Walimu mishahara yao inapanda kwa kasi zaidi - waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu mishahara yao inapanda kwa kasi zaidi - waziri

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mizambwa, Feb 13, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Waziri: Mishahara ya walimu inapanda kwa kasi zaidi

  Saturday, 11 February 2012 09:22


  SERIKALI imesema kuwa mishahara ya walimu imekuwa ikipanda kwa kiasi kikubwa kuliko watumishi wengine nchini.Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia alisema kuwa walimu wamekuwa wakipandishiwa mishahara kila mwaka na kwamba kiwango cha upandishaji kinatofautiana na watumishi wa kada nyingine.

  Ghasia alisema katika kipindi cha mwaka 2005 hadi mwaka 2011, kiwango cha upandaji wa mishahara kwa walimu kimekua kwa asilimia 12 na 12.4 kwa mwaka wakati kada nyingine mishahara iliongezeka kwa asilimia tano hadi 12.6 kwa mwaka.

  Katika swali la msingi Seleman Jafu (Kisarawe-CCM) alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kushughulikia tatizo la mishahara kwa walimu ambayo imekuwa haipandi mara kwa mara na kufanya walimu wawe na ugumu wa maisha.
  Mbunge huyo alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuwasaidia walimu wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa vya usafiri.

  Waziri alifafanua kuwa mwaka 2005, mwalimu wa daraja la tatu ‘A’ alianza na mshahara wa Sh 74,570 ambapo kwa sasa mwalimu huyo anaanza na mshahara wa Sh244,400 kwa mwezi.

  Kwa mujibu wa Ghasia, walimu wa Stashahada walianza na mshahara wa Sh108,800 na sasa wanaanza na Sh325,700 wakati walimu wa shahada walikuwa wakianza na mshahara wa Sh140,000 lakini kwa sasa wanaanza na mshahara wa Sh449,200 kwa mwezi ambalo ni ongezeko la asimilia 235.14.

  Kuhusu posho za walimu za kujikimu pamoja na usafiri kwa walimu wanaokwenda katika mazingira magumu, alisema serikali imeboresha mazingira yake ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo kulingana na mishahara yao.


  CHANZO: GAZETI MWANANCHI 11-02-201


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 2. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Dah! haya bwana fumbo amfumbie mjinga inapanda lakini bado haijafikia kwenye wizara zingine mfano afya mwenye degree ya nursing yuko juu sana kuliko mwl. mwenye degree pia.
   
 3. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ishu sio kupanda kwa kasi angeweka bayana awali walikua wanalipwa kiasi gani na ss hivi wanalipwa kiasi gani,hivi mtu kumlipa 80,000 na ukawa kila mwaka unapandisha 25,000 utajisifia?boresha walipwe vizuri kama kada zingine kama utaona waalimu wanauza ubuyu.ukwaju,maandazi,vitumbua,barafu n.k
  Tunashuhudia hii fani serikali imewadharau sana na kufanya maisha ya waalimu kuwa magumu sana na wengi wao wanakua na madeni sana mitaani kiasi inafikia mshahara ukitoka unaishia kwenye madeni tu
  Mishahara ya wakubwa haipandi kwa kasi ila once ukipanda ni mara 10 ya kiwango cha mwalimu ulivyopanda.
   
 4. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna transport allowance,risk allowance,hardship allowance,meal allowance,house allowance,bidhaa zinapanda bei kila baada ya sekund,unategemea nini,hayo majibu ya kuwapa mbuzi sio walimu,shame 2 your family.
   
 5. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waziri naona amelidanganya BUNGE,nashangaa kwa nini wabunge hawakuendelea kuhoji zaidi hayo majibu ya waziri.Au wabunge wanasubiri walimu wagome ndio waanze kuomba kuwasilisha hoja binafsi?Kimsingi ktk tz kuna ubaguzi wa hali ya juu sana kwenye uwiano wa mishahara kwa watumishi wa umma.Ni zaidi ya miaka 5 tangu serikali ilipoongeza vyuo kwa ajili ya kuzalisha walimu ili kuondoa upungufu uliopo kwenye shule zetu,lakini tatizo la upungufu wa walimu ktk shule zetu bado liko palepale.Hii inadhihirisha kuwa tz kuna walimu wa kutosha ila wanakimbia fani ya ualimu.Mwaka jana serikali iliajiri walimu,walimu wengi kati hao walipofika kwenye hizo halmashauri walizopangiwa walichukua posho za kujikimu na kukimbilia kusikojulikana.Sasa serikali ijiulize kwa nini hao walimu wakimbie?Kwa nini watumishi kwenye kada zingine kama BOT,TRA,PPF,NSSF,Migodini,wizarani,Tanesco,n.k kusiwe na upungufu?Bila shaka serikali ina majibu ila inajifanya kiziwi na ikaamua secta ya elimu iwe likizo kwa muda usio na kikomo.Huo mshahara uliokuwa unatolewa kabla ya 2005 ulikuwa na thamani kubwa kuliko huu unaotolewa sasa hivi na hii ni kutokana na mfumuko kubwa wa bei ambayo serikali yetu imeshindwa kuthibiti.Serikali itaendelea kushuhudia matokeo mabaya kwenye matokeo ya mtihani kwani walimu wapo kwenye migomo baridi hadi hapo serikali itakaposikiliza madai yao.
   
 6. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Hawa mawaziri wetu bana..,they will never stop to surprise me. You
  wonder if they have ever seen the inside of a class room (I know most of them did go to school but I doughty if learnt something

  ...I say they will never stop to surprise because the good walimu are asking for pay rise and this Minister whatever is name is talking about salary growth... incremental amount that is high for teachers when compared to other civil servant...the question is how much them teachers are getting now and whether it make sense as far as their work/life is concerned?

  Anyway I guess we have to get used these kind of arguments as the other day I head that this administration has generated more MW than any of the previous government combined!
   
 7. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Hakuwa hata na uso wa aibu alipokua anayasema hayo?
  Mawaziri wetu kwa kweli, ni comedy tu kwenye maisha ya watu. Eti mshahawa wa mwalimu unapanda sana kuliko kada nyingine. Kweli?
   
 8. M

  Malolella JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nikweli mshahara wa mwl unapanda kwa kasi japo bado hautoshi. Mdogowangu kaanza 2008 kwa 165,000 sahvi analipwa 392,000.
   
Loading...