Walimu wa sekondari wahamishiwa kufundisha msingi Masasi mkoani Mtwara

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,051
Waraka wa Elimu namba 6, wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Elimu ya Msingi Bila Malipo, ambao kwa mujibu wa waraka huo elimu msingi inaanzia Awali hadi kidato cha nne, umeanza kutekelezwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bi Gimbana Ntavyo, kwa kuwahamisha walimu zaidi ya 50 kutoka shule za sekondari kwenda msingi.

Nikiongea na walimu hao wenye nyuso za huzuni wanasema hawajui hatma ya stahiki zao kwani hata barua zao za uhamisho sharti namba 3 linasema kwamba " Stahiki zako zote za kiutumishi zitazingatiwa endapo mabadiliko haya ya kituo cha kazi yanakulazimu kubadilisha makazi", suala ambalo halipo kisheria za kiutumishi.

Walimu hao wamekuwa na malalamiko mbalimbali wengi wakidai kuwa na msongo wa mawazo kwa kile walichokidai kuwa wamedhalilishwa. Mmoja wa walimu hao alisema kuwa kama yeye binafsi angetaka kufundisha shule za msingi hasingepoteza fedha na muda kusoma kidato cha tano na sita na chuo kikuu, badala yake angeishia kdt cha nne na kwenda vyuo vya ualimu.

Pia zoezi hili limesababisha maandamano ya wanafunzi wa kidato cha 5 & 6 siku ya 14/10/2017 katika shule ya sekondari ya wasichana Masasi kupinga uhamisho wa mwalimu wao wa somo la historia ambaye ni tegemeo kwao. Mwl huyo aliyejulikana kwa jina moja MROPE, yumo kati ya walimu hao 50 wanaokwenda shule za msingi.

Kadiri ya walimu hao ni kwamba zoezi hili limechukuliwa kama fursa pekee kwa wakuu wa shule kuwaondoa walimu ambao wanahoji utawala na mapungufu yao. Hakuna usawa na haki katika zoezi hili kwani kuna walimu wenye vipindi zaidi ya 25 wamepelekwa msingi na yule mwenye vipindi vitatu ameachwa.

Note: Serikali hii ni aibu! wahitimu wa ualimu level mbalimbali wapo mtaani wanauza migahawani na wengine wanaendesha Bodaboda.
Hivi mwl wa kidato cha sita tena tegemeo la wanafunzi kwenye shule kongwe aliyosoma hadi spika mstaafu mama Anna Makinda ameondolewa, pamoja na wanafunzi tena wa kike kuandamana hadi kwa Mkuu wa wilaya, bado hawajasikilizwa kilio chao.
Serikali naomba haya mambo mapya yafanyiwe tafiti kwanza na hili la Masasi Liwe kama case study kabla Sera yenu haijaenda mikoa mingine.
 
Sipati picha mwalimu alosoma saikolojia ya mtoto anaebalehe (elimu ya upili) anaenda kupambana na hali yake kwa watoto wenye saikolojia tofauti na watoto wa balehe
 
Uzi Kama Huu Hukuti Unachangiwa Na Vijana Wa Lumumba, Ni Mchungu Na Ngumu Kumeza! Come Back Kikwete.
 
Kama wamejaa sekondari huko msingi hakutajaa?
Wangeanza na wale ambao wangependa kuhamia msingi. Kulazimisha inakuwa Kama adhabu vile.
 
Kama wamejaa sekondari huko msingi hakutajaa?
Wangeanza na wale ambao wangependa kuhamia msingi. Kulazimisha inakuwa Kama adhabu vile.
Mimi nililiona hili na ndio maana nimesema kwa hili la Masasi serikali ichukue kama case study, waende kufanya tafiti na kurekebisha mapungufu. Cha ajabu zoezi lenyewe limeanza kwenye mkoa usio na mwamko kielimu...badala ya kujenga wanazidi kubomoa.
 
Mimi nililiona hili na ndio maana nimesema kwa hili la Masasi serikali ichukue kama case study, waende kufanya tafiti na kurekebisha mapungufu. Cha ajabu zoezi lenyewe limeanza kwenye mkoa usio na mwamko kielimu...badala ya kujenga wanazidi kubomoa.
Wewe wamekupeleka kijiji gani mkuu?
 
Walimu ni wito. Mnalalamika nini?
Mnadai ualimu ni wito, eti wanyanyaswe, wadhadhalilishwe, wadhulumiwe, na kila mabaya wafanyiwe kila baya, wengine zenu ndio kazi, mnakula bata tu!
D u u ! Uko wapi moyo unaopenda haki, usiohuzunika kwa Ubinafsi na ukatili kama huu?
 
hv kweli mwalimu aliyesomea kufundisha sekondary tena kwa kingereza leo hii unampeleka msingi akafundishe kwa kiswahili unategemea nn kwenye elimu ya mwanafunzi tokea msingi. elimu ndio inapigiliwa misumari ya mwisho kaburini hivyooo....
 
Si Mkulu aliwaambia wasihame kama hawajapewa yao hata wakiambiwa nafikiri alimaanisha hata wakifosiwa au!?
 
Cha maana ni kudai stahiki zinazoambatana na uhamisho. Kulalamika eti ni udhalilishaji si kweli! Kuna walimu kibao wana masters zao na wanafundisha shule za msingi kwa furaha! Ulaya hali kadhalika!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom