Walifariki watu wengi kwenye kivuko lakini viongozi hawakuwa wengi kama msiba wa Ruge

moto wa maji

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
3,795
2,000
mwaka Jana ajali hii ilisikitisha na kuumiza wengi sana hapa nchini na nje ya nchi takribani watu 200 walipoteza maisha kwenye ajali ya kivuko.

Wananchi wengi walijitokeza kuweza kuwaokoa wenzao na kuwafariji lakini chakushangaza wawakilishi wa wananchi hawakuweza kufika kwa wingi kama walivyofika kwa Ruge. swali je ina maana Ruge ana thamani kubwa kuliko watu 200. Sio ccm sio chadema wote hamna kitu.

Viongozi jirekebisheni...!!!
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,540
2,000
Wote hatuwezi kuwa sawa hapa duniani, wengine hufa na kuviringishwa kwenye viroba na kutupwa baharini. Wengine huzikwa na ndugu zao wachache na wengine hubahatika kuzikwa kwa heshima ya kitaifa, cha muhimu ni nini ulichofanya wakati ukiwa hai hapa duniani.
 
MwanaWA Ebrania

Senior Member
Oct 6, 2017
199
250
mwaka Jana ajali hii ilisikitisha na kuumiza wengi sana hapa nchini na nje ya nchi takribani watu 200 walipoteza maisha kwenye ajali ya kivuko.

Wananchi wengi walijitokeza kuweza kuwaokoa wenzao na kuwafariji lakini chakushangaza wawakilishi wa wananchi hawakuweza kufika kwa wingi kama walivyofika kwa Ruge. swali je ina maana Ruge ana thamani kubwa kuliko watu 200. Sio ccm sio chadema wote hamna kitu.

Viongozi jirekebisheni...!!!
Acha wivu wa kijinga ndugu.
Kunatofauti kubwa Kati ya watu na mtu.
Boss Ruge ni mtu aliyewatengeneza watu weengi wajue thamani Yao na wajitambue hasaa vijana.
Taifa linajua mchango wa Boss Ruge MUNGU akuhifadhi unapostahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,056
2,000
Kuna uzi wangu nimeweka humu kuhusu sababu 3 zilizopelekea umarufu wa msiba huu @mod wameunganisha tayari sijui wapi uko.
hu msiba ni marufu na si kwamba umegusa(umiza weng)
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,875
2,000
mwaka Jana ajali hii ilisikitisha na kuumiza wengi sana hapa nchini na nje ya nchi takribani watu 200 walipoteza maisha kwenye ajali ya kivuko.

Wananchi wengi walijitokeza kuweza kuwaokoa wenzao na kuwafariji lakini chakushangaza wawakilishi wa wananchi hawakuweza kufika kwa wingi kama walivyofika kwa Ruge. swali je ina maana Ruge ana thamani kubwa kuliko watu 200. Sio ccm sio chadema wote hamna kitu.

Viongozi jirekebisheni...!!!
Labda ukifariki na wewe watajaaa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NeverExisted

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
409
1,000
Ndio ujue binadamu especially watanzania ni wanafiki kupitiliza. Na vijana wajue hivyo, viongozi wa kisiasa ndio wanaoongoza kwa unafiki,watu wanakwenda kwenye misiba wanayoiona ni ya 'maana' ili waonekane! Ikiwezekana wapate kiki. Sickening.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,910
2,000
mwaka Jana ajali hii ilisikitisha na kuumiza wengi sana hapa nchini na nje ya nchi takribani watu 200 walipoteza maisha kwenye ajali ya kivuko.

Wananchi wengi walijitokeza kuweza kuwaokoa wenzao na kuwafariji lakini chakushangaza wawakilishi wa wananchi hawakuweza kufika kwa wingi kama walivyofika kwa Ruge. swali je ina maana Ruge ana thamani kubwa kuliko watu 200. Sio ccm sio chadema wote hamna kitu.

Viongozi jirekebisheni...!!!
Hawawezi kujirekebisha. Sahau. Tatizo ni sisi wananchi tunacheka na ngedere! N aukicheka na ngedere siku zote utavuna mabua. Tungekuwa tuko serious kuwabana wawajibike kama viongozi wengine duniani unafikiri wangepata muda wa kujilundika hivyo sehemu moja kama wako picnic na hawana kazi ya kufanya! Nchi yenye wananchi wanaojielewa kama mambo hayaendi sawa siku ambayo viongozi watafanya ujinga wa kujilundika sehemu moja namna hii kwa mambo ya kijinga kama ilivyotokea jana basi watakuwa wamewarahisishia wananchi nafasi ya kuwapa kisago cha mbwa koko!
 
carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,877
2,000
We jamaa una safari ndefu sana ya kuuelewa huu ulimwengu..
Kwanini hujauliza rais analindwa 24/7 halafu shule kama tosamaganga zenye wanafunzi 1000+ zinalindwa na mlinzi mwenye rungu..
Binadamu sio sawa mkuu..thamani yako inatokana na mchango wako..huwezi fananisha watu 100 wakulima na mtu mmoja ambaye amewapa ajira vijana zaidi ya 100 (huu ni ukweli mchungu kwa sisi masikini) .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom