Walimu nao watangaza mgogoro na serikali nao Kugoma

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini wametanzaza mgogoro na serikali wakiwa na dhamira kubwa ya kugoma kama madai yao ya maingi hayatatimizwa ikiwa ni pamoja na nyongeza za mishahara kutokana na kupandishwa madaraja, malimvikizo ya madeni wanayodai serikali, fedha za likizo, fedha za uhamisho toka kituo kimoja hadi kingine, nk

Sasa nao wanaweza kugoma mda wowote kuanzia sasa.
 
Nimesoma kwenye thread mojawapo kwamba: Watavuruga DATA za sensa, watavuruga kwenye usimamizi wa mitihani, na uchaguzi mkuu ujao. Serikali kama yuko humu ndani afikishe hizo taarifa kwa serikali wenzake kwani siyo nzuri sana kwa chama tawala na serikali yake.
 
sio tu swala la malimbikizo bali hata kiasi cha mshahara tunacholipwa ni kidogo sana ukilinganisha na kada nyingine this time serikali itaisoma namba na hao magamba wao walioko kwenye cwt piga chini wote.
 
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini wametanzaza mgogoro na serikali wakiwa na dhamira kubwa ya kugoma kama madai yao ya maingi hayatatimizwa ikiwa ni pamoja na nyongeza za mishahara kutokana na kupandishwa madaraja, malimvikizo ya madeni wanayodai serikali, fedha za likizo, fedha za uhamisho toka kituo kimoja hadi kingine, nk

Sasa nao wanaweza kugoma mda wowote kuanzia sasa.

Migomo ili iwe active inatakiwa timing, sasa wao wanagoma wakati shule zimefungwa ni mgomo au na wao wanaenda likizo? Walimu acheni maigizo
 
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini wametanzaza mgogoro na serikali wakiwa na dhamira kubwa ya kugoma kama madai yao ya maingi hayatatimizwa ikiwa ni pamoja na nyongeza za mishahara kutokana na kupandishwa madaraja, malimvikizo ya madeni wanayodai serikali, fedha za likizo, fedha za uhamisho toka kituo kimoja hadi kingine, nk

Sasa nao wanaweza kugoma mda wowote kuanzia sasa.

Sisi Serikali wengine posho zetu zikipunguzwa ili walimu waongezewe mishahara na sisi tutagoma dosama
 
Last edited by a moderator:
"Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa TZ (Tanzania); (Ajira mpya cheti) mwalimu Sh244,400, Afya Sh472,000, Kilimo/Mifugo Sh959,400, Sheria Sh630,000.
Diploma: Mwalimu Sh325,700, Afya Sh682,000, Kilimo/Mifugo Sh1,133,600, Sheria Sh871,500.

"Degree (shahada) Mwalimu Sh469,200, Afya Sh802,200, Kilimo/Mifugo Sh1,354,000, Sheria Sh1,166,000. Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivyo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na CWT kudai nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance (posho ya kufundisha), hardship allowance (posho ya mazingira magumu). Wape sms hii walimu 20 tu! Mshikamano daima.
 
Mnyika;tumefikishwa hapa na Bunge dhaifu iliyojaa magamba dhaifu kutoka chama tawala dhaifu inayoongozwa na m/kiti dhaifu anayeongoza serikali dhaifu, iliyojaza mawaziri dhaifu, waolioleta bajeti dhaifu na kuutetea kwa hoja dhaifu na mikakati dhaifu ya kumfukuza jasiri Mnyika anayewaambia ukweli kuwa wao ni wabunge dhaifu na Rais wao JK ni dhaifu.
Waalimu wafanye nini?
 
ikifika wakati wa bajeti ndio unasikia migomo,hawa watu ni watumishi maslahi hawa.rais wa tano hakubaliani na hali hii hata kidogo
 
Mnyika;tumefikishwa hapa na Bunge dhaifu iliyojaa magamba dhaifu kutoka chama tawala dhaifu inayoongozwa na m/kiti dhaifu anayeongoza serikali dhaifu, iliyojaza mawaziri dhaifu, waolioleta bajeti dhaifu na kuutetea kwa hoja dhaifu na mikakati dhaifu ya kumfukuza jasiri Mnyika anayewaambia ukweli kuwa wao ni wabunge dhaifu na Rais wao JK ni dhaifu.
Waalimu wafanye nini?

Mimi kama mtanzania wa kawaida sikubaliani na uropokaji kama wa mh.mnyika na huu wa mh.Aweda.
si kweli kwamba hakuna kilichofanyika hata kidogo,huku ni kukufuru mungu.
mnyika ni mchaga mpare amefaidi matunda ya uhuru hadi amechoka.
aweda ni mbulu,amefaidi matunda ya uhuru hadi amechoka....wamesoma kwa kodi za watanzania lakini wamejisahau sasa wameanza kujisaidia mezani ili wadogo zao wasifaidi kama wao walivofaidi.

mimi kama rais wa tano sikubaliani na mgomo wa walim kwani ni wadogo zetu ndio watakaoathirika,ndio tutakaowakomoa kwa kuwanyima haki zao.tuache chuki binafsi.
 
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini wametanzaza mgogoro na serikali wakiwa na dhamira kubwa ya kugoma kama madai yao ya maingi hayatatimizwa ikiwa ni pamoja na nyongeza za mishahara kutokana na kupandishwa madaraja, malimvikizo ya madeni wanayodai serikali, fedha za likizo, fedha za uhamisho toka kituo kimoja hadi kingine, nk

Sasa nao wanaweza kugoma mda wowote kuanzia sasa.
Sina imani na walimu! Ndiyo kada yenye wafanyakazi wasio na misimamo kushinda kada zote nchini. Hata wafagizi tu kwenye mataasisi wakiamua kugoma huwa wanakuwa serious lakini si walimu. Hawa ni kama mashamba boys au mahousegirls wa serikali. Kila kazi za kijinga zisizo na malipo mazuri wanapewa wao, kuandikisha sensa, kuandikisha wapiga kura, kusimamia uchaguzi na ujinga mwignine wote ambao una malipo ya 10000 kwa siku ndiyo wanapewa wao.

Hawa watu hawajui hata sheria na taratibu za malipo kwa watumishi wa umma, wapo wapo tu. I hate to be a teacher! Sijui ni kwanini niliingia kwenye kundi hili, and I am seriously struggling to get out of this career. Bora nikawa mfunga vidonda kuliko kula chaki!
 
"Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa TZ (Tanzania); (Ajira mpya cheti) mwalimu Sh244,400, Afya Sh472,000, Kilimo/Mifugo Sh959,400, Sheria Sh630,000.
Diploma: Mwalimu Sh325,700, Afya Sh682,000, Kilimo/Mifugo Sh1,133,600, Sheria Sh871,500.

"Degree (shahada) Mwalimu Sh469,200, Afya Sh802,200, Kilimo/Mifugo Sh1,354,000, Sheria Sh1,166,000. Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivyo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na CWT kudai nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance (posho ya kufundisha), hardship allowance (posho ya mazingira magumu). Wape sms hii walimu 20 tu! Mshikamano daima.

Hivi viwango si vya kweli,ni uongo na ni upotoshaji mkubwa.

viwango vya mishahara serikalini ni hivi hapa.

TGS A hadi C ni kiwango cha watumisha kwa watumishi wa serikali wanaoanza kazi bila kuwa na shahada. Hiyo TGS D ndo wale wanaoitwa maafisa pindi wanapoanza kazi ingawa hata wasiokuwa na shahada wanaweza panda toka A hadi G ambayo huwa ndio kiwango chao cha mwisho hawawezi kupanda zaidi ya hapo labda wawe wamepewa madaraka (sio cheo).

Kwa government system, mshahara wa TGD D huanzia around 470,000/= kwa mwezi na kwa TGD E huanzia 600,000. Hii haiwahusu walimu na madaktari. Kwa engineers wote including ARDHI degrees wao wanapoanza kazi huanzia na TGS E na kwa degree nyingine zote huwa wanaanza na mshahara wa TGS D upon first employment na Government. kwa wenye degree mshahara ya hupanda hadi kufikia TGS H amabapo ili kwenda TGS I, ni lazima upate cheo cha madaraka (i.e uwe mkuu wa idara, mkurugenzi etc, hii haiwahusu wakurugenzi wa mashirika ya umma yanayojitegemea kama tanesco, TBS, TANAPA, Ngorongoro TRA etc. wao wana mifumo yao ya mishahara ambayo ni mikubwa kuliko ya watumishi wa wizara za serikali na halmashauri ambao ndiyo wanaotumia mfumo wa TGS)

Unapokuja kwenye TGS I, hivyo ni viwango vya mishahara vinavotokana na madaraka km ukiwa mkuu wa idara serikalini basi mshahara wako ndo utaanzia na TGS I au ukiwa na cheo cha Principal, mshahara wako walau utaanzia na TGS I. Hao unaowasikia wakuu wa idara za wizara wote mishahara yao huanzia hapa ambao ni around 1,400,000/=.

Hope mpaka hapa utakuwa umepata mwanga kidogo.
 
Hii nimeisema sana na ninairudiaa tena, sijui ni nani ana organise hii migomo ya walimu na kivipi? Walimu wameshindwa kumtambua adui wao wa kweli (their true Enemy) na wanabaki wanatapatapa kama vile waingereza enzi hizo za mabadiliko ya viwanda (industrial Revelution) wakaishia kubomoa, kuvunja na kuharibu Mashine na viwanda wakihisi ndio maadui wao (wakashindwa)

Hili ndilo linalotokea kwa walimu (siwalaumu) wengi hawajui na wachache wanaweza kuwa wanajua ila hawajajua waanzie wapi ingawa sasa Tumaini lipo kuwa walimu wa level za juu wanazalishwa kwa wingi na hawa ndiyo wenye shauku (desire) ya mabadiliko, wanajaribu kumjua adui, ila awajajua kuviruka vikwazo (nitaandika siku moja kwa undani) ila leo niseme tu

Kwa ufupi walimu walimu wanajaribu kuangaika na matawi ya miti (kudai posho, nyongeza za mishara na vinginevyo) Bila kuangaika na mizizi/ chanzo cha mti wanaohitaji kuuondoa (kile kinachokwamisha wao kusikilizwa na kutendewa haki hata wakigoma).

Wanachopaswa kujua walimu ni kuwa kuongezwa kwa mishahara na kulipwa posho na madeni yote wanayodai si suluhisho, kama ndivyo itadumu kuwa hivyo milele (Kama wafanyiwavyo wazee wa iliyokuwa East Africa).

walimu wanahitaji chombo huru kitakachosimamia masilahi yao, kama vile walivyo wanasheria, madaktari, wahasibu na wengine wengi. Kwakiingreza twawezasema THEY NEED BOARD OF PROFESSIONAL na si tena Chama. madaktari wanaringa na wanasheria kwasababu wanabodi inayosimamia mambo yao ya taaluma yao, na hawaendeshwi na chama na wanasiasa ndio maana wakigoma wanagoma kweli tena katika umoja.

walimu wanapaswa wapiganie kuanzishwa kwa Board of Professionals huo ndio utakuwa msingi wa kuondoa ukiritimba katika Taaluma ya ualimu, watajipangia mambo yao, sheria zao na kila kitu bila kuingiliwa kama taaluma Huru. mkifanikiwa katika hili mtashuhudia mabadiliko makubwa, Tanzania haitakuwa tena na failuires kujiunga na ualimu, wala kila aliye maliza form 4, form 6 kuwa mwalimu, sheria zitaeshimika na vigezo vitakuwepo nani ni mwalimi nani siyo, hamtadharauliwa tena. huo ndio utakuwa mwanzo mpya wa Ualimu na Taaluma hiyo kwa ujumla.

HIVYO ADUI MKUBWA NITOKUWEPO NA CHOMBO CHA KUSIMAMIA TAALUMA HII (BOARD OF TEACHING PROFESSIONALS) MPAKA SASA, MKIWEZA HILI MTAKUWA KAMA MADAKTARI, WANASHERIA NA MAINJINIA, WAHASIBU NA PROFESSIONALS WENGINE.

WALIMU TAMBUENI HILI, NEEMA IPO KATIKATI YENU.
 
mimi kama mtanzania wa kawaida sikubaliani na uropokaji kama wa mh.mnyika na huu wa mh.aweda.
Si kweli kwamba hakuna kilichofanyika hata kidogo,huku ni kukufuru mungu.
Mnyika ni mchaga mpare amefaidi matunda ya uhuru hadi amechoka.
Aweda ni mbulu,amefaidi matunda ya uhuru hadi amechoka....wamesoma kwa kodi za watanzania lakini wamejisahau sasa wameanza kujisaidia mezani ili wadogo zao wasifaidi kama wao walivofaidi.

Mimi kama rais wa tano sikubaliani na mgomo wa walim kwani ni wadogo zetu ndio watakaoathirika,ndio tutakaowakomoa kwa kuwanyima haki zao.tuache chuki binafsi.

huna busara, huoni mbali na ni mjinga ndio maana hukupewa uraisi wa kwanza, umepewa uraisi wa tano..
 
Back
Top Bottom