Elections 2010 Waliitwa wapiganaji ndani ya CCM, mbona hawako vitani Igunga?

Igunga ni ya rostam kwa hiyo kama rostam aliona nape na wenzake walimtukana basi ametoa mashariti kuwa waliomtukana wasifike vinginevyo hatashiriki. Ccm wanakete chache za kucheza njia zote walizobaki nazo si salama. Hii ya kutokwenda inwapa unafuu maana wapiga kura wote ni warostamu walishalipwa kitambo kwa hiyo akiwaambi apigieni cdm watafanya hivyo.
Unique

Na itapofika 2012 RA atamlazimisha chairman wa chama cha magamba kumpiga chini Nape otherwise ana withdraw sponsorship kwenye chama.
 
Mkuu hao unaowasema unataka waende Igunga kufanyia kampeni chama gani? Chama chao hakijasajiliwa bado. Unapoona hata baadhi ya wabunge wa ndani ya mkoa wamepigwa marufukiu kwenda kumpa support mwenzao yaani Mbunge Mtarajiwa basi ujue kuna shida kubwa hapo. Hivi unaweza amini kwamba Mzee Sitta hajatia mguu Igunga!! Igunga imeonyesha wazi kabisa jinsi CCM ilivyo na makundi yalivyo. Yaani pamoja na juhudi zoooote za akina Mwinyi na Mzee Msekwa lakini mambo bado!!

Kuna gazeti moja liliandika kwamba kuna kada mmoja aliombwa akagombee Igunga akakataa na kusema kwamba wacha wamuweke mtu wao washindwe ili tuheshimiane!! CCM ikishinda Igunga kuna watu watanuna ndani ya CCM humohumo na ikishindwa kuna wana CCM wataandaa karamu ya kushangilia kushindwa kwa CCM!! CCM wanamung'unyana wao kwa wao!! Mungu kiepushilie mbali kikombe hiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom