Walimu 10, 000 kuajiriwa kabla ya disemba, zoezi hilo kufanywa na tume ya utumishi wa walimu badala ya wizara

Jensen salamone

JF-Expert Member
Sep 28, 2019
316
1,000
WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo inasubiri kibali cha kuajiri walimu 10,000 kabla ya Desemba, mwaka huu.

Akizungumza mjini Dodoma jana, Ummy alisema itakuwa mara ya kwanza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) itahusika kuajiri walimu hao badala ya wizara.

Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa baraza jipya la wafanyakazi wa tawi la Tume ya Utumishi wa Walimu lililohusisha wajumbe 58 ambao ni wawakilishi wa wafanyakazi 516 wa tume hiyo waliopo katika halmashauri mbalimbali nchini.

“Hivyo tume inatakiwa kujiandaa kuajiri mwaka huu kwani Tamisemi inategemea kupokea kibali cha kuajiri walimu 10,000 kabla ya Desemba, mwaka huu,” alisema Ummy.

Alisema TSC itaajiri walimu baada ya wizara kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwa kuweka vigezo vya kupata walimu wanaostahili.

Alisema miongoni mwa vigezo hivyo ni pamoja na kutumia fomula nzuri ambapo kila halmashauri au jimbo lipate walau asilimia 20 ya walimu wa eneo hilo na wengine kutoka maeneo mengine.

Ummy alisema halmashauri za pembezoni zitapewa kipaumbele ili zipate walimu kutokana na kuwa na uhaba mkubwa kuliko maeneo ya mjini.

Alitoa wiki mbili kwa tume hiyo hadi Septamba 21 iwe imekusanya takwimu katika halmashauri 139 na kupeleka orodha ya mahitaji ya walimu waliopo na upungufu uliopo.

Alisema hajazuia walimu kuhama ila ameitaka TSC itoe vibali vya uhamisho walimu wahame kutoka kwenye majiji na kwenda vijijini na si kutoka vijijini kwenda mijini.

“Mwalimu akitaka kuhama kutoka jiji kwenda mikoa ya Kigoma, Katavi, Simiyu na Rukwa apewe kibali mara moja,” alisema.

Ummy pia aliiagiza tume hiyo ianzishe mfumo wa kudhibiti utoro wa walimu kwa kuweka mashine ya kubofya katika majiji sita ya Mwanza, Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Dodoma na Mbeya na baadaye utaendelea katika mikoa mingine.

Chanzo: habari leo

My take: vijana anzeni kutafuta konekisheni kwa makatibu wa tume ya utumishi wa walimu maana ajira zinaenda kuuzwa
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,801
2,000

Utoro sio sababu kuu ya elimu kushuka ila motisha na mazingira ya kazi ya waalimu ndo sababu kuu. Boresheni kwanza ndo muweke hizo machine zenu za kubofya
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,433

Bi waziri, Kwa nini halmashauri za pembezoni zina uhaba mkubwa wa waalimu kuliko za mjini? Mtaajiri sana na bado tatizo litakuwa palepale!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom