Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kama mkumbukavyo kauli ya Rais wa awamu hii ya tano, Mheshimiwa Magufuli kuzuia mikutano ya vyama vya kisiasa vya upinzani, alilolitoa mwaka 2016 na vyombo vya usalama kulichukulia tamko hilo kuwa ni sheria na Jeshi la Polisi, kuanza kukamata kila kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa anataka kupingana na kauli hiyo ya Rais!
Akaja waziri wa Habari kuanza kuzuia urushaji mubashara wa vipindi vya televisheni, vilivyokuwa vikionyeshwa awali, kwa sisi wananchi kuwaangalia Live, wawakilishi wetu namna wanavyotutea Bungeni, nayo ikapigwa FULL STOP
Wakaja kwenye vyombo vya habari vya binafsi kuvidhibiti kwa hali ya juu, kwa chombo chochote cha habari kitakachotoa habari ambazo ni "negative" kwa serikali hii ya awamu ya tano, navyo vikaangukiwa na rungu la kufungiwa
Mifano michache ya magazeti yaliyofungiwa maisha ni Mwanahalisi,Mseto na Michapo
Lakini ambacho kimewastua watanzania wengi ni kuona kuwa kumbe hata simu zetu binafsi, zinaweza dukuliwa!
Mifano halisi, ni namna simu za watu mashuhuri nchi hii walivyodukuliwa siku zao, katika siku za hivi karibuni
Nimekuwa nikijiuliza hivi kumbe hawa jamaa wa TCRA hawana "private policy" kwenye mitandaoni yao??
Iweje kama mitandao yao INA hiyo "privacy policy" simu za hao watu mashuhuri ziweze dukuliwa??
Kama ndiyo hivyo, ni kwanini basi wameshindwa kudukua simu za waliokuwa wanapanga njama za kutaka kumwua mbunge wetu Tundu Lissu na badala yake hivi sasa yakaribia miaka miwili wameendelea kutuamimlnisha kuwa hao watu waliokuwa wamepanga jaribio hilo la mauaji, ni WATU WASIOJULIKANA!
Vile vie watu waliopanga njama za kumteka mwandishi wa habari Azory Gwanda, kule Rufiji ni lazima mawasiliano yao ya simu yapo kwa hao wadukuzi
Jambo ninalojiuliza ni kwa vipi hawataki "kulikisha" mawasiliano hayo na badala yake wanaendelea kutusminisha watanzania kuwa watu hao ni WATU WASIOJULIKANA??
Vile vile makampuni ya simu ni lazima waelewe kuwa biashara yao ya maongezi ya kwenye simu itaahirika sana, kwa kuwa hata Mimi nitaogopa kuongea na "mchepuko" wangu nikiamini kuwa NITADUKULIWA!