Walichoahidi "zaidi" ni kile kile zaidi au zaidi ya kilekile? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walichoahidi "zaidi" ni kile kile zaidi au zaidi ya kilekile?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 30, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  MM (Tanzania Daima Jumatano)


  MANENO yanabeba maana. Wakati mwingine maneno yanaficha maana vile vile. Lakini wakati mwingine maneno yanakwepesha maana.
  Ni jukumu la mtu mwenye akili kujua kinachomaanishwa nini na kama hajui aulize watu wamfafanulie.
  Mtu anayekwenda na kutenda na kukumbatia kitu ambacho haelewi maana yake anajifanya mtumwa, kwani kama wahenga walivyosema: “asiyejua maana haambiwi maana” na kuwa “ukimwamsha aliyelala, utalala wewe”.
  Wakati Mwenyekiti wa CCM anachukua fomu ya kutaka kuwa mgombea pekee (namaanisha hilo) mojawapo ya ahadi ambazo amezitoa na kuwa kama kauli mbiu yake mpya kwa mwaka huu ni kuwa katika uongozi wake ujao kutakuwa na ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi.
  Hii ni nyongeza ya kauli ya 2005 ambapo ahadi ilikuwa ni ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Kwa maneno mengine, mwaka huu ili ‘mpya’ imeongezwa na kuwa ‘zaidi.’ Wapo watu walioshangilia!
  Walishangilia kwa sababu neno ‘zaidi’ limebeba maana ya ‘wingi, kuzidi na kama nyongeza ya aina fulani.’
  Mtu ambaye alikuwa anakwenda mwendo wa kilomita 50 kwa saa akisema ameongeza zaidi mwendo ni wazi kuwa atakuwa ameenda zaidi ya kilometa zaidi ya 50 kwa saa. Haijalishi kama ni 55, 60, 70, au 100! Alimuradi tu kuwa ni ‘zaidi’ ya ile ya 50. Lakini kabla hatujaangalia ‘zaidi’ hebu turudi nyuma na kuangalia ‘mpya’.
  Ya zamani inapokuwa ‘mpya’
  Kitu cha zamani hakiwezi kuwa kipya. Unaweza ukakipaka rangi mpya, unaweza kukipamba kwa maua na unaweza hata kukiweka mafuta ya kuking’arisha lakini cha zamani ni cha zamani tu hakiwezi kuwa kipya.
  Gari la zamani linaweza kupakwa rangi, kufanyiwa matengenezo na kusifiwa kuwa lina mlio kama wa gari mpya lakini ukweli unabakia pale pale kuwa bado ni gari la zamani.
  Sasa wote ndani ya hilo gari mnaweza kushangilia na kuimba kuwa gari lenu linaenda kwa ‘kasi mpya’, au linaonekana lina ‘nguvu mpya’ na dereva wake anaenda kwa ‘ari mpya.’ Haya yote yanaweza kuwa ni kweli lakini ni ‘mapya’ kwa maana tu kuwa yanahusiana na vya zamani.
  CCM na uongozi wake ni wa ‘zamani’ hakuna kilicho kipya ndani ya CCM. Anayefurahia rangi mpya, tsheti mpya na nyimbo mpya anajidanganya kwa sababu hakuna kitu chochote kilichofanywa ndani ya CCM kuifanya kuwa ni mpya.
  Isipokuwa kimepakwa rangi vitu vya zamani, kuvipamba vilivyochuja na kuvitia mafuta vilivyokuwa vigumu kwa kutu. Hivi ndivyo huletwa kwa wapiga kura na kuambiwa kuwa ni ‘kipya!’ Na wale wasio na muda wa kufikiria (wengine wana vyeti vya vyuo vikuu) wanakuwa wa kwanza kushangilia kuwa ni ‘kipya.’
  Kwa miaka karibu ishirini sasa CCM imekuwa ni chama kile kile chenye viongozi wale wale wenye sera zile zile.
  Ni chama ‘kilekile’ Bado kinaamini wawekezaji ndio wataliinua taifa hili, bado kinaamini Watanzania hawawezi kutengeneza maisha yao na kuyafanya bora, bado kinaamini Watanzania hawawezi kuaminiwa kuchagua kiongozi wanayemtaka hata kama hana chama, bado kinaamini maendeleo ni kuendeleza vitu na si watu, na bado kinaamini kabisa kuwa bila chenyewe Tanzania itasambaratika na ni wao pekee ndio wana uwezo wa kulinda na kuutetea Muungano! Cha kutisha kuna mamilioni ya watu wenye kuamini hivi vile vile!
  Wanaamini kuwa pasipo CCM wao hawawezi kufanikiwa na kwamba pasipo CCM basi Tanzania ‘haiwezekani.’ Lakini ukiwasogelea kwa karibu utajua ni kwa nini wanaamini hivyo.
  Sababu kubwa ni kwamba wao ni wanufaika wa mfumo wa utawala wa kifisadi uliojengwa kwa miaka hii kumi na saba hivi. Wale wanaonufaika na mfumo huu ndio ambao hawako tayari kupambana na ufisadi na hawawezi kujitahidi kuubadili mfumo huu.
  Tena kwa wao mfumo hauna tatizo isipokuwa ‘watu’ ndio wenye tatizo. Ukiuwaliza kuna ufisadi CCM watakataa kabisa na kudai kuwa ‘mtu mmoja mmoja’ ndiyo fisadi. Na wengine watakuambia kuwa chama kizima kina mafisadi ‘wanne’ tu ambao tayari wamefikishwa mahakamani! Hivyo hiki ni chama cha zamani.
  Kitu cha zamani kinapofanywa kwa upya ni mgongano usioweza kupatana. Huwezi kufanya kitu cha zamani kikawa kipya kwa sababu kinapingana kimantiki. Kipya ni kile ambacho hakikuwapo awali, sasa cha zamani chaweza vipi kuwa kipya isipokuwa kwa maneno na mapambo tu?
  CCM na uongozi wake wanaweza kuvaa mavazi mapya ya rangi ya njano, wanaweza kununua magari mapya ya kampeni, wanaweza kuzungumza kwa lugha mpya ya kisiasa lakini ndani kabisa ni ‘wale wale.’
  Kilekile kinapofanywa zaidi
  Sasa hapa ndipo tunakutana na mgongano mpya wa uchaguzi huu mkuu. CCM wanatupendekezea kuwa sasa hivi watafanya mambo yale yale isipokuwa ‘kwa zaidi’. Yaani ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi.
  Hapa ndipo tunajiuliza, kama kitu ni kile kile (si kipya) unapokifanya kwa zaidi unakiongeza au unaongeza uwepo wa kitu kile kile? Hii ‘zaidi’ ina maana gani?
  Kwa uelewa wangu wa kisiasa ni kuwa chini ya ngwe ya pili ya Kikwete Tanzania itategemea wahisani zaidi, itaendelea kubelembeleza misaada zaidi, Kikwete ataendelea kusafiri zaidi na kutakuwa na majaribio zaidi ya mwonekano wa kupambana na ufisadi! Yaani yote tuliyoyaona miaka hii mitano inayoisha ndiyo tutayaona zaidi.
  Chini ya utawala huu watoto wengine wakifa kizembe kama kule Tabora, watawala wetu wataendelea kuwa wakimya zaidi!
  Chini ya utawala huu wanafunzi wa Kitanzania wataendelea kutupwa na serikali yao tena kwa haraka na kasi zaidi bila ya mtu yeyote kuwajibishwa!
  Chini ya utawala huu yale yaliyoonyeshwa hivi juzi kuhusu matatizo ya utawala na matumizi mabaya ya fedha katika vituo vyetu vya afya ndiyo yatakuwepo tena zaidi.
  Chini ya utawala huu matatizo ya ubora wa elimu yatatatuliwa kwa kuongoza idadi na siyo ubora kwa zaidi.
  Huu ni mwaka wa zaidi wa ‘yale yale.’ Kama tumesikia matatizo ya magari na usafiri wa rais miaka hii mitano iliyopita fikiria itakuwaje miaka mitano ijayo. Sitoshangaa kuwa huko mbeleni kama Kikwete atashinda (sidhani kama atashinda) inaweza kutokea rubani akakosekana angani na hakuna mtu atakayejua imekuwaje. Labda Salva atatoa maelezo kuwa wanaijaribu mitambo ya kisasa ya ndege!
  Hivyo, uchaguzi uliopo mbele yetu Watanzania ni rahisi sana (japo kwa wengine ni mgumu). Ni uchaguzi wa ‘kile kile zaidi’ au ‘cha tofauti zaidi’.
  Wapo ambao wanataka kile kile hawa watakipata. Lakini sisi wengine bado tunaamini tunahitaji cha ‘tofauti zaidi.’ Pande hizi mbili haziwezi kupatana. Zaidi.
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Jun 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nimependa approach yako.Nitarejea
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  "zaidi" imeongezwa kwenye mpya,kama maisha yalikuwa magumu kipindi chake cha miaka mi tano anamaanisha kwamba miaka mingine inayokuja mitano maisha yatakuwa magumu zaidi.

  kama bei ya vitu vilipanda katika miaka yake mitano ya mwanzo basi zitaongezeka "zaidi" kwenye miaka mitano inayokuja.

  na inaendelea hivyo hivyo kwenye kila sehemu ni nyingi sana kuzitaja wengine wanaweza kumalizia.
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mkuu mwana kijiji kama washauri wake wanasoma humu unaweza ukawa umewapa mtihani mkubwa sana ha ha ha.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Na wanavyoogopa mitihani si watasema mtihani umetokana na "chuki binafsi"..
   
 6. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ni tandiko zuuri kabisa...tatizo linakuja tu ni wangapi watafuniliwa kwa andiko hili??? Ni matumaini yangu kuwa malaria Sugu atabadilisha msimamo yeye na wamfuatao au sivyo anaweza akajenga hoja dhidi ya mzee mwanakijiji......ningependa kupata makala hii katika gaziti la Mwanahalisi. Nadhani utanisaidia kwa hili MKJJ
   
 7. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,813
  Likes Received: 2,754
  Trophy Points: 280
  Kweli Mwanakijiji, huu ni mtihani kiboko kwa wapambe na makada Chama ch Mafisadi. Kwa hali hii, kauli mbiu hii ikipata wapinzani wa kujenga hoja vizuri, ni ya kulimaliza zimwi hili liyujualo na lenye azma ya kutumaliza. Ukifikiri kwa makini, pamoja na ukweli kuwa kuna mengi mazuri yaliyofanywa na jk, hali mbaya inna overwhelm mazuri yote. Yaendelee haya kwa ari zaid kasi zaidi na nguvu zaidi? Miaka mitano mingine, zimwi hili litujualo kakika litatumaliza. Tufanye uchaguzi sahihi Octorber 2010.
   
Loading...