Walianza kuzuia nyumbani kwa Balali sasa wazuia kuingia BOT

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
2008-05-31 09:22:39
Na Mashaka Mgeta

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imepiga marufuku waandishi wa habari kuripoti kikao chake na Wabunge wa Kamati ya Fedha na Uchumi.

Hatua hiyo, ilifikiwa jana, ikiwa ni siku moja, baada ya wabunge kuhoji masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya benki hiyo.

Katika kikao cha juzi kilichofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, wabunge waliuliza maswali ambayo hata hivyo hayakujibiwa, badala yake, BoT iliomba kuwasilisha majibu hayo jana.

Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa, yalihusu hatua ya baadhi ya Watanzania, hususani viongozi wa umma, kuhifadhi fedha za kigeni kwenye benki za nje.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Dk. Abdallah Kigoda, aliwaambia wabunge hao juzi kuwa, baada ya kupata ushauri kutoka kwa Manaibu Gavana wa BoT, Bw. Enos Bukuku na Bw. Juma Reli, majibu ya maswali yao (wabunge) yangejibiwa jana.

Tofauti na kikao cha juzi ambapo waandishi wa habari waliruhusiwa, uongozi wa BoT ulidaiwa kuagiza walinzi wa geti kuu la kuingilia, kutowaruhusu waandishi wa habari.

``Tumeambiwa leo hamruhusiwi kuingia kwenye kikao cha wabunge Hakuna maelezo mengine yaliyotolewa zaidi ya hayo,`` alisema mmoja wa walinzi hao ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Kuzuiliwa kwa waandishi wa habari kumefikiwa huku uongozi wa BoT, kupitia Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa benki hiyo, D. J. Masawe, kuwaeleza wabunge juu ya kuwepo ushirikiano mzuri na vyombo vya habari, hivyo kutekeleza misingi ya uwazi.

Baadhi ya wabunge waliouliza maswali juzi ni Mbunge wa Iringa (CCM), Bi. Monica Mbega, aliyetaka kujua, chombo kinachotumika kuisimamia na kukagua utendaji wa BoT.

Mbunge wa Wawi (CUF), Bw. Hamad Rashid Mohamed, aliuliza maswali kadhaa, likiwemo kutaka kujua hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watu wanaohifadhi fedha za kigeni nje ya nchi.

Naye Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM), Bw. Hamza Mwenegoha, aliuliza mikakati ya BoT katika kulinda thamani ya dhahabu inayochangia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni na mauzo ya nje.

Mbunge wa Ilemela (CCM), Bw. Anthony Diallo, aliuliza ikiwa BoT inafarijika kutenda kazi ikiwa chini ya Wizara ya Fedha.

Bw. Diallo, alipendekeza kuwa, kutokana na majukumu ya kusimamia sera za fedha, ingefaa kama BoT ingekuwa chini ya chombo ama wizara nyingine.

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Bw. Siraju Kaboyonga, alipendekeza BoT kupanua wigo wa utoaji taarifa zake, hususan kupitia vyombo vya habari, ili ziwe wazi na kupatikana kwa urahisi kwenye jamii.

Pia alipendekeza kwa BoT kutoka hadharani na kuzungumzia mwenendo wa riba kubwa zinazotozwa na benki za biashara hapa nchini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Sumve (CCM), Bw. Richard Ndassa, alitaka kujua sababu za kushuka ubora wa sarafu wa Sh 100 na noti ya Sh 500.

Bw. Ndassa alitaka kujua ikiwa BoT haioni umuhimu wa kuziondoa sarafu za Sh 50 katika mzunguko wa fedha, kwa vile hivi sasa hazina matumizi makubwa.

Aidha, aliuliza kuhusu jitihada zinazofanywa na BoT kudhibiti `utitiri` wa maduka ya kubadilika fedha za kigeni nchini.

Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM), Dk. Omari Mzeru, alitaka kujua jitihada za BoT kufanikisha uanzishwaji wa benki na mipango ya utoaji mikopo kwa wakulima, kama sehemu ya kuinua uchumi wa wananchi walio wengi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mfenesini (CCM), Mossy Suleiman Mussa, aliuliza ikiwa BoT ina mkakati wa kuwatambua na kuwawezesha wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga, wanaochangia asilimia 30 ya pato la Taifa.

Naye Mbunge wa Kisarawe (CCM), Bw. Athuman Janguo, alitaka kujua ni wakati gani BoT inaingilia kati na kudhibiti nguvu ya soko inayochangia kupanda kwa thamani ya ununuzi wa Dola ya Marekani.
SOURCE: Nipashe
 
Hivi hii Benki inasimamia fedha za Taifa gani ambalo watu wake hawatakiwa kujua kinachojadiliwa..? Ushauri wangu kwa waandishi... gomeni kuandika taarifa zozote toka BoT wakiwaita msiende, wakitaka kutoa maelezo msikubali hadi waombe radhi kwa upuuzi huu. Hii nchi mbona inataka kuwa kama kigenge cha watu fulani hivi.

Yaani nyie mjadili fedha za watu wetu, mkiwa mmeshazungukwa na kashfa halafu mna balls za kuzidi kuleta usiri? Huu ni uhuni wa watu wenye pesa ambao wanafikiri wameumbwa kututawala milele na ya kuwa kutaka kujua kinachoendelea katika Benki "YETU" ni hisani na tuwaombe!!

Naombeni namba ya Gavana Ndullu.. pleaseeeee!
 
Huu ni ubakwaji wa uhuru wa vyombo vya habari unaofanyika mchana kweupeee tena bila haya. Its our bank, its our money, we have the right to know. Naunga mguu hoja ya MMK kuhusu waandishi wa habari kususia kuandika habari zote za BOT kwa muda.
 
Hiki wanajaribu kufanya hakitafanikiwa kwani wakibana official information zitapatina unofficial ambazo zitawaumbua zaidi kuliko wanavyofikiri, kwani ufisadi si ulianza kuleak kwa unofficial information wakaanza kupinga kuwa sio kweli lakini mwisho wa siku wakakubali
 
Sounds like "kuna mkono wa mtu hapa"; specifically Chenge na wenzake wengi tu. Hii ni damage control baada ya ofisa wa BoT kunukuliwa akisema kuwa na vijisenti nje ni kosa la kisheria (kama chanzo cha pesa hii kiko Tanzania). Can you imagine how many vigogo who are implicated by this statement? Some participated in enforcing this law (Chenge), some know this in and out like Mgonja na hata hizi akaunti za Che Nkapa zinazosemwa huko nje...yaani hii ni slip of tongue ambayo ni bora kuliko zote.

Once again, the ball is back to the government or BoT (whoever is an enforcer of this crime). What are you going to do about it? Naungana na Mzee wa kijijini kwa kusema waandishi waigomee BoT. No more PR for them. Watu walikuwa na sympathy nao and now they are kissing some you know what. Shame on Ndullu who some of us had highest regard in respect of being independent and have full autonomy from CCM pressure.
 
behind closing doors ni jambo la kawaida kwenye financial institutions. Kuna data ambazo mnataka ziwe public na kuna data ambazo zinakuwa kwa matumizi ya ndani tuu. Sioni tatizo liko wapi, kama kuna reason ya wao kufanya behind closing door then inabidi iheshimiwe.
 
Hivi hii Benki inasimamia fedha za Taifa gani ambalo watu wake hawatakiwa kujua kinachojadiliwa..? Ushauri wangu kwa waandishi... gomeni kuandika taarifa zozote toka BoT wakiwaita msiende, wakitaka kutoa maelezo msikubali hadi waombe radhi kwa upuuzi huu. Hii nchi mbona inataka kuwa kama kigenge cha watu fulani hivi.

Yaani nyie mjadili fedha za watu wetu, mkiwa mmeshazungukwa na kashfa halafu mna balls za kuzidi kuleta usiri? Huu ni uhuni wa watu wenye pesa ambao wanafikiri wameumbwa kututawala milele na ya kuwa kutaka kujua kinachoendelea katika Benki "YETU" ni hisani na tuwaombe!!

Naombeni namba ya Gavana Ndullu.. pleaseeeee!

Labda ni benki ya Tanzania huku ikihifadhi fedha za investors....
Hivi huyu NDULU alipokuwa deputy wa Balali, alikuwa anafanya nini kuzuia mihela isipite? Inamaana hakujua kuna ufisadi??? au ndo ile ondoa fisadi weka fisadi???? kuna mtu anadetails za Ndulu atumwagie hapa?
 
Labda ni benki ya Tanzania huku ikihifadhi fedha za investors....
Hivi huyu NDULU alipokuwa deputy wa Balali, alikuwa anafanya nini kuzuia mihela isipite? Inamaana hakujua kuna ufisadi??? au ndo ile ondoa fisadi weka fisadi???? kuna mtu anadetails za Ndulu atumwagie hapa?

Ndulu hakuwa deputy wa Balali, go check your facts plz. Ndulu amekuja lini BoT akitokea US?
 
nasikia ana maradhi fulani yasiyopona, si mnajua hawa watu wenye maradhi yasiyopona jinsi wanavyokuwaga na roho mbaya?ila iko siku yao na siku hiyo watajuta
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom