Walikuwa wapi wanablog wa Tanzania wakati wa sakata la Max?

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,053
4,595
Habari za asubuhi wana JF family,

Awali ya yote nataka kuwapa pole Max na Mike pamoja na kundi nzima la watendaji wake wa Jamii Forums wanachama wenzangu wa JF. Nia yangu si kuwalaumu watu la, bali kutaka kujua kama kitu gani kiliwafanya wana blog mahiri wa Tanzania na waendesha mitandao kulikalia kimya suala la mwanahabari mwenzao wa mitandao Max.

Kuna watu wanajiita mpaka ma queen na ma king wa mitandao Tanzania lakini sikuona juhudi zozote za kulipigia kelele suala la mwenzao kunyanyaswa kwa makosa yasiyokuwa na mikono wala miguu. Nitataja baadhi ya majina ya mitandao mikubwa kama Michuzi Blog, hii ni blog kubwa sana na inayotembelewa na watu wengi sana hapo Tanzania na nje ya nchi, kwa wiki nzima wakati hili sakata la Max likiendelea nilikua najitahidi kupitia huko kuangalia kama nitaona chochote kitu kuhusu hii kesi, lakini sikufanikiwa zaidi ya kuona sifa za viongozi wa serikali.

Mange Kimambi, huyu alijitahidi lakini nina wasiwasi na uandishi wake kama kweli ulikuwa wa kumuonewa huruma Max na uhuru wa habari kama anavyotaka tumuamini ama ilikua kuchukua fursa ya kesi ya Max kumalizia hasira zake kwa Serikali kwasababu anazozijua mwenyewe. Kwangu mimi japo Mange simjui zaidi ya kupewa namba yake ya simu na mke wangu ili niwasiliane naye kuhusu biashara anayoifanya ya kuuza nywele za waliokufa simjui na spendi kumfahamu pia. Kwanini nasema Mange si mtetezi wa uhuru wa kusema, sababu kubwa ni moja Mange hana tofauti na huyo anayemsema kuwa anaminya uhuru wa habari. Mange katika social media zake zote ukitaka kubaki kama member wake unatakiwa uwe ndiyo mama ama siyo unapewa ban la mwaka hivyo hana tofauti na serikali ya Magufuli.

Lemutuz, sina unahakika sana sababu mimi si mtembeleaji wa site yake na najua yupo hapa anaweza kuja kujitetea kivyake lakini sina hakika kama kweli atakua amejitahidi kuitangaza hii kesi kama tunavyotaka iwe kwa kuzingatia kuwa yeye ni King of social Media.

Clouds, hawa najua siwezi kutumia muda wangu mwingi kusema maana wenzetu wapo kwa maslahi yao zaidi japo ni wajasiriamali vijana lakini utu wao umenunuliwa na uroho wa utajiri zaidi kuliko kuhudumia watu.

Majidi Mjengwa, sina hakika pia kama alijitosa kuwasaidia wanahabari wenzake katika kuitangaza hii kesi ya Max, kama alifanya hivyo natanguliza samahani na ningeomba wanaojua kama alifanya hivyo wanisaidie kutoa maoni yao hapa.

Inatia aibu kubwa sana kuona magazeti kama ya Tanzania yalikaa kimya hasa ya wale tunaowaita wana mageuzi ama UKAWA nao walikaa kimya kulikemea hili suala la kubana uhuru wa kusema na kujadili mambo ya maendeleo ya Taifa letu. Niliona kikundi cha watu wakifanya Press Conference na kuishinikiza ama kuipa serikali masaa 48, watu kama hawa huwa najiuliza kama kweli wana akili timamu ama wana agenda zao za siri? Maana sikuona juhudi zozote walizozifanya zaidi ya wakili wake JF.

Ningependa kuwaandika wengi hapa lakini si juu yangu kuwa hukumu watu lakini ni juu yangu kama raia mpenda haki kuwatuhumu watu kama hawa ambao wajibu wao ni kutuwakilisha kufikisha ujumbe ndani na nje ya nchi ili dunia itambue nini kinachoendelea hapa nchini kwetu. Kutangaza ubovu wa serikali ya nchi si kosa, maana kama sisi tutashindwa kuwakemea viongozi wetu labda majirani na marafiki zetu wanaweza kutusaidia.

Swali langu kwa serikali ni moja KAMA KWELI MNAFANYA MAMBO KWA MANUFAA YA WANANCHI WA TAIFA HILI NA HAMNA CHEMBE YA UCHAFU KWANINI MNAOGOPA TUWATAHMINI? NYAKATI HIZI NI ZA UWAZI NA UKWELI NA TUKUBALI KUWA SIKU ZOTE UONGO HUJIFICHA NA UKWELI HUONEKANA LAKINI SERIKALI INATAKIWA ISILAZIMISHE KUFICHA UONGO BALI UJICHIFICHE WENYEWE KWAKUA HAKUNA UBAYA NA NI PALE TU SERIKALI IKIWEKA MAMBO YAKE KI UWAZI.

Marehemu Mwalimu Nyerere katika kuwakemea viongozi wa serikali ya CCM ya awamu ya Mwinyi aliposema "Hatutaki Rais wetu anayeambiwa usiku na mke wake nini afanye na kesho anaamka na kututangazia kile kitu" Sina maana rais anayafanya hayo bali inatushangaza watu wengi ambao tulikuwa na imani naye, pale anapoamua kufanya matumizi makubwa ya kununua ndege bila kuwahusisha wabunge kufanya hivyo huku huduma za jamii zikidorora. wengi wetu tuliokuwa tunamtetea japo siyo wana CCM kama baadhi mnaotaka kutuita tunashindwa kuendelea kumtetea japo wakati huu upande mwingine utatuita ni WAPIGA DEAL MILANGO IMEMINYWA.

Tukubaliane hii nchi ni yetu wote hakuna anayeitakia mabaya lakini pia Wanasiasa wanatakiwa kujua kuwa sisi ni binadamu kama wao na pale mambo yakizidi kuwa mabaya ndipo tunapokuwa tunazidi kubadilika. Mwadhama Polycarp kardinal Pengo katika HOMILY yake mwaka 1995 kabla ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi alisema: " MLIO MADARAKANI YAANI CCM MZILAMISHE WANANCHI WAJE WAWACHAGUE MPAKA VICHAA TUISHIE KULIANGAMIZA TAIFA KAMA WAJERUMANI WALIVYOFANYA. HITTLER HAKUIPINDUA SERIKALI YA UJERUMANI BALI WANANCHI WALICHOKA NA WALICHOKUA WANAKIPATA KWA SERIKALI YA WAKATI ULE WAKAAMUA KUJARIBU MTU MWINGINE. NA YALIYOTOKEA WOTE TUNAJUA YAMEATHIRI DUNIA MPAKA LEO." Kwa kutolea mfano huu naomba nisieleweke kuwa kuna wanasiasa walio kama Hittler bali kuonyesha tu namna gani wananchi wakishachoka wanaweza kulamizisha mageuzi ambayo baadaye wanakuja kuyajutia na hili litakuwa limesababishwa na serikali iliyopo sasa.

Nikirudi na wazo kuu la thread hii ya wanamitandao kuungana katika kupigania uhuru wenu wa kutoa habari. Msitegemee kabisa main stream media zitawasaidia na wito kwa wachangiaji wenzangu pamoja na mapungufu ya Serikali yetu tujue tu kuwa tumpatie benefit of doubt rais wetu nina imani kubwa sana naye kuwa ana lengo nzuri, lakini pia tujue kuwa yeye ni binadamu kama sisi lakini ana silaha kubwa moja ni mkuu wa nchi yenye katiba onevu, hivyo tunavyokosoa tuliweke hilo akilini kuwa kashika mpini na sisi tumeshika makali busara katika ukosoaji inatakiwa zaidi kuliko kumuita majina yasiyokubaliki na ya kejeli. NINA IMANI KUBWA SANA NA RAIS.

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA

+447422980024
 
Michuzi Blog, hii ni blog kubwa sana na inayotembelewa na watu wengi sana hapo Tanzania na nje ya nchi

Huyo si nasikia yuko Ikulu?
 
Wewe umetaja clouds tu,tbc itv au radio one efm haujazisema mpaka muiseme clouds tu
Lipi unanilaum nimesema nitataja chache halafu mwishoni nimeandika main stream media sijui ITV na TBC mkuu unaziita nini?
 
Duniani hapa usitegemee kama kuna mtu wa kukutetea...hiyo haipo....kila mmoja anafanya kwa faida yake....mambo yakiharibika unakomaa kivyako
 
Uko biased ktk hilo ntamsimamia Mange Kimambi mara mia huyo alisema na anaendelea kusema na alisema kabla yake kuwa sheria ya habari ni mbaya, sasa ww umekuja kuongea kuhusu nywele za watu waliokufa sijui nini! Simamia hoja yako biashara yake ni mambo yake binafsi, au sema hao akina lemutz ambao hawakusema kabisa.
 
Uko biased ktk hilo ntamsimamia Mange Kimambi mara mia huyo alisema na anaendelea kusema na alisema kabla yake kuwa sheria ya habari ni mbaya, sasa ww umekuja kuongea kuhusu nywele za watu waliokufa sijui nini! Simamia hoja yako biashara yake ni mambo yake binafsi, au sema hao akina lemutz ambao hawakusema kabisa.
Mbona wewe pia upo biased nimeweka nywele kuhusu kumfahamu haikuhusiana na nini nimekisema kuhusu mange. Nimesema ni vigumu kumuelewea anasimamia nini maana hata yeye hutaki kukosolewa hivyo ukitaka kumtetea simamia hapo siyo nywele
 
Mbona humu akina Lizaboni,Faizafox,Ruttashoborolwa and company walikaa kimya mpaka Mubyazi alipotoka ndio wakakimbilia kuanzisha mada uchwara
 
Mbona humu akina Lizaboni,Faizafox,Ruttashoborolwa and company walikaa kimya mpaka Mubyazi alipotoka ndio wakakimbilia kuanzisha mada uchwara
Ulitaka niwataje wote? halafu mimi sijui kama lizabon ana blog kama anayo basi mada imemuhusu. Halafu naona hujanielewa mada. mada inawahusu wamiliki wa blog siyo wachangiaji. Naomba ondoa chuki zako binafsi na uliowataja jikite katika mada. Sizungumzii ukada hapa nazungumzia haki ya kusema kwa uhuru bila kusumbuliwa kama unataka kuzungumzia vinginevyo uwanja upo fungua thread nyingine
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom