Walijiuzulu au walifukuzwa!

OMWITUMA

Senior Member
Aug 6, 2013
119
29
Jamani wana JF naomba kupewa ufafanuzi juu ya hawa mawaziri 4, kuna baadhi ya vyombo vya habari waliandika na kutangaza kuwa mawaziri 3 walifukuzwa ila mmoja alijiuzuru, vingine vingine vilitangaza wamejiuzulu na vingine wakatangaza Rais katangaza kutengua uteuzi wao huku mwingine akitangaza kujiuzulu, PM alitangaza kuwa Rais anaweza kuwateua tena maeneo mengine, Je, aliyejiuzulu naye anawezateuliwa tena? je, waliofukuzwa watawezaje kuteuliwa tena? kama walijiuzulu kuna barua waliandika kuthibitisha kuwa wamejiuzulu? karibu kwa ufafanuzi
 
swala la kujiuzulu linakuja pasipo shinikizo la mtu kwa hiari ila MB kagasheki amejiuzuru kwa shinikizo la kikazo cha dharura kabla ya PM kutangaza uamuzi wa raisi kimsingi alitaka sifa walifukuzwa na Chama si kujiuzuru
 
Vyovyote mtu atakavyopenda kuita kama kujiuzulu au kufukuzwa la msingi ni kuwawamepoteza nafasi zao. Mmoja wao aliwahi kusema huko nyuma kuwa akijiuzulu Tanzania katu haiwezi kupata waziri mzuri kama yeye. Napata tabu kuona waziri mzuri namna yake akifukuzwa kazi!
 
Mawaziri wote wanne walitimuliwa kazi na Mh. Rais baada ya wao kusita kujiuzulu. Hata Kagasheki alipotangaza kujiuzulu tayari rais alikuwa ameshatengua uteuzi wake.

Wote walifukuzwa
 
swala la kujiuzulu linakuja pasipo shinikizo la mtu kwa hiari ila MB kagasheki amejiuzuru kwa shinikizo la kikazo cha dharura kabla ya PM kutangaza uamuzi wa raisi kimsingi alitaka sifa walifukuzwa na Chama si kujiuzuru

Kuna mara mbili aidha maamuzi yako au umma kukulazimisha kujiuzulu.
 
Mawaziri wote wanne walitimuliwa kazi na Mh. Rais baada ya wao kusita kujiuzulu. Hata Kagasheki alipotangaza kujiuzulu tayari rais alikuwa ameshatengua uteuzi wake.

Wote walifukuzwa

Hofu yangu ni kuwa hawa nao wanageuka kuwa wapinzani waliondani ya ccm. Muda si mrefu ujao wataungana na wale waliopewa jina la "mawaziri mizigo" na kuzidi kuliimarisha kundi hili. Sijui Nape atafanyaje tena maana wakibaki mizigo na wakitoka mizigo.
 
Back
Top Bottom