Walimu 8 wakamatwa kwa kujihusisha na mapenzi na wanafunzi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi.

Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013.

Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel.

Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.

Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size).

Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.

“Ni fedheha na haivumiliki kuona walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.

Amri hiyo ilitekelezwa mara moja kwa walimu hao kuwekwa chini ya ulinzi.

Mulongo pia alimwagiza Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani kuwaandikia barua za onyo walimu wa kike shuleni hapo kwa kushindwa kulinda na kutetea masilahi ya wanafunzi wa kike waliokuwa wakidhulumiwa kingono na walimu wenzao kiasi cha baadhi yao kuathirika kisaikolojia.

Pia, alimwagiza Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Khamisi Maulid kuangalia uwezekano wa kuwahamishia shule nyingine wanafunzi waliodhulumiwa kingono na walimu wao ili kuwaepusha na matatizo ya kisaikolojia.

Maulidi alisema wanafunzi walioathirika zaidi ni wale wa kidato cha nne.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Mwanza, Said Mselem alisema kitendo hicho kimeifedhehesha taaluma ya ualimu na kuahidi kuwa ofisi yake itatanua wigo wa uchunguzi hadi kwenye shule nyingine.
 
Hili tatizo ni kubwa. Kwa shule nyingine wanafunzi wenyewe wako macho juu wala hawaathiriki kisaikolojia tena wanafanya siri kubwa na walimu wa kike wakijaribu kufatilia wanawachukia na kusambaza malalamiko kuwa walimu wa kike ni wabaya
 
Alafu unategemea wanafunzi wafaulu!

Kuna jamaa alikuwa rafiki yangu ni mwalimu kumbe kitambo alikuwa anatoka na mtoto wa uncle alafu mimi sijui, nilipokuja kugundua nikakata ubest kabisa,nilitaka kumpeleka polisi lakini nikamwonea huruma
 
Usemalo ni kweli ila mpaka tatizo likomae kiasi icho hao waalimu wa kike wasingejali wao kuchukiwa ila hata kwa siri wangetoa taarifa izo,nao wanastahili adhabu kabisa maana mwalimu ni mlezi walipaswa kuwalinda hao watoto.
 
Sasa wao wale wapiiiii? Walimu wanaonewa tuuuu nchi hiiii basis tuuuuuu

Ilo sio jibu kabisa maana hata kama wewe ni kijana iko siku utakua mzazi na hautafurahi mwanao kupotezewa malengo ya kusoma na mwalimu wake ambaye ndo anayetambua umuhimu wa elimu kwa mtoto.
Ilo nalo ni pepo tu hao waalimu wawajibishe alafu maombi watajifanyia wenyewe baada ya kupata adhabu.
 
Alafu unategemea wanafunzi wafaulu!

Kuna jamaa alikuwa rafiki yangu ni mwalimu kumbe kitambo alikuwa anatoka na mtoto wa uncle alafu mimi sijui, nilipokuja kugundua nikakata ubest kabisa,nilitaka kumpeleka polisi lakini nikamwonea huruma

Ulikosea ungemfunza adabu maana ualimu sio kazi ya kujitolea ni ajira kama ajira zingine ,na kama mwalimu unaona una udhaifu kwa wanafunzi badilisha kazi au oa umshonee mkeo uniform ,sio kutuharibia watoto wetu.
 
Ilo sio jibu kabisa maana hata kama wewe ni kijana iko siku utakua mzazi na hautafurahi mwanao kupotezewa malengo ya kusoma na mwalimu wake ambaye ndo anayetambua umuhimu wa elimu kwa mtoto.
Ilo nalo ni pepo tu hao waalimu wawajibishe alafu maombi watajifanyia wenyewe baada ya kupata adhabu.
Ndugu kwani una uhakika wamewala? Hata kama wamewala ndo watafeli? Wakifeli shule ndo wamafeli maisha? Halafu,je,walikuwa hawajaliwa kabla ya hapo?
 
Ulikosea ungemfunza adabu maana ualimu sio kazi ya kujitolea ni ajira kama ajira zingine ,na kama mwalimu unaona una udhaifu kwa wanafunzi badilisha kazi au oa umshonee mkeo uniform ,sio kutuharibia watoto wetu.
Huyu jamaa ndio kwanza alikuwa anaanza ajira,nikaona niwahurumie wazazi wake tu kwasababu ndio wanamtegemea!
 
Hili ni tatizo kubwa sana kwenye shule nyingi hapa nchini, serikali ilitafutie ufumbuzi maana inauma sana kwetu tunaosomesha watoto na unaweza ukajikuta unaua mwalimu bure kutokana na ushenzi wanaofanya kwa watoto wetu tena kwa kuwalazimisha na kuwapiga viboko wanapokataa kitu ambacho watoto was kike kinawafanya wachukie shule kama si somo la mwalimu husika. Na hizi neo sababu za watoto wa like kutofanya vizuri darasani na hats kuacha shule kabla ya kuhitimu.
 
Back
Top Bottom