Mjukuu wa Sechenga
Member
- Nov 13, 2015
- 34
- 37
Leo hii Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Ezekiel Olouch kamuibukia waziri Ndalichako, amesema upangaji matokeo ya kidato cha nne kwa mfumo wa divisheni uliofanywa na Wizara ya Elimu, ni batili na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako anatakiwa kushtakiwa. Hivi hawa CWT kazi yao nini? Maana kila mwezi wao wanachukua chao mapema kwenye mishahara ya walimu na marejesho hayajulikani. Kero za walimu zinajulikana lakini hadi leo hakuna kinachofanyika kilichobaki wanachukua hela kwa ajili ya kulipana posho na mishahara, walimu amkeni hawa si watu wa kutetea haki zenu ipo haja ya kuliangalia upya vinginevyo mtaishia kupata tisheti za CWT tu. Hili ni jipu Ndalichako litazame upya vinginevyo walimu wataendelea tu kunyang'anywa kidogo chao mwisho wa mwezi.