Walimu mkoa wa Morogoro tuna dukuduku; Tunadai posho ya kusahihisha mitihani ya 'Mock' tokea mwezi wa 6

Ruyama

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
367
561
Ninafurahi kujiunga na JamiiForums,

Niende moja kwa moja kwenye hoja,tulisahisha mitihani ya mock mwezi wa 6 baada ya hapo tukaambiwa tutalipwa mpaka leo tumedai kwa Afisa elimu kimya.
 
Ninafurahi kujiunga na jamii forum,niende moja kwa moja kwenye hoja,tulisahisha mitihani ya mock mwezi wa 6 baada ya hapo tukaambiwa tutalipwa mpaka leo tumedai kwa Afisa elimu kimya
Ifike mahala walimu mjitafakari na kujitathmini yaani kila siku hamuishi kulalamika hivi kwani hamna uongozi?
 
Kwahiyo umejiunga JF baada ya kuingizwa mkenge na Afisa Elimu wako? Nchi nyingine walimu ni mfano kwa raia hapa kwetu ni kinyume chake, tunakosea wapi!?
 
Tulikwenda mpaka ofisi ya Afisa elimu wa mkoa wakatwambia tusubirie mfumo wa malipo ufunguke yaani hadi leo hii tukiwakumbushia wanasema eti bado
 
Sawa
MwalimuKwani Taarifa Mlizonazo Wengine Wamelipwa
Maana Jamiiforums.com Ndiyo Ina Mpaka Mawaziri
Jieleze Vema Msaada Upo Jirani
Umeona Watendaji Wameitwa Ikulu Sasa Hivi Wanatembea Kifua Mbele Tupo Kwenye Light Track
 
Siku zote huwa najiuliza kwa nini mnasahisha mitihani kwa pesa? Hilo ni jukumu lenu kulingana na taaluma yenu. Kwa hiyo wanajeshi au polisi wakitaka wasafishe bunduki nao wadai kulipwa?
Acheni ujinga fanyeni bure hilo ni jukumu lenu mnatakiwa kulipenda.
 
Huu mtihani wakuu waliambiwa wawakipie wanafunzi ikiwa kila mwanafunzi analipiwa elfu 8 sasa jiulize mkoa mzima unawanafunzi wangapi,pesa hizo ni kwa kudurufu mitihani na usahihisha wa mitihani
 
Mkuu kuwa na subira , ni kweli mfumo Wa malipo tokea mwezi wa saba haujafunguka. Hata huku Handeni watu tunamadai mbalimbali ila mfumo wa malipo unasumbua
Tulikwenda mpaka ofisi ya Afisa elimu wa mkoa wakatwambia tusubirie mfumo wa malipo ufunguke yaani hadi leo hii tukiwakumbushia wanasema eti bado
 
Siku zote huwa najiuliza kwa nini mnasahisha mitihani kwa pesa? Hilo ni jukumu lenu kulingana na taaluma yenu. Kwa hiyo wanajeshi au polisi wakitaka wasafishe bunduki nao wadai kulipwa?
Acheni ujinga fanyeni bure hilo ni jukumu lenu mnatakiwa kulipenda.
 
Siku zote huwa najiuliza kwa nini mnasahisha mitihani kwa pesa? Hilo ni jukumu lenu kulingana na taaluma yenu. Kwa hiyo wanajeshi au polisi wakitaka wasafishe bunduki nao wadai kulipwa?
Acheni ujinga fanyeni bure hilo ni jukumu lenu mnatakiwa kulipenda.
Chizi maarifa wewe! Ungeuliza ufafanuliwe kuliko kuleta haya mashudu.
 
Mkuu kuwa na subira , ni kweli mfumo Wa malipo tokea mwezi wa saba haujafunguka. Hata huku Handeni watu tunamadai mbalimbali ila mfumo wa malipo unasumbua
Eti mfumo haujafunguka! Kwani unajigungua wenyewe ?
So ukijifungua mwaka 2050 kwa wahusika ni sawa tu?
 
§Walimu tuna hali ngumuu..Walimuu
..tutajazua kitimtimuu..Walimuu.
..hadi wizara ya Elimuu..Walimuu
..nasi tuna majukumuu..Walimuu..
..Walimu.. Walimuu..Walimuu..§
Mwalimu kilio chako bila shaka kimesikika sababu Serikali Sikivu imo humu na wamekusikia..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
 
Nafikiri hujaelewa! Ni vema ukaulizwa ueleweshwe!

Kuna kazi za ndani zinazomhusu mwalimu kwa mujibu wa mkataba wake, atafundisha, atatoa mazoezi na mitihani katika darasa lake na pia ataisahihisha.

Mock na NECTA ni mitihani ya nje, hivyo mwalimu akiitwa kusahihisha ni lazima alipwe maana hiyo ni 'extra duty'

Askari analazimika kutimiza majukumu yake ya ndani, nae akitoka nje analazimika kulipwa, kwa mfano wanaolinda bank, au wakitoka nje ya kituo chake/wilaya.

Mwalimu Mstaafu.
Siku zote huwa najiuliza kwa nini mnasahisha mitihani kwa pesa? Hilo ni jukumu lenu kulingana na taaluma yenu. Kwa hiyo wanajeshi au polisi wakitaka wasafishe bunduki nao wadai kulipwa?
Acheni ujinga fanyeni bure hilo ni jukumu lenu mnatakiwa kulipenda.
 
Ninafurahi kujiunga na jamii forum,niende moja kwa moja kwenye hoja,tulisahisha mitihani ya mock mwezi wa 6 baada ya hapo tukaambiwa tutalipwa mpaka leo tumedai kwa Afisa elimu kimya
Walimu wa Tanzania mmezidi unyonge na mbaya zaidi hamna umoja ndani na wengi wenu ni wanafki na mamluki wa serikali.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom