Walimu mkoani mara wilaya ya bunda watemwa kwenye majina ya makarani wa kuhesabu watu na makazi ( se | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu mkoani mara wilaya ya bunda watemwa kwenye majina ya makarani wa kuhesabu watu na makazi ( se

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by laurentp, Aug 8, 2012.

 1. l

  laurentp New Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la kuhuzunisha sana kuona serikali yenye kulipa visasi na kuwaadhibu wale wote wanaothubutu kusema ukweli ama kudai haki zao za msingi.
  Hili linadhibitishwa na matukio mawili makubwa yaliyofatana,nayo ni mgomo wa madaktari na mgomo wa walimu.kwenye mgomo wa madaktari serikali inahisiwa kumuadhibu kiongozi wa mgomo kinyama(dk ulimboka) na kuwasimamisha kazi madaktari wengi. Na tukio la pili ni pale serikali kupitia wakuu wa wilaya kuwaadhibu waalimu wote walioshiriki mgomo kwa kuwaondoa katika zoezi la sensa.
  Je hii maana yake ni nini.
  1.serikali inaonesha dhahili kuwa yenyewe ndio chanzo cha migogoro na fujo
  2.serikali imesahau kuwa, hii ni serikali ya wananchi na si serikali ya viongozi
  3.serikali inaonyesha kutokuwa makini ktk kila jambo pale wanapowachukua vijana waliomaliza kidato cha nne na sita na wengine ambao bado ni wanafunzi mashleni na madereva bodaboda kuhesabu watu na makazi
  4.wameweka chuki na visasi mbele kuliko kuangalia uyakinifu na unyeti wa zoezi lenyewe na hasara itakayopatika kama kazi hii itaharibika.

  Mimi napenda kuhoji, hivi kikwete upo macho au umelala? Na unachotegemea ni nni.
  Kweli wananchi tumechoka.
  Kwa hali hii ni nni kinachotufanya tusiamini kama serikali imehusika na kumteka na kumtendea mambo ya kinyama dk ulimboka?
   
 2. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo, wale boda boda pale stand ya zamani, posta, yankiiz, CN, Nyasura etc wamepewa kazi ya kuhesabu watu? Kweli Bunda wilaya ya kazi.
   
 3. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Kwani ni lazima walimu watumike katika zoezi hili? kuna jeshi kubwa la vijana waliomaliza shule karibuni linaweza kutumika.
  Hata hivyo si walisema kuwa hawatoshirika kwenye sensa?? sasa imekuwa vipi? Iwapo mwenye shughuli hii ameamua kutumia raslimali watu nyingine tatizo nini? Hivi ni sawa kila kitu kulalamika?? YOU ARE DAMNED IF YOU DO AND YOU ARE DAMNED IF YOU DONT. Wacheni hizo jamani kwani kuna mambo mengi tu yanayotukabili na ambayo tunapaswa kuyapa kipa umbele.
   
 4. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Swala hapa sio walimu lazima wawepo, swala kwa nini wametolewa baada ya kufanya mgomo? je serikali imekuwa na tabia za mtu kuweka visa na visasi?
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nimekubali unaijua vizuri bunda kwa kutaja hayo maeneo na "Motto"wao wilaya ya kazi
   
 6. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  you seem to be too blind about the issue! SI serikali iseme ukweli kwamba imewaacha walimu kwa sababu ipi? kama umemsikia Pinda akijibu swali kuhusu hilo leo ungeona kuwa serikali inasema hili inafanya lile. shule zimefungwa zaidi ya mwezi kwa ajili hiyo halafu hakuna kitu.
   
 7. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  nionavyo mimi kuna watu wanamislead Rais wetu tena wanataka kumwangusha. Juzi tu alisema anawaheshimu sana walimu na kwamba yeye ni mtu wa kwanza kwa hilo. Basi walioamua kuwaondoa walimu wamemsaliti rais. Mbaya zaidi wanatoa porojo porojo tu. Rais aangalie vizuri huenda tatizo haliko kwa wapinzani pekee bali lipo ndani ya serikali katika ngazi za wilaya na mikoa na katika chama chake. Rais anaweza kufikiri wapinzani wanamsumbua kumbe kwa upande ndio wanaomsaidia zaidi. hawakukosea wahenga waliposema kikulacho ki nguoni mwako. Uamuzi wa kuwaondoa walimu bila sababu za msingi una negative impact ni bora kusingekuwa na mgomo kabla maana walimu wengeona ni mabadiliko ya kawaida tu.
   
 8. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  kwa nn shule zilifungwa. mipango ya serikari ya magamba haina mantiki. ni mambo ya itifaki na ukada.
   
Loading...