Elections 2010 Walimu wa Sekondari kutopigakura huko Igunga tarehe 2/9/2011

teh! Magari ya serikali....!? we sasa naona umeanza kuota wakati jua linachomoza, yapi hayo wakati hata baiskeli za kupelekea wagonjwa mahospitalini zimebinafsishwa.
"Ndugu yangu kajipange sawa sawa"

Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.
 
Jamaa ametoa hoja nyeti sana,mimi ni msimamizi wa mitihani hiyo pia<sio Igunga>,kifupi uwezekano wa walimu hao kupiga kura utakuwa mdogo saana,hii ni changamoto nyingine kwa tume ya uchaguzi
 
Jamaa amekuja na hoja muhimu. Tume ya Uchaguzi ishughulikie suala hili ipasavyo. Kwa hali ilivyo Igunga ya Shinyanga yanaweza kujirudia. Kila kura ichukuliwe kwa uzito unaostahili.

kila kitu Tume. Hapa tume wafanye nini sasa? Wagonjwa mahospitalini nao wabebwe wapelekwe vituo vya kura. Zoezi la kusamamia mitihani ni muhimu kama lilivyo la kupiga kura.
 
Jamaa ametoa hoja nyeti sana,mimi ni msimamizi wa mitihani hiyo pia<sio Igunga>,kifupi uwezekano wa walimu hao kupiga kura utakuwa mdogo saana,hii ni changamoto nyingine kwa tume ya uchaguzi

Wanaoguswa na 'thread' hii ndiyo wanaojua UKWELI wa jambo hili
 
Good observation mkuu. CCM najua kabisa watafurahia walimu kutopiga kura maana most likely kura za walimu zitachagua mabadiliko(Mwl Kashindye). Kikubwa ni wao wenyewe kuhakikisha wanapaza sauti waachiwe haki yao ya kupiga kura, so zoezi la kusambazwa kwao lianze saa 7 mchana muda wa asbh wautumie kupiga kura!
 
najua ulichotaka kuelezea ila kwa utaratibu wa serikali walimu hupangwa kusimamia mitihani ktk shule zilizo ndani ya wilaya yao kiasi kwamba mtu anaweza kufika muda wowote ule,na siku ya jpili hao walimu wanaweza wakapiga kura halafu wakaenda kusimamia mitihani halafu isitoshe sio wengi kihivyo kiasi kwamba wafikie kuharibu utaratibu wa uchaguzi
 
Kupiga kura ni haki ya ya kidemokrasia ya kila mwananchi, na si hivo tu katika kupiga kura kila kura inahesabika (inauzito tosha kuleta tofauti) na ina muhimu katika kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa, kwa hiyo kwa sababu hizi lazima wawezeshwe kupiga kura zao.
 
Mkuu,
Ni kweli kura zao ni muhimu lkn wanaweza wakapelekwa kwa magari ya serikali na wakalazimika kuondoka makao makuu ya wilaya asubuhi ya j2 wakipelekwa walikopangiwa kusimamia mtihani. Je wafanyeje?
Kwa kuwa ni haki yao kupiga kura, na vituo vya kupigia kura vipo across Igunga na anayechaguliwa ni huyo huyo, basi watafutiwe vibali vya kupigia kura katika vituo watakavyokuwa karibu navyo kulingana na kama watakavyopangwa kusimamia mitihani....! Kama vile wasimamizi wa kura wanavyofanyiwa...!
Hofu yangu ni kwamba;
  1. Je, Wanaigunga wamejiandaa vema kuwaumbua wageni wanaoingia huko wasipige kura?
  2. Je, tangu vituo vya kujiandikisha kupiga kura vifungwe mwishoni mwa mwaka juzi, ni wangapi wameshatimiza umri wa kupiga kura na sasa hawana kadi hizo? Na hawa watazingatiwa vipi? Hasa ikizingatiwa kuwa ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA?
 
Back
Top Bottom