Walid Aman Kabourou ajitosa uenyekiti CCM Kigoma

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
kabourou.jpg


DK. KABOUROU AJITOSA UENYEKITI KIGOMA


Makada saba wa CCM wamerejesha fomu kuchuana kugombea nafasi ya uenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, akiwemo Dk. Aman Walid Kabourou.

Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma, Mohamed Nyawenga, alisema kuwa waliorejesha fomu hizo ni Azim Seleman Premji, ambaye anatetea kiti chake, Nashoni William Bidyangunze, William Ntahindala Ruturi, Nunu Mrisho Mwamba, Dk. Aman Walidi Kabourou, Michael Mbwano Ndereka na Edgar Mkosamali.

Alisema wagombea wote kwa pamoja walichukua fomu na kuzirudisha na kwamba hakuna tatizo lolote lililojitokeza katika uchukuaji fomu na urudishaji.
 
watu wana CV zinazoshuka kweli kweli. Yaani siamini kwamba huyu Jamaa aliishawahi kukalia kiti cha DR SLAA ndani ya CHADEMA.
 
Uchaguzi huu ndio utakuwa safari ya mwisho ya kumzika kisiasa Walid Kabourou. Hatashinda tena na is no longer Mbunge wa Africa Mashariki. Aanze sasa na yeye kuchoma mahindi kama Hiza Tambwe!
 
AMANI WALI KABOUROU; Nyota ya Mageuzi iliyofifia!!!!
 
Uchaguzi huu ndio utakuwa safari ya mwisho ya kumzika kisiasa Walid Kabourou. Hatashinda tena na is no longer Mbunge wa Africa Mashariki. Aanze sasa na yeye kuchoma mahindi kama Hiza Tambwe!

Mbona alikuwa kimya sana?
 
Mbona alikuwa kimya sana?

Mkuu CS,
Hawezi kusikika kwa sababu ukiwa Mbunge wa Afrika Mashariki hutumikii wananchi moja kwa moja. Yani hujihusishi na Local Politics matokeo yake ndio amekufa kisiasa. Ndiyo maana Dk Harisson Mwakyembe alitoka kule akaja kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri.

TUMBIRI (PhD In Progess at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams),

tumbiri@jamiiforums.com
 
mimi nafikiri ni bora angeenda kushika chaki kama mnafiki mwenziye Lamwai maana walishalaaniwa kwa kuwatapeli watanzania na siasa zao feki za ukombozi!!!!!
 
Mkuu CS,
Hawezi kusikika kwa sababu ukiwa Mbunge wa Afrika Mashariki hutumikii wananchi moja kwa moja. Yani hujihusishi na Local Politics matokeo yake ndio amekufa kisiasa. Ndiyo maana Dk Harisson Mwakyembe alitoka kule akaja kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri.

TUMBIRI (PhD In Progess at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams),

tumbiri@jamiiforums.com
\

tumbiri umesoma sana naomba kutumia jina lako nigombee vyeo ndani ya chama
 
kafanya mistake moja kubwa, sasa inabidi a spend the rest of his life kutetea ujinga wake.Bora angekuabali kuwa alitokota na kuanza life mpya."Mentality Gamba"
 
Magamba walimnunua kwa bei rahisi sana na impact yake hadi sasa anakiogopa kivuli chake,anaenda kujidhalilisha tu kwa wana Kigoma.....hana jipya na unafiki wake umefikia mwisho wake!!
 
Jamaa kwa madaraka hawezekani. Toka Ubunge/Ukatibu CDM na sasa uenyekiti wa CCM! Wakati yupo CDM si alikuwa akisimama majukwaa na kuisema CCM haifai, hivyo sasa atakuwa nagombea kwenye Chama kinachofaa!

Nasikia alikuwa akifundisha vyuo huko Marekani imekuwaje manake tangia arudi TZ sijamsikia akisema anatembelea marekani au ana vyesi huko Amerika?
 
Hapo kunaweza kuwa ndio mwisho wake wa kisiasa kama atashindwa, mwenzake Tambwe Hiza mpaka sasa sijajua kama atagombea nafasi yoyote.
 
Mharakati:Nimekukubali kumkubali kwako Tumbili kwamba amesoma sana hatimaye kuomba utumie jina lake kugombea vyeo ndani ya chama.Angalizo:siasa sihasa yataka usomi kama hivyo,wajua cheza na maneno?Waweza liita chungwa-chenza wewe?
 
Huyu atakuwa fundisho zuri kwa watu kama Zitto!! Wanakuwa watu wakiwa CHADEMA na wakitoka tu wanageuka vinyago!!
 
DR. Mkumbo alisema jana, "huwezi ukatoka chama cha upinzania ukawa mwanasiasa". Hiki ndo kinachomla huyu jamaa.

Wiki mbili zilizopita nilikuwa naongea na mtu fulani kutoka mwisho wa reli juu ya huyu jamaa. akanieleza jinsi watu wa mkoa huu walivyomtegemea kuleta mabadiliko ya mkoa wa KG lakini baada ya kutangaza kuhama CDM alitaka kuchoma nyumba na mali zake pale mwisho wa reli.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba amekuwa anaishi kwa kificho sana pale KG kwa yale aliyofanya kurudi ccm.

Hivyo, asitegemee kuwa mwanasiasa tena hasa kwa kusaliti upinzani na mioyo ya wana-Kigoma.
 
Back
Top Bottom