Walimu wa sec newala walipwe mishara yao.

Dec 6, 2012
7
0
Nakuja kwenu wadau wa elimu katika kuweka wazi swala hili la aibu na ajabu kabisa. mwanzoni mwa mwaka huu kulikua na zoezi la ukaguzi wa watumishi zoezi ambalo liligusa pia kada ya elimu, katika wilaya ya newala zoezi hili liliacha majeraha kwa baadhi ya walimu kwani walikatiwa mishahara yao ya mwezi wa pili na watatu, lakini iligundulika yalitokea matatizo ya kiutendaji hivyo walimu wale walirudishiwa mishahara yao lakini walibaki wanaidai halmashauri mishahara miwili ya mwezi wa pili na watatu ambayo hadi napost topic hii hakuna dalili wala kusikia mtu aongelee swala la mishahara hiyo, sasa naomba wadau mtoe mawazo yenu nini kifanyike kuwarudishia walimu hawa haki yao ya msingi yani walipwe hiyo mishahara miwili,
kama tunavyojua wote kada ya elimu ni miongoni mwa kada ambazo mishahara yake bado haina tija kwa watumishi wake lakini pamoja na kulipwa kiwango kidogo cha mshahara bado kunadhuruma na uonevu ndani ya kada hii, kwa kwani unaposhindwa kumlipa mtumishi haki yake kwa wakati ujue unadhorotesha utendaji wa kazi katika halmashauri zetu, alafu siku ya mwisho tuna lalamika ufaulu umekua hafifu, utaongezekaje kama kunamwalimu ambaye tangu anaanza kazi mwaka 2008 hadi leo bado hajalipwa baadhi ya mishahara yake, kweli walimu bado wapo kazini lakini kwa kinyongo.
na wahanga wa tatizo hili ni watoto wetu na Tanzania ya kesho sijui itakua nasura gani?kama hatuzalishi vijana wengi wasomi?
TAFAKARI CHUKUA HATU,,,
 
Back
Top Bottom