Walimu kugoma... Kuna kikundi kinaendesha kampeni ili kuivuruga serikali- Majaliwa. Ukweli ni huu ha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu kugoma... Kuna kikundi kinaendesha kampeni ili kuivuruga serikali- Majaliwa. Ukweli ni huu ha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SG8, Jun 29, 2012.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  Nimechukizwa sana na kauli ya Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Kassim Majaliwa.

  Majaliwa, kiongozi wa zamani wa CWT amesema kuna kikundi kinaeneza propaganda za kuhamasisha Walimu wagome kwa kutumia vyombo vya habari. Ameshauri Walimu wasiunge mkono mgomo huo na kwamba CWT ipo kwenye majadiliano.
  Ukiacha tukio la kuumizwa kwa DK Ulimboka hii ni habari nyingine iliyoniharibia siku yangu

  Baaada ya saa 2 kutoka sasa nitaweka hapa mpango mzima wa CWT na malalamiko ambayo yamemfikia hadi JK lakini hakuna hata mmoja aliyeonyesha nia ya kuwasikiliza Walimu.
  Document hiyo nimepewa na rafiki yangu ambaye ni Kiongozi wa CWT Mkoa mmojawapo..

  Uongo wa mchana kweeeppppee
   
 2. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walimu gomeni, gomeni.
  Kugoma inawezekana....
  Msikubali kuitwa na kuonwa waoga kila siku, haiwezekani nyie vita yenu na serikali ni kulipwa malimbikizo ya mshahara.
  Mshahara wenyewe laki tatu. Lak 3?
  Unaishije?
  Au nyie ni certified TZ11 users?
   
 3. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkigoma mtaungwa mkono nchi nzima.
  Hamuwezi kuanza wote
  wengine wanajoin wakiona moto unakolea.
   
 4. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  huyo jamaa nimemsikia nadhani ana ubongo wa samaki hivyo ameshindwa kabisa kuona hatari ya kauli yake. Wanasubiri mambo yaharinike ndipo wakurupuke na kauli zao za kijinga,ina maana hajasikia matamko ya cwt mikoa mbalimbali ,km yeye anashiba kodi za watanzania awaache nao wadai haki zao
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  tunaomba walimu mtimize adhma yenu ya kugoma ili mpate stahiki zenu.
   
 6. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  uwezo wa kugoma tunao, sababu ya kugoma tunayo na nia ya kugoma tunayo TUNATAKA SERIKAkLI ITUELEWE HIVYO.
   
 7. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  umepanda lini.? ulikua laki na hamsin.!
   
 8. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa.kuna kikundi kingine pia kinajaribu kuwaambia watanzania kuwa wana maisha magumu wakati wote tunakula kuku kwa mrija..ivi kiongozi wa ccm ni mpaka uwe na kauli ziso na mantiki hivi??kwani kuna mtu anahitaji kuingizwa darasani aeleweshwe kuwa mshahara wa mwalimu hauwezi kutosheleza hata yale mahitaji muhimu ya kila siku??na huu mfumuko wa bei "made in ccm"??..
   
 9. Judi wa Kishua

  Judi wa Kishua JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 525
  Trophy Points: 180
  Walimu mkigoma itabidi mkaguliwe vyeti vyenu,nyie danganyweni tu.
   
 10. s

  sisala Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kugoma kupo pale pae hata majaliwa na ofisi yake wafanye kitu gani, haiwezekani nchi moja kiwango cha elimu kimoja
  tofauti ya mishahara kubwa kiasi hiki.
   
 11. s

  sisala Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  siyo kila mwalimu ana chet feki kama unavyofikiri wewe, wengine wana cv nzuri kuliko wale wanaopata mishahara ya
  kinyonyaji, subiri uone kama watagoma au la afu useme wameogpa vyeti vyao. unapotoa comment uwe na moyo wa kizalendo kuona wenzako wananyanyasika ndani ya nchi yao,
   
 12. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nawashauri walimu wagome manake serikali hii ya wadanganyika imelowea na inafkiri wao ndio wakufaidi matunda ya nchi hii na wawe na msimamo kamili bila ya kuteteleka.
   
 13. O

  Original JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  waalimu wakianza mgomo wao na mapolisi pia wanaandaa mgomo wao.
   
 14. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tobaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 15. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  si wewe tu ila hata mimi nimeumia sana na kauli ya Majaliwa. Naomba vyombo vya habari waendelee kutangaza ili siku chache zijazo majaliwa aje aibike, Kwa taarifa mimi ni mwalimu mpango huu upo na inawezekana ni kuanzia tarehe saba mwezi wa saba. tarehe ambayo kilizaliwa TANU. waraka umesambazwa kila shule. Madai yetu ni nyongeza ya asilimia 100, posho ya kufundishia 55% mazingira magumu 30% serikali waliombwa kwenye majadiliano tangu mwezi wa nne ili ikiwezekana madai hayo yaingizwe kwenye bajeti serikali ikagoma kwenda kwenye baraza la majadiliano, rais kapewa taarifa lakini hakufanya hivyo, kwa vile tu wanaamini walimu ni wanyonge. Safari hii lazima kieleweke. Kwa maelezo ya Majaliwa amewadharau viongozi wa chama cha walimu kwani ndiyo walioandaa mpango mzima. Na kama watakubali kusitisha mgomo huu CWT waachie ngazi lakini walimu tuunde jumuiya ya walimu kuliko dharau hii ya makusudi ya viongozi wa serikali. pia wananchi acheni kutoa kashfa dhidi ya walimu. walimu ni muhimu sana tofauti na mnavyodhani. Wito kwa vyombo vya habari tangazeni kwa nguvu na mkitaka waraka huo utafuteni kwenye shule yoyote ili ikiwezekana utolewe magazetini ili umma ujue kuwa si kikundi cha watu wachache bali ni walimu wote hakika tumechoka kupuzwa na kudhalilishwa. Kwa walimu waoga tafadhali ondoeni uoga wa kipuuzi vinginevyo tutaendelea kupuuzwa na kunyanyaswa. Nani asiyepitia mikononi mwa mwalimu akawa na mafanikio?
   
Loading...