Shenzi kabisa

Manesi nao mjenge wodi za kujifungulia

Polisi nao mjiandae kujenga sentro

Kila mtumishi jiandaeni kujenga hapo mnapofanya kazi
Screenshot_20190219-191506.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chwekamu

JF-Expert Member
Nov 1, 2017
466
500
Yaani Hawa walimu natamani kuwa Osama mwaka juzi juzi kipindi Cha mbio za mwenge walichangiswa madawani, vyoo, maabara alafu bado mishahara yenu miduchu bado mnaisaidia serekale kwenye wajibu wake

Shenzi kabisa

Manesi nao mjenge wodi za kujifungulia

Polisi nao mjiandae kujenga sentro

Kila mtumishi jiandaeni kujenga hapo mnapofanya kazi View attachment 1026797

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao walimu ni Wasenge.Wanaendekeza ukabila kuonesha kwamba wanamuunga mkono msukuma mwenzao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
3,204
2,000
Ujanja wa mtanzania nikuona nchi yake ikijengwa na mabeberu.walimu kujitolea pamoja kuwa na mishahara kiduchu bado kuna wenye akili wanawaona wao ni wajinga sana kuchangia maendeleo yao wenyewe na watoto wao.
 

mbari

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
504
500
Sishangai kuona hilo kwa walimu wa Tz.
Weng wanaish maisha duni sana ya kukopakopa na kuweka bondi smart zao na kadi zao za bank.
Nimeskitika sana nawaonea huruma walim wasiojielewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

damper

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
476
500
Mi nawapongeza sana hao waalimu kwa kitendo chao.
Huo ndo uzalendo, hata kama wana mishahara midogo kiasi gani lakini wamekubali kufanya jambo la kukumbukwa kwenye hio shule.
Leo watukaneni kwa maneno yote machafu lakini ipo siku mtatambua mchango wao ulikuwa na manufaa makubwa kwa watoto wetu.
MUNGU WABARARIKI NA KUWAPA MOYO KWA KAZI YAO NGUMU WAALIMU WETU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
Pongezi zangu nyingi ziwafikie tu hao walimu 'wazalendo' 14 kati ya wote 48 ambao kimsingi hawakuchangia. Hao ni wale wanaojitambua na hawakuogopa vitisho vingi vya kipuuzi walivyotishwa iwapo wasingechangia. Unachangiaje ujenzi wa darasa wakati kila mwezi unakatwa kodi? Tena ni pesa nyingi tu!

Mwalimu mshahara umejaa makato, huna sehemu ya kuishi, huna posho yoyote ile, hujapandishwa daraja pasipo sababu ya msingi, hujaongezewa mshahara kwa zaidi ya miaka 3 sasa! Bado utoe kahela unakopata, eti uchangie ujenzi wa darasa! Hii ni aibu ya mwaka. Si bora umtumie hiyo hela mzee wako kule kijijini ili apate ahueni ya maisha.
 

Sir Khan

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
5,128
2,000
Michango ya harusi kwa mwaka ni zaidi ya hiyo hela waliyochanga mmoja mmoja na katika hilo hakuna anayelalamika lakini leo kisa walimu wamejichanga kujenga darasa kwa manufaa ya sasa na vizazi lijavyo Watanzania baadhi kwa sababu ya upumbavu uliojaa kichwani wanaanza kuwatukana walimu wazalendo.
Enyi ngozi nyeusi ni nani aliyewaroga?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom