Walimu wa masomo ya sayansi jitathimini

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,394
9,279
Niende moja kwa moja kwenye mada walimu wa masomo ya sayansi ebu angalieni ufauru wa matokeo ya wanafunzi kidato cha pili arafu mkae chini mjitathimi maana haiingii akilini mtoto wa kidato cha pili anaepata A somo la kingereza arafu anapata F somo la Biology au Chemistry kidato cha pili kweli hampo serious zile kelele zenu sijui watoto hawafundishiki hamna uyu mtoto kajuache kusoma na kuandika kama afundishiki

Hii kasumba ya masomo ya sayansi magumu tuache wajibikeni mbona zamani haikuwa hivi tulizoea kuona hayo mambo somo la hesabu tu tena kidato cha nne ila sasa mambo yamekuwa tofauti physics shida, Biology shida, Chemistry shida hapana kuna uzembe hapa kidato cha pili yani kidato cha pili mtoto anashindwa fauru Biology au Chemistry are you serious?

NICHOMEKEE NA HILI PIA

Ukija kwenye somo la CIVCS napo huu ni ujingaa wa wataaluma kuamini kila mwalimu anaweza fundisha CIVICS matokeo yake ndio hayo nayo somo linafanya vibaya wakati zamani somo hilo kila mwanafunzi alifauru sababu lilifundishwa na walimu mahiri wa somo husika leo hii mwalimu wa kiswahili anaenda fundisha CIVICS kweli
 
CCM wameua elimu,hawataki kuajiri walimu shule ya kata inamwalimu 1 wa sayansi Sasa mtoa mada hujui haya matatizo yenu au uhuni tu
Hakuna shule ya kata haina mwalimu wa sayansi serikali hii miaka muwili imewapangia walimu moja kwa moja shule kutokana na uhitaji na tarifa zilizopo Tamisemi kwaiyo kama kuna shule haina mwalimu wa somo la sayansi wakuanza ulizwa ni afisa elimu na mkuu wa shule uyo mwalimu kaenda wapi maana hawaruhusiwi kuhama hao walimu
 
Elimu bora ni neno pana, linaanzia kwenye kuwepo kwa waalimu wa kutosha, mishahara mizuri ya waalimu, mazingira rafiki ya ufundishaji, mitaala bora n. K

Bado hatujawa serious na swala la elimu.
 
Hakuna shule ya kata haina mwalimu wa sayansi serikali hii miaka muwili imewapangia walimu moja kwa moja shule kutokana na uhitaji na tarifa zilizopo Tamisemi kwaiyo kama kuna shule haina mwalimu wa somo la sayansi wakuanza ulizwa ni afisa elimu na mkuu wa shule uyo mwalimu kaenda wapi maana hawaruhusiwi kuhama hao walimu
Sawa ,Sasa kuanzia form one hadi 4 mwalimu wa sayansi ni mmoja Unategemea matokeo yawe mazuri?Haya Leo nimeona mwalimu mpwayungu anasema walimu wamekwenda kusahisha kutoka mtwara hadi shinyanga na wamelipwa 520000 hivi Unategemea mwalimu atakuwa na uzalendo upi wa kufundisha! Tuendelee kwenye hiyo mada wamesema walimu walioenda semina za mitihani hawalipwi kulingana na muongozo wa serikali ,yaani halmashauri wanaamka asubuhi Leo tutalipaa ELFU 30000 Unategemea huyu mwalimu atakuwa mzalendo!
 
Unafuta ada,,halafu wazazi wanakataa kuchangia hata chakula,,ikifika saa saba watoto wamelegea kwa njaa,,wakati huohuo maslahi ya walimu ni duni unategemea utainua elimu? kugharimia elimu ni zaidi ya kufuta ada wahusika wanajua na wameamua kufumba macho.

Kuhusu civics,,mwalimu aliyeiva kwenye somo la historia una uwezo mkubwa wa kufundisha civics,,maana uhusiano wa civics na history ni mkubwa mno na hata walimu wengi ambao wanatoa matokeo mazuri ya civics ni wale ambao wamesomea au wanafundisha history.

N.B nimesoma political science na kiuhalisia kuna mwalimu kasoma history na tulikuwa tunasaidiana kufundisha civics kimsingi anafanya vizuri kiasi cha kunizidi mie ambae nahisi nimesoma mambo mengi yanayohusiana na civics.

Kingine ni experience ya somo husika
 
Tujiulize kabla ya elimu kuwa bure ilikuwaje,na baada ya elimu kuwa bure imekuwaje?
Vya bure siyo?
Hata walimu wenyewe hawapeleki watoto wao kwenye bure.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada walimu wa masomo ya sayansi ebu angalieni ufauru wa matokeo ya wanafunzi kidato cha pili arafu mkae chini mjitathimi maana haiingii akilini mtoto wa kidato cha pili anaepata A somo la kingereza arafu anapata F somo la Biology au Chemistry kidato cha pili kweli hampo serious zile kelele zenu sijui watoto hawafundishiki hamna uyu mtoto kajuache kusoma na kuandika kama afundishiki

Hii kasumba ya masomo ya sayansi magumu tuache wajibikeni mbona zamani haikuwa hivi tulizoea kuona hayo mambo somo la hesabu tu tena kidato cha nne ila sasa mambo yamekuwa tofauti physics shida, Biology shida, Chemistry shida hapana kuna uzembe hapa kidato cha pili yani kidato cha pili mtoto anashindwa fauru Biology au Chemistry are you serious?

NICHOMEKEE NA HILI PIA

Ukija kwenye somo la CIVCS napo huu ni ujingaa wa wataaluma kuamini kila mwalimu anaweza fundisha CIVICS matokeo yake ndio hayo nayo somo linafanya vibaya wakati zamani somo hilo kila mwanafunzi alifauru sababu lilifundishwa na walimu mahiri wa somo husika leo hii mwalimu wa kiswahili anaenda fundisha CIVICS kweli
Soma hii
Screenshot_2023-01-07-11-40-16-936_com.android.chrome.jpg
 
Tujiulize kabla ya elimu kuwa bure ilikuwaje,na baada ya elimu kuwa bure imekuwaje?
Vya bure siyo?
Hata walimu wenyewe hawapeleki watoto wao kwenye bure.
Uko sahihi sana,,hata kama tutajenga madarasa mengi kiasi gani na malumalu na vioo juu,,kama hatutaboresha maslahi ya walimu na kutengeneza mazingira bora ya wanafunzi kusoma mfano upatikanaji wa chakula cha uhakika mashuleni basi matokeo yatakuwa hayahaya miaka yote.

Wazo la kujenga shule za kata lilikuwa sahihi,,ila kutokana na changamoto wanazokabiliana wanafunzi nyumbani na mitaani nadhani kwa sasa ni bora shule zilizopo zikatanuliwa na kuwekewa hostel ili watoto wakae hostel kuliko hali ya sasa,,kwa maeneo yanayowezekana hasa mikoani ambako bado ardhi ipo ya kutosha.
 
Tujiulize kabla ya elimu kuwa bure ilikuwaje,na baada ya elimu kuwa bure imekuwaje?
Vya bure siyo?
Hata walimu wenyewe hawapeleki watoto wao kwenye bure.
Screenshot_20230107-115015_1.jpg
ukisema wazazi hawapeki kwenye bure ebu niambie shule kama hii wenye uelewa anajua mda ule elimu si bure idadi ya watoto ilikuwa ampaka mia saba sasa elimu bure angali hiyo ni META SEC ipo mbeya shule kongwe na marufu nchi hii
 
Km umewahi kufundisha hata tempo tu utaelewa msoto wa walimu, nakumbuka niliendaga kupiga tempo uko Shinyanga vijijini daaah ni hatari kwanza watoto wanapenda shule Ila sasa maabara hakuna vifaa vya kufundishia vichache library hakuna,

Kuna maswali ya practical inabidi unawaonyeshe vijana jinsi litmus paper inavyobadirika rangi unashindwa sababu ya uhaba wa vifaa, miezi 6 kwangu ulikua km mwaka, Sayansi sio Literature inahitaji practice na mtu aone nini kinakua nini na practice ni vifaa vya kutosha nenda Kilwa kajionee shule zilivyo utachoka na mbunge wao yupo tu anasubiri kula pensheni, mbunge wa Kilwa soma hii comment
 
Physics
Chemistry
Biology
Mathematics

Sio makalio kwamba kila mtu anayo.

