Uchaguzi 2020 Walidhani wameiua CHADEMA, sasa kampeni ya "Kitanda kwa Kitanda" ya nini?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,126
33,156
Nilikua nafuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa. Kuna maneno yamenifikirisha jambo.

Walijua wameiua Chadema, tuliambiwa humu mitandaoni kuwa Magufuli kaua Upinzani. Mara ooh, Chadema haitasimama tena.

Sasa nilichoshuhudia kutoka kwenye kinywa cha Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndio tuliambiwa kaua Upinzani na kaua Chadema, nimeshangaa Sana. Kumbe Mkubwa kweli kapaniki.

Amesikika akisema, "Msipuuze mkazembea kwenye kampeni kwamba tayari tumeshinda,
hapana. Tena safari hi tutafanya kazi kweli, tutafanya kampeni kitanda kwa kitanda".

Akaendelea kusema, "Tena niwahakikishie safari hi tutafanya kazi kweli (kampeni)."

Msipuuze mkidhani timeshashinda, tutafanya kampeni kitanda kwa kitanda.

Kwanini kufanya kampeni kwelikweli, tena kitanda kwa kitanda? Mnashindana na nani wakati Upinzani umekufa na ninyi mnakubalika, mnapendwa na mmefanya mambo ambayo hayajafanywa na awamu yeyote?

Haya maneno yanafuta kabisa yale maneno kuwa Upinzani umekufa nchini, Magufuli kaua upinzani, na Chadema haitatamalaki tena.

Haya maneno yamefuta kabisa yale maneno kuwa Magufuli kaua upinzani, upinzani umekufa.

Return of the Lissu,
Lissu strikes again,
Lissu is back,
Lissu is back in town.
 
Always never underestimate your enemy(opponent). Kuna dogo alimpiga mtama baunsa wa msanii flani maarufu kule Tandale, mbavu alilamba mchanga sababu ya dharau zake kwa dogo hakujiandaa.

Acacia imepotea kwenye ramani ya dhahabu za Bongo sababu waliwadharau watanzania na uwezo wao kukusanya taarifa za kiintelijensia.

CHADEMA inapata taabu kwenye uchaguzi huu sababu walimdharau Magufuli hajui siasa, walimdharau Polepole na wenzie hawakudhania wanaweza siasa na fitina za kisiasa kiwango hiki.
 
Na hapo 4 years uwanja ulikuwa wao, wasanii wote maalufu Ni wao na Pesa ya honga wanayo Ila Bado ccm hawajiamini hii inatokana na ubabe wa m/kiti wao, nakwataarifa yako, team ya kampeni mwaka huu Ni mbovu kuliko zote zilizowahi kuwepo.
Yaani leo nimeona Lissu anashinda mchama kweupe. JPM amekuwa mpole kuliko maelezo. Huo unyonge sijui unatokana na nini.
 
Always never underestimate your enemy(opponent).
Kuna dogo alimpiga mtama baunsa wa msanii flani maarufu kule Tandale, mbavu alilamba mchanga sababu ya dharau zake kwa dogo hakujiandaa.

Acacia imepotea kwenye ramani ya dhahabu za bongo sababu waliwadharau watanzania na uwezo wao kukusanya taarifa za kiintelijensia.

CHADEMA inapata taabu kwenye uchaguzi huu sababu walimdharau Magufuli hajui siasa, walimdharau Polepole na wenzie hawakudhania wanaweza siasa na fitina za kisiasa kiwango hiki.
Umesahau kuwa m/kiti wako alizuia shughuli zote za vyama vya siasa kasoro CCM? Acha kudhani Watanzania wote ni wajinga, CCM ni sawa na shetani
 
Always never underestimate your enemy(opponent).
Kuna dogo alimpiga mtama baunsa wa msanii flani maarufu kule Tandale, mbavu alilamba mchanga sababu ya dharau zake kwa dogo hakujiandaa.

Acacia imepotea kwenye ramani ya dhahabu za bongo sababu waliwadharau watanzania na uwezo wao kukusanya taarifa za kiintelijensia.

CHADEMA inapata taabu kwenye uchaguzi huu sababu walimdharau Magufuli hajui siasa, walimdharau Polepole na wenzie hawakudhania wanaweza siasa na fitina za kisiasa kiwango hiki.

..acacia haijapotea ktk ramani ya dhahabu za bongo.

..kampuni ya kwanza kuingia nchini ilikuwa barrick gold.

..baadae wakabadilisha jina wakawa wanaitwa african barrick gold.

..halafu mwaka 2014 wakabadilika tena wakaitwa acacia.

..kilichotokea ni minority shareholders kuuza hisa zao ili majority shareholder/barrick waweze kuyamaliza na serikali ya Tz.

..waTz huku mtaani tulipigwa changa la macho kuaminishwa kwamba waliokuwa wakituibia ni acacia na siyo barrick.

..kama aliyekuwa anatuibia ni acacia kwanini serikali ilikuwa inafanya mazungumzo na barrick?
 
umesahau kuwa m/kiti wako alizuia shughuli zote za vyama vya siasa kasoro ccm? Acha kudhani Watanzania wote ni wajinga, CCM ni sawa na shetani.
Wewe unaelewa nini unaposikia neno fitina?

Hicho ulichozungumzia ndiyo fitina zenyewe, hapo mwenyekiti wao siyo wangu alifanya fitina za kisiasa kuzuia wenzie wasifanye siasa za majukwaani.

NB: Siku zingine uwe makini sana unapojaribu kusoma na kujibu comment zangu.

Naandika ujumbe mkubwa au uliojificha zaidi ya kile unachohisi umekielewa au zaidi ya ulichokiona.
 
..acacia haijapotea ktk ramani ya dhahabu za bongo.

..kampuni ya kwanza kuingia nchini ilikuwa barrick gold.

..baadae wakabadilisha jina wakawa wanaitwa african barrick gold.

..halafu mwaka 2014 wakabadilika tena wakaitwa acacia.

..kilichotokea ni minority shareholders kuuza hisa zao ili majority shareholder/barrick waweze kuyamaliza na serikali ya Tz.

..waTz huku mtaani tulipigwa changa la macho kuaminishwa kwamba waliokuwa wakituibia ni acacia na siyo barrick.

..kama aliyekuwa anatuibia ni acacia kwanini serikali ilikuwa inafanya mazungumzo na barrick?
Sawa mkuu.

Upo sahihi Acacia bado wapo kwenye ramani ya dhahabu Bongo. Pia Acacia hawaku wa- underestimate Watanzania.
 
lee van cliff,

Kuna neno Mbowe alipenda kulitumia kila apatapo nafasi ya kuongea na lilipuuzwa nalo ni " sisi wapinzani hasa chadema tumeimarika kuliko wakati wowote ule" hili neno halikuaminiwa hata na baadhi ya wanaChadema wenyewe na kupelekea baadhi ya viongozi kuunga juhudi.

Sasa ndiyo watu wanaanza kuuona uimara wa upinzani, na matokeo yake ndiyo hizo kampeni za kitanda kwa kitanda. Sasa hivi zile kauli za ushindi wa 100% hazipo tena.
 
Back
Top Bottom