Walimu sasa kusaini kwa alama za vidole kwa ajili ya kuhakiki mahudhurio

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,998
5,130
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kuandaa mfumo wa kielektoniki wa alama za vidole kwa ajili ya kuhakiki mahudhurio ya Walimu Mashuleni kwenye Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri zote nchini ili kudhibiti mahudhurio ya Walimu Mashuleni.
IMG_20210910_154749_939.jpg

Wakina Lugumi wameshapata tenda tayari! Wanasubiri tu bunge kibogoyo lipitishe bajeti, ili wafaidi mema ya nchi hii.

Mnavyotaka kuwabana, kana kwamba mnawalipa mamilioni!! Kumbe ni vi jilaki kadhaa tu.
 
Hivi issue ni uwepo wao au wanachotoa wakiwepo...

Wanaweza wakawepo wanapiga usingizi kwenye meza zao hapo mbele..., Haya mambo inabidi yaanze kuwa results oriented, na results hizo sio kuona wangapi wanafaulu mtihani bali mkaguzi akija na kuchagua at random wanafunzi wachache na kuwapiga maswali kuangalia uelewa wao...
 
Ni hiviiiii !!! Tusichoshane !!! Unawahi unatia dole kwenye hicho king'amuzi unazuga zuga unawasha boxer yako ( tena unapaki mbali ili ukiwasha isisikike kisha unaenda kwenye mitikasi yako dipacha time unawahi unatia dole kwenye king'amuzi)
Tusiumuzane vichwa kenge nyie
 
Hahaha!kama.ww m mwl hili jambo limekuumiza sanaa..ila bila kuwa na chenga chenga watoto hawatokula
 
Ukipata pesa nyingi zisizo za jasho (tozo) matokeo yake unawaza ujinga.
Wanafunzi hawana madawati na madarasa ya kutosha. Ulete hivyo ili iweje?
Nunueni computer, vitabu na projector kwa ajili ya ufundishaji kuliko huo ujinga mnaowaza kuufanya.
Ndiyo shida ya kuwa na viongozi wengi wanawake.
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kuandaa mfumo wa kielektoniki wa alama za vidole kwa ajili ya kuhakiki mahudhurio ya Walimu Mashuleni kwenye Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri zote nchini ili kudhibiti mahudhurio ya Walimu Mashuleni.
View attachment 1932054
View attachment 1932059
Watengeneze za kuhakiki ufundishaji wa vipindi darasani na si mahudhurio !!
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kuandaa mfumo wa kielektoniki wa alama za vidole kwa ajili ya kuhakiki mahudhurio ya Walimu Mashuleni kwenye Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri zote nchini ili kudhibiti mahudhurio ya Walimu Mashuleni.
View attachment 1932054
View attachment 1932059
Hizo mashine ni very delicate, zinatumia umeme na ni gharama kubwa.Ukiweka mchakato mzima mpaka zipatikane na 10% zake kwa wahusika gharama yake itakuwa ni sawa na kuajiri walau walimu 1,000 au hata zaidi waende wakafundishe mashuleni.Mimi nipo taasisi binafsi tuliweka hizo mashine zilidumu miezi mi3 tu zikaharibika. Pia zinahitaji umeme usio mashaka ili ziweze kufanya kazi vizuri na kuwe na printer ya kuprint mahudhurio kila siku. Kwa mazingira ya shule zetu za msingi na sekondari nyingi zipo vijijini ambako huduma ya umeme hairidhishi, hivyo kuweka hizo mashine ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Kama ningekuwa waziri,mwarobaini wa mahudhurio kwa walimu ni kuhakikisha kila shule inawekewa mazingira bora na nyumba za walimu.Kama nyumba zipo hapo shuleni mwalimu atachelewa darasani? atakosa kuhudhuria? Shule nyingi hazina nyumba za walimu,utakuta Mwalimu anatoka kilomita 200 toka ilipo shule tena kwa mguu kufika shuleni, je atawahi vipindi?
Naomba wizara ije na mikakati inayoeleweka kwa wadau siyo hiyo ya alinacha.
Kama kuna mtu alimshauri waziri basi waziri inabidi amuangalie vizuri huyo mshauri wake maana kuna harufu ya kidilidili zaidi kuliko kuboresha elimu.
 
Back
Top Bottom