Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,896
2008-05-31 09:22:39
Na Mashaka Mgeta
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imepiga marufuku waandishi wa habari kuripoti kikao chake na Wabunge wa Kamati ya Fedha na Uchumi.
Hatua hiyo, ilifikiwa jana, ikiwa ni siku moja, baada ya wabunge kuhoji masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya benki hiyo.
Katika kikao cha juzi kilichofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, wabunge waliuliza maswali ambayo hata hivyo hayakujibiwa, badala yake, BoT iliomba kuwasilisha majibu hayo jana.
Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa, yalihusu hatua ya baadhi ya Watanzania, hususani viongozi wa umma, kuhifadhi fedha za kigeni kwenye benki za nje.
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Dk. Abdallah Kigoda, aliwaambia wabunge hao juzi kuwa, baada ya kupata ushauri kutoka kwa Manaibu Gavana wa BoT, Bw. Enos Bukuku na Bw. Juma Reli, majibu ya maswali yao (wabunge) yangejibiwa jana.
Tofauti na kikao cha juzi ambapo waandishi wa habari waliruhusiwa, uongozi wa BoT ulidaiwa kuagiza walinzi wa geti kuu la kuingilia, kutowaruhusu waandishi wa habari.
``Tumeambiwa leo hamruhusiwi kuingia kwenye kikao cha wabunge Hakuna maelezo mengine yaliyotolewa zaidi ya hayo,`` alisema mmoja wa walinzi hao ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Kuzuiliwa kwa waandishi wa habari kumefikiwa huku uongozi wa BoT, kupitia Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa benki hiyo, D. J. Masawe, kuwaeleza wabunge juu ya kuwepo ushirikiano mzuri na vyombo vya habari, hivyo kutekeleza misingi ya uwazi.
Baadhi ya wabunge waliouliza maswali juzi ni Mbunge wa Iringa (CCM), Bi. Monica Mbega, aliyetaka kujua, chombo kinachotumika kuisimamia na kukagua utendaji wa BoT.
Mbunge wa Wawi (CUF), Bw. Hamad Rashid Mohamed, aliuliza maswali kadhaa, likiwemo kutaka kujua hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watu wanaohifadhi fedha za kigeni nje ya nchi.
Naye Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM), Bw. Hamza Mwenegoha, aliuliza mikakati ya BoT katika kulinda thamani ya dhahabu inayochangia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni na mauzo ya nje.
Mbunge wa Ilemela (CCM), Bw. Anthony Diallo, aliuliza ikiwa BoT inafarijika kutenda kazi ikiwa chini ya Wizara ya Fedha.
Bw. Diallo, alipendekeza kuwa, kutokana na majukumu ya kusimamia sera za fedha, ingefaa kama BoT ingekuwa chini ya chombo ama wizara nyingine.
Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Bw. Siraju Kaboyonga, alipendekeza BoT kupanua wigo wa utoaji taarifa zake, hususan kupitia vyombo vya habari, ili ziwe wazi na kupatikana kwa urahisi kwenye jamii.
Pia alipendekeza kwa BoT kutoka hadharani na kuzungumzia mwenendo wa riba kubwa zinazotozwa na benki za biashara hapa nchini.
Kwa upande wake, Mbunge wa Sumve (CCM), Bw. Richard Ndassa, alitaka kujua sababu za kushuka ubora wa sarafu wa Sh 100 na noti ya Sh 500.
Bw. Ndassa alitaka kujua ikiwa BoT haioni umuhimu wa kuziondoa sarafu za Sh 50 katika mzunguko wa fedha, kwa vile hivi sasa hazina matumizi makubwa.
Aidha, aliuliza kuhusu jitihada zinazofanywa na BoT kudhibiti `utitiri` wa maduka ya kubadilika fedha za kigeni nchini.
Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM), Dk. Omari Mzeru, alitaka kujua jitihada za BoT kufanikisha uanzishwaji wa benki na mipango ya utoaji mikopo kwa wakulima, kama sehemu ya kuinua uchumi wa wananchi walio wengi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Mfenesini (CCM), Mossy Suleiman Mussa, aliuliza ikiwa BoT ina mkakati wa kuwatambua na kuwawezesha wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga, wanaochangia asilimia 30 ya pato la Taifa.
Naye Mbunge wa Kisarawe (CCM), Bw. Athuman Janguo, alitaka kujua ni wakati gani BoT inaingilia kati na kudhibiti nguvu ya soko inayochangia kupanda kwa thamani ya ununuzi wa Dola ya Marekani.
SOURCE: Nipashe