Elections 2010 Waliitwa wapiganaji ndani ya CCM, mbona hawako vitani Igunga?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Waliitwa wapiganaji ndani ya CCM na wakawa ndio tumaini la CCM katika uvuaji magamba, je imetokea nini ? Mbona hawako Igunga kwenye uwanja wa mapambano na badala yake walioitwa mafisadi ndio wanatamba ? Naomba maoni ya wakereketwa humu ndani wanisaidie kulitatua hili fumbo, imekuaje hadi hawa wapiganaji hatuwasikii tena ?

Untitled-1.jpg



attachment.php



Je wametupa silaha chini au yenyewe ndio magamba na sasa yamevuliwa ?
 
Waliitwa wapiganaji ndani ya CCM na wakawa ndio tumaini la CCM katika uvuaji magamba, je imetokea nini ? Mbona hawako Igunga kwenye uwanja wa mapambano na badala yake walioitwa mafisadi ndio wanatamba ? Naomba maoni ya wakereketwa humu ndani wanisaidie kulitatua hili fumbo, imekuaje hadi hawa wapiganaji hatuwasikii tena ?

View attachment 38028




attachment.php



Je wametupa silaha chini au yenyewe ndio magamba na sasa yamevuliwa ?

Yaani mkuu ni vichekesho, sijui wapiganaji gani huwa wanauogopa uwanja wa Vita, yaani hii Igunga imewaondolea kabisa japo kale kaheshima kidogo walikojenga kwa baadhi ya watanzania. RA kweli kidume huko CCM hauna sijui Nape, Mwakyembe Sitta, Killango wote wamefyata kimyaaaaaaaaa!!!!
 
Ni vigumu wananchi kulielewa hili,na kama tungekuwa si wavivu wa kufikiri hapa ndio lilikuwa anguko la CCM maana wale waliokuwa wanajiita makamanda wa kupambana na ufisadi hata kama ni kwa kujipendekeza basi hawatakiwi maana watakiua kabisa chama,CCM wanachotaka ni kushinda kwa hila zote sasa hawa wakienda na sera zao za kuyapinga magamba wakati moja ya gamba CCM ililiangua lifanye kampeni unategemea nini hapo?

Hilo gamba ndo liliombwa liwasaidie kupiga kampeni,hao nao wenye hizo picha wanajifanya wanapinga ufisadi hawataruhusiwa kwenda huko.anaeruhusiwa ni yule tu anaekubali ufisadi,ila hao nao ni waongo tu kwani wanafiki huwa wako hivyo,mbona hawakusimamia sakata la Richmond, mwisho wa siku Siita alisema mjadala wa Richmond umefungwa ulifungwaje? Nani ni Richmond na je kamati ilimpata na hatia leo ikoje hali? Hao wote ni magamba.
 
Wote kwishnei. Sitta nia yake ilikuwa ni kumvua Lowassa Uwaziri Mkuu, Mwakyembe alikuwa anatafuta unaibu waziri, Nepi keshalambishwa ukatibu wa kupuyanga mitaani na Sendeka naskia ameamua aconcentrate kwenye biashara ya kuuza Ngombe baada ya kugundua kina Mwakyembe wamempotezea muda wake. Anna Kilango nae thamani yake kama ya Mwakyembe anasubiri unaibu Waziri soon.
 
Ni vigumu wananchi kulielewa hili,na kama tungekuwa si wavivu wa kufikiri hapa ndio lilikuwa anguko la CCM maana wale waliokuwa wanajiita makamanda wa kupambana na ufisadi hata kama ni kwa kujipendekeza basi hawatakiwi maana watakiua kabisa chama,CCM wanachotaka ni kushinda kwa hila zote sasa hawa wakienda na sera zao za kuyapinga magamba wakati moja ya gamba CCM ililiangua lifanye kampeni unategemea nini hapo? Hilo gamba ndo liliombwa liwasaidie kupiga kampeni,hao nao wenye hizo picha wanajifanya wanapinga ufisadi hawataruhusiwa kwenda huko.

Anaeruhusiwa ni yule tu anaekubali ufisadi,ila hao nao ni waongo tu kwani wanafiki huwa wako hivyo,mbona hawakusimamia sakata la Richmond,mwisho wa siku Siita alisema mjadala wa Richmond umefungwa ulifungwaje?nani ni Richmond na je kamati ilimpata na hatia leo ikoje hali?hao wote ni magamba.

