Walimu Halmashauri ya Wilaya ya Masasi hatujalipwa madeni yetu.

Mkulia

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
375
95
Kama mtakumbuka,serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa ya kulipa madeni ya watumishi ikiwa ni pamoja na madeni ya walimu. Madeni hayo yamekuwa yakilipwa baada ya kufanyiwa uhakiki na timu ya wahakiki wa Halmashauri husika na labda ikishirikiana na viongozi wa juu wa wizara (TAMISEMI). Taarifa iliyopo ni kuwa serikali imeshamaliza kulipa madeni yote ya watumishi. Binafsi sina uhakika sana hili lina ukweli gani.

Katika Halmshauri ya wilaya ya Masasi (Masasi DC) jumla ya walimu waliolipwa madeni yao ni wanne tu,kati ya hao mmoja ni mwalimu wa sekondari na watatu ni wa msingi na wamelipwa jumla ya Tsh 911,000/= (Laki tisa na kumi na moja elfu) tu.

Kiuhalisia walimu tunaodai ni wengi mno lakini Mwajiri (DED),wakuu wa Idara na Mkaguzi wa ndani (Internal auditor) waliamua sina uhakika kwa utashi wao au vipi kupeleka majina ya walimu hao wanne TAMISEMI kwa ajili ya malipo na kuwaacha wengine wengi. Huu ni unyanyasaji mkubwa!

Baadhi ya walimu (mimi nikiwamo) tulijaribu kufuatilia kwa Mkuu wa idara (DEO) na Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT) kujua sababu ya kutolipwa madai hayo,majibu tuliyoyapata ni kuwa hatukuwa na viambatanisho katika barua zetu za madai jambo ambalo siyo la kweli. Kwa mfano binafsi ninadai pesa ya uhamisho na gharama za masomo na madai yote hayo niliweka viambatanisho lakini sijalipwa kwa madai kuwa barua zilikosa viambatanisho. Ninaamini viambatanisho hivyo vilinyofolewa katika majalada yetu na kutupwa labda kwa manufaa ya mwajira au mhakiki.

Kwa ujumla hali hii ya unyanyasaji wa walimu imekithiri sana katika Halmashauri yetu ya Masasi na hakika inashusha moyo wa utendaji kazi kwa walimu. Tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuiitupia macho Halmashauri hii na kuhakikisha kuwa watumishi wote ikiwa ni pamoja na walimu tunalipwa madeni yetu kwani ni haki yetu na siyo fadhila.

Ninatoa RAI kwa TAMISEMI waje kuhakiki madeni hayo upya wao wenyewe na kamwe wasiache kazi ya uhakiki ifanywe na DED na wakuu wa Idara kwani inaonesha hawana nia njema na watumishi wao. Tafadhali hili siyo jambo la kupuuzia kwani linaumiza walimu wengi na kushusha moyo wa utendaji kazi. Elimu Halmashauri wilaya ya Masasi inazidi kushuka kwa kasi ya ajabu sana na chanzo ni mambo kama haya. INAUMA SANA! Sijui ni kwanini kada hii watumishi wake tunadhalilishwa hivi. Hata haki zetu inakuwa shida kuzipata.
 
Nakushauri mwalimu nenda moja kwa moja kwa Mkurugenzi kaongee nae uone anasemaje huenda hela imeliwa hapo hapo,tatizo la kutolipwa madeni limekuwa sugu pia Mbozi,japokuwa wanalipa wachache.Mbinu mbadala nenda kashinde palepale Bomani(kama si mwoga) ni mbinu aliyotumia jamaa yangu na kulipwa ndani ya mwez mmoja,binafsi next week ntalianzisha hilo timbwili
 
Nakushauri mwalimu nenda moja kwa moja kwa Mkurugenzi kaongee nae uone anasemaje huenda hela imeliwa hapo hapo,tatizo la kutolipwa madeni limekuwa sugu pia Mbozi,japokuwa wanalipa wachache.Mbinu mbadala nenda kashinde palepale Bomani(kama si mwoga) ni mbinu aliyotumia jamaa yangu na kulipwa ndani ya mwez mmoja,binafsi next week ntalianzisha hilo timbwili
Ninashukuru kwa ushauri wako. Binafsi niwewahi kufika kwa DED kufuatilia hili na akaahidi kulipa deni langu lakini orodha ya wanaostahili kulipwa ilipotolewa jina langu halikuwepo. Huku tumeshaanza mchakato wa kulifuatilia hili bila shaka kitajulikana tu. Juu ya woga huo haupo hasa ukizingatia kuwa ninachofuatilia ni haki yangu.
 
Back
Top Bottom