Wanafunzi wana fail wenyewe kwa uzembe wao.
Fundisheni watoto hizi hoja zenu zinafanya muwe wazembe na kufail ioneka e kawaida
 
Physics
Chemistry
Biology
Mathematics

Sio makalio kwamba kila mtu anayo.

Wanafunzi wana fail wenyewe kwa uzembe wao.
mwalimu anayefundisha shule hizi za kata amekuelewa sana,,watoto wanaendekeza sana michezo,,ili wasome wanahitaji mkono wa chuma,,ukiwabinya ili wasome wazazi wanakuja juu,,viongozi wanakuja juu kwa mgongo wa haki za binadamu..

Wanasahau kuwa hakuna mwalimu kichaa anayeweza kutoka nyumbani kwake kwenda kuadhibu watoto wakitanzani bika sababu ya msingi.

Nilipoajiriwa nilikaa mwaka mzima simuwahi adhibu mtoto kwa kuwa nili amini ushauri na nasaha na kuwatia moyo pamoja kuwa inspire kunatosha sana kwa watoto kutekeleza wajibu wao wamsingi.

Baada ya muda nikagundua nilikuwa najidanganya maana ni asilimia ndogo tu ya watoto walinielewa wengi walianza kuniona dhaifu kila nikitoa oda watoto wengi hawatekelezi,,

Nikaamua kubadili muelekeo kwanza naanza kwa kuwelekeza nini wafanye na nini wasifanye wakienda tofauti wanakutana na mkono wa chuma,,ofcoz mambo yalikuwa yanaenda kwelikweli,,mpaka mkui wa shule ananiita ofisini kunipongeza.

Ila sasa ukikosea kidogo wazazi,,viongozi wanakuja juu,,inakatisha tamaa nishawahi semeshana vibaya na afisa elimu kisa utoaji wa adhabu,,nilijiuliza maswali mengi sana ,,na mwisho nikafanya maamuzi.

N.B mwalimu anapokosea mazuri yake yote yanafutika kwa msingi huu,,idadi kubwa ya wanafunzi ambao wangeweza kuokolewa wanaangamia walimu wengi wameamua kuwa reluctant.Kama kuna kiongozi wa elimu halijui hili basi uteuzi wake ulikosewa.
 
  • Mshangao
Reactions: K11
Wanafunzi wakifaulu hamsemi walimu wanafundisha vizuri, mnasema wanafunzi wana akili ila wakifeli sasa utasikia walimu hawafundishi
 
  • Thanks
Reactions: K11
Afadgali masomo ya science ila watoto wamefeli civics mpaka huruma.

Civics hii hii ya human rights mtu anafeli namna ile
 
Walimu wengi ni bodaboda. Serikali iwaongezee mishahara ili kukidhi mahitaji na kwendana na kazi yao ngumu kufundisha mtoto hadi ajitambue na kuwa mjuzi/mtaalam wa fani fulani. Baada ya mishahara kuboreshwa basi wabanwe hasa na wachape kazi. NECTA nao watoe kile anachopata mtoto-standardization iwe mwisho ITV
mwalimu wa daraja E analipwa 990,000/= bila makato hana posho mwenzi mzima,,unafikiri ataacha kutafuta hata bodboda kujiongezea kipato? hapo viongozi wanataka ufundishe remidial bure kwakisingizio cha elimu bure ila wakuu wanapewa posho na wanakomaa walimu kufundisha remedial bure,,ni suala la muda tu kama hakutakuwa na marekebisho basi tutegemee anguko kubwa sana la elimu huko mbele.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom