Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Ripoti zinasema Bw David Evans alikuwa na mkewe Michelle katika hoteli hiyo kwa chakula cha jioni
Mmoja wa wahudumu alienda mezani mwao kuuliza kama wanafurahia chakula chao, akasema nyama ilikuwa ngumu na ukitafuna ni kama anayetafuna