Haludzedzele
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,468
- 529
Kweli ualimu wito sio ajira mana watu wanafanya wanavyotaka tuu, nakatishwa tamaa sana na hii kada ya ualimu kimsingi Walimu wa kigoma manispaa tulioajiriwa 2012 hatujapewa barua za kupanda madaraja mpaka sasa ijapokuwa wenzetu wa halmashauri zingine wameshapewa barua za kupanda daraja kuanzia Kigoma vijijini,Kasulu na Kibondo ukiachilia mbali mikoa mingine mingi kama Geita waliopandishwa mwaka jana Kahama mapema mwaka huu Makete nk.
Kuona hivyo tukashtuka na kuanza mikakati ya kufahamu ni kwanini sisi tuu manispaa tukaenda TSD wakasema mwaka 2015/16 hatumo kwenye bajeti hiyo ambayo kimsingi ndio bajeti yetu kwenda kwa Afisa utumishi majibu hayo hayo mmmmm kwenda kwa Mkurugenzi nae majibu hayo hayo tena kwa nyodo tumeona huko kote kumegota leo tumeenda kwa Afisa Elimu Mkoa nae anasema hana majawabu labda tumsubiri Katibu tawala mkoa ambae yupo kwenye uwashaji Mwenge Morogoro hivyo mtetezi hasa ni nani iwapo walimu hawapati stahiki zao?
Nimepata kizungumkuti sana leo hasa nchi ni moja mwaka wa kuajiriwa ni mmoja iweje kuwe na mambo kama haya? kimbilio letu hasa ni wapi? tumesimama kidete kuhakikisha hatuendelei kuchezewa kama wanavyotaka kwa kufahamu haki haiombwi bali hutafutwa na ikibidi hulazimishwa kupatikana. Kwakweli wanajamvi hasa jukwaa hili ambalo linahusu moja kwa moja kada yetu tupeane ujanja ni namna gani tunaweza kwenda sawa na waajiri wasiotambua stahiki za watumishi wao japo kwa Kigoma Manispaa mimi sidhani mana pameoza sana hawana utu kabisa.
Mwenye namba ya Waziri TAMISEMI naomba pamoja na Naibu wake labda baada ya ngazi zote ni kunyooka tuu kwa hawa kazi tuu inawezasaidia kwa kiasi fulani. Tushikane mikono jamaani haya ni maisha yetu sote ahsanteeni na poleni kwa kusoma andiko lefu baada ya hapa mtasikia tuu kinachoendelea!
KARIBUNI KWA MAWAZO