Uchaguzi 2020 Walianza na Seriakli za Mitaa, sasa Uchaguzi ni mzaha tu

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
CCM walipoanza mchezo wa kitoto katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa, hatukujua kwamba tabia hiyo itakomaa. Sasa wameingia uchaguzi mkuu, mambo bado ni hayo hayo! Mtu anavamia fomu ya mgombea, eti Tume ya uchaguzi wanaamini vigezo havikufuatwa. Mwingine anaweka picha mwenzie anapinga eti resolution ya picha ni mbaya. Kwa ujumla imekuwa ni upuuzi ktk jambo la munimu kwa nchi.

Hii imetokana na ubora duni wa wanasiasa. Wengi hawana uwezo wa kusaidia nchi kwa lolote na hao ndo wanaingia ktk siasa. Wanaamini wanapata ubunge kwa mbinu na si ubora. Kwa haya yanayotokea na kwa kuwa yameachwa kuendelea, baada ya miaka 5 ijayo ubora wa wanasiasa wetu utaporomoka zaidi. Wakati tunafanya haya, wenzetu katiki East Africa wanainua viwango vya wanasiasa na kuweka masharti ya elimu. Kenya, Uganda na Rwanda hakuna Mbunge wa elimu ya Darasa la 7 Kwetu sisi hao ndo wenyeviti wa vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom