Elections 2010 Walimu wa Sekondari kutopigakura huko Igunga tarehe 2/9/2011

Esoterica

Member
Jun 18, 2011
48
11
Wanafunzi wa Kidato cha 4 nchini kote watakuwa wakifanya MTIHANI WA TAIFA wa KUMALIZA KIDATO CHA 4 kuanzia tarehe 3/10/2011. Hivyo walimu kadhaa wa sekondari nchini kote watahusika kusimamia mtihani huo. Walimu wa Igunga nao watahusika kusimamia mtihani huo pia.

Kwa taratibu za NECTA walimu wanaosimamia mtihani wanapaswa kusimamia mtihani ktk shule ambazo siyo vituo vyao vya kazi. Hivyo walimu wengi tu wa shule za sekondari za Igunga watamepelekwa kusimamia mtihani ktk maeneo yaliyo mbali na shule zao kuanzia tarehe 2/10/2011 siku ambayo pia wanapaswa kupigakura katika kata zao huko Igunga. Nionavyo mie walimu hao wakipangwa kusimamia mtihani ktk kata za mbali watakosa haki yao ya kumchagua mbunge wanayemtaka.

Je itawezekanaje kuwarudishia walimu hao haki yao ya kumchagua mbunge wamtakaye?
 
Kwanza badili heading si 2/9, pili kusimamia mtihani si walimu wote shule inaweza kutoa msimamizi mmoja au wawili au isitoe kabisa, tatu wasimamizi huwa hawapelekwi nje ya wilaya nne kura zinapigwa J'2 mwl anaweza kupiga asubuhi na akawahi kwenye kituo chake.
 
Nawashauri wapige kura kwanza ndio waende huko pori, kula zao ni muhimu sana!
 
Heshima kwako mkuu,
Ni kweli siyo wote. Lakini je walimu zaidi ya 60 wasipopiga kura hakuna 'impact' ktk kumuongezea mgombea ushindi? Kumbuka kwamba kuna mbunge mmoja wa bunge la 10 kutoka ktk Mkoa wa Shinyanga alishinda kwa tofauti ya kura moja.

Je waifaham vema miundombinu ya barabara za Igunga? Sheria inawanataka walimu waripoti ktk vituo vya mtihani masaa 24 kabla ya kuanza kwa mtihani hasa vijijini ktk wilaya hiyo.
 
Mkuu,
Ni kweli kura zao ni muhimu lkn wanaweza wakapelekwa kwa magari ya serikali na wakalazimika kuondoka makao makuu ya wilaya asubuhi ya j2 wakipelekwa walikopangiwa kusimamia mtihani. Je wafanyeje?
 
Hapo hakuna jinsi kwakuwa kazi wanayoenda kuifanya ni muhimu pia.
 
Heshima kwako mkuu,
Ni kweli siyo wote. Lakini je walimu zaidi ya 60 wasipopiga kura hakuna 'impact' ktk kumuongezea mgombea ushindi? Kumbuka kwamba kuna mbunge mmoja wa bunge la 10 kutoka ktk Mkoa wa Shinyanga alishinda kwa tofauti ya kura moja.

Je waifaham vema miundombinu ya barabara za Igunga? Sheria inawanataka walimu waripoti ktk vituo vya mtihani masaa 24 kabla ya kuanza kwa mtihani hasa vijijini ktk wilaya hiyo.
Najua msimamizi anatakiwa ku ripoti at least one day before exam ili ayajue mazingira lakini si lazima alale hapo, iwapo kuna dharula anaweza kumjulisha mkuu wa shule kwa simu na akafika asubuhi siku ya mtihani hasa kama shule yenyewe anaijua na iko karibu. Ninavyojua kwa mfano shule ikiwa na ukumbi wa kuingiza watahiniwa wote sema 60 msimamizi mmoja tu anatosha na mkuu wa shule husika, sielewi Igunga ina shule ngapi zinazofanya mtihani wa F4 na idadi ya wanafunzi ila hoja yako si ya kupuuza.
 
Kwanza badili heading si 2/9, pili kusimamia mtihani si walimu wote shule inaweza kutoa msimamizi mmoja au wawili au isitoe kabisa, tatu wasimamizi huwa hawapelekwi nje ya wilaya nne kura zinapigwa J'2 mwl anaweza kupiga asubuhi na akawahi kwenye kituo chake.
Majibu rahisi sana!I'm happy for them coming from unofficial..!
 
Najua msimamizi anatakiwa ku ripoti at least one day before exam ili ayajue mazingira lakini si lazima alale hapo, iwapo kuna dharula anaweza kumjulisha mkuu wa shule kwa simu na akafika asubuhi siku ya mtihani hasa kama shule yenyewe anaijua na iko karibu. Ninavyojua kwa mfano shule ikiwa na ukumbi wa kuingiza watahiniwa wote sema 60 msimamizi mmoja tu anatosha na mkuu wa shule husika, sielewi Igunga ina shule ngapi zinazofanya mtihani wa F4 na idadi ya wanafunzi ila hoja yako si ya kupuuza.
No research no right to say...!
 
Mkuu,
Ni kweli kura zao ni muhimu lkn wanaweza wakapelekwa kwa magari ya serikali na wakalazimika kuondoka makao makuu ya wilaya asubuhi ya j2 wakipelekwa walikopangiwa kusimamia mtihani. Je wafanyeje?
Nakubaliana na hoja yako, lakini sidhani kama huwa wanapelekwa kwa magari ya serikali, ila ikitokea hiyo wilaya itakuwa na utaratibu mzuri sana lakini nijuavyo mwl anatakiwa kujigharamia usafiri wa kwenda na kurudi kwa sababu kila kitu huwa included kwenye posho wanazopewa.
 
Zipo wilaya zinazowasafirisha.
 
Wanafunzi wa Kidato cha 4 nchini kote watakuwa wakifanya MTIHANI WA TAIFA wa KUMALIZA KIDATO CHA 4 kuanzia tarehe 3/10/2011. Hivyo walimu kadhaa wa sekondari nchini kote watahusika kusimamia mtihani huo. Walimu wa Igunga nao watahusika kusimamia mtihani huo pia.

Kwa taratibu za NECTA walimu wanaosimamia mtihani wanapaswa kusimamia mtihani ktk shule ambazo siyo vituo vyao vya kazi. Hivyo walimu wengi tu wa shule za sekondari za Igunga watamepelekwa kusimamia mtihani ktk maeneo yaliyo mbali na shule zao kuanzia tarehe 2/10/2011 siku ambayo pia wanapaswa kupigakura katika kata zao huko Igunga. Nionavyo mie walimu hao wakipangwa kusimamia mtihani ktk kata za mbali watakosa haki yao ya kumchagua mbunge wanayemtaka.

Je itawezekanaje kuwarudishia walimu hao haki yao ya kumchagua mbunge wamtakaye?

Wataona namna ya kufanya kwa wale wanaopenda kupiga kura..mara nyingi kwenye hii mitihani mwalimu hawezi kuvushwa toka mkoa mmoja kwenda mwingine..mara nyingi wanatoka shule moja kwenda nyingine katika mkoa au wilaya moja...
 
Nawashauri wapige kura kwanza ndio waende huko pori, kula zao ni muhimu sana!

Jamaa amekuja na hoja muhimu. Tume ya Uchaguzi ishughulikie suala hili ipasavyo. Kwa hali ilivyo Igunga ya Shinyanga yanaweza kujirudia. Kila kura ichukuliwe kwa uzito unaostahili.
 
Mkuu,
Ni kweli kura zao ni muhimu lkn wanaweza wakapelekwa kwa magari ya serikali na wakalazimika kuondoka makao makuu ya wilaya asubuhi ya j2 wakipelekwa walikopangiwa kusimamia mtihani. Je wafanyeje?

teh! Magari ya serikali....!? we sasa naona umeanza kuota wakati jua linachomoza, yapi hayo wakati hata baiskeli za kupelekea wagonjwa mahospitalini zimebinafsishwa.
"Ndugu yangu kajipange sawa sawa"
 
Back
Top Bottom