Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,384
Historia ina mafundisho mazuri na ya wazi mno:
Jambo moja lilikuwa dhahiri mno machoni pa wananchi wengi wa Libya pale kiongozi wao alipofikia hatua ya kuhamaki na kuwaita wananchi wake MAPANYA na kwamba hatishwi na nguvu zao;Jambo moja pia lilikuwa dhahiri kwa wananchi wa Rwanda pale utawala wa Wahutu na wanamgambo wa Intarahamwe walipofikia hatua ya kuhamaki na kufikia hatua ya kuwaua wananchi wao wenyewe huku wakiwaita MENDE,
Kilichokuwa dhahiri ni kuwa saa ya ukombozi kwa wananchi wa Libya na wale wa Rwanda ilikuwa karibu mno,na kwa hakika ilifika japo kwa gharama kubwa mno.
Sasa nikiwa mzalendo ninayeipenda nchi yangu,nawaomba watanzania tuwe majasiri na tuwe wavumilivu kipindi hiki kuelekea October 25 hata tutakapoitwa VIBAKA,MAKAPI,OIL CHAFU,MAADUI na hatuwezi kujua pengine pia CCM watafikia hatua ya kutuita MAPANYA au MENDE(Inyenze).
LONG WALK TO FREEDOM...Alluta Continua!