Yaani huu ni uthibitisho wa maandishi kwamba CCM ni chama cha kifisadi period!
 
ole wao waonekane Igunga naskia RA amechagua watu wa kwenda kule
haswaaa mkuu. Nepi kazi yake kusema huko fesibuku kuwa nimekwenda igunga na nitakwenda tena.
masikini wa mungu, kangoja ccm wametoa kafara mtoto wa watu ndo yeye kesho yake huyooo mbio, kaenda kutoa rambirambi.

mwanaume pekee huko ccm ni rostam, CHENGE NA LOWASA....don. wengine ni tia maji tia maji tu! mbinguni hawapo, duniani hawapo
 
nilimsikia mama kilango akihutubia wana same ikilaani hijabu nikajiuliza mbona hayuko uwanja wa mapambano leo nimepata jibu hayo ndio ya kuwaambia wana igunga wanafanywa wajinga na ccm ana kilango ni kama nape hatakiwi maana ndio walewale vigeugeu.
 
Waliitwa wapiganaji ndani ya CCM na wakawa ndio tumaini la CCM katika uvuaji magamba, je imetokea nini ? Mbona hawako Igunga kwenye uwanja wa mapambano na badala yake walioitwa mafisadi ndio wanatamba ? Naomba maoni ya wakereketwa humu ndani wanisaidie kulitatua hili fumbo, imekuaje hadi hawa wapiganaji hatuwasikii tena ?

View attachment 38028




attachment.php



Je wametupa silaha chini au yenyewe ndio magamba na sasa yamevuliwa ?

CCM ina jeshi kubwa, kwa nn watumie bunduki kumuua nzi ? walio enda igunga wanatosha kuwapakata CDM na kuwafanya watakavyo
 
Lakini hata Lowassa na Chenge anayekijua vizuri Kisukuma hawako kule. Binafsi nakwazwa mno na mtu kufanyiwa kampeni badala ya yeye mwenyewe kufanya. Hii naifananisha na mtu kuchangiwa ili afanye harusi yake mwenyewe. Dalali kafunikwa kabisa na hawa ma-celebrity wa siasa za nchi hii.
 
Wakati Nape anaanza kupiga 'Kelele' alionekana kama sisimizi anayepiga kelele akitaka Tembo ambaye ni Rostam aondoke pale alipokaa kwa sababu amewaumiza na alikuwa anaendelea kuwaumiza wengi sana, isipokuwa wana-CCM wa Igunga tu. Kelele zikazidi sana mpaka Tembo akakosa usingizi ila akavumilia kwa kudhani kuwa sisimizi hawezi kumuondoa pale. Lakini Nape hakuacha kupiga kelele mpaka Tembo Rostam akakosa amani kabisa na kusema hii shida yote ni ya nini? Kwa nini nisiondoke ili niachane na Kelele hizi. Taratibu Tembo likajinyanyua na kuondoka, sio kwa kupenda, bali ni kwa sababu ya Kelele za Nape. Kwa hasira na gadhabu ya kukosa usingizi likaamua kuharibu kabisa makazi ya sisimizi ali asirudie tena kupiga kelele za namna hiyo, na kikubwa ni kwenda kumshitaki kwa watu wa Igunga ambao wamefaidika sana na fadhila zake, na kuwaambia kuwa mbaya wangu ndio mbaya wenu, na mbaya huyu ni Nape. Lakini kwa picha kubwa sidhani kama Tembo huyu anakubalika nchi nzima, hususan kwa wale ambao wameumia zaidi kiuchumi kutokana na wizi wa kifisadi, na kisiasa kutokana na uanzishaji wa siasa uchwara za kupakana matope. Ni juzi tu gazeti lake limeendelea kuzidi kulipa fidia watu kama Mzee Sumaye, ambaye nasikia haziivi kabisa na Mzee wa Monduli
 
Dawa ya mchawi mpe mtoto akulelea, mtoto atakuwa salama, ho wapiganaji uchwara wamezibwa midomo kwa kupewa uwaziri, unaibu na kelele zote kwisha, Ole sendeka na Kilango nao wananyenyekea huenda wakapata chochote , hii inaonyesha wazi kuwa wapiga kelele ndani ya CCM ni njaa tu,uchu wa madaraka hawana lolote.
Tanzania itakombolewa na umma wa watanzania kwa nguvu ya umma,walafi wa madaraka hawatatusaidia lolote.bahati nzuri Mungu humaliza mchezo wote hapahapa duniani na watu wakishuhudia,mfano Libya,aliyewaita wananchi Panya ndo kageuka panya buku sijui anakaa mapangoni kama Saddam. Mwisho wa CCM tutaushuhudia kwa macho yetu wenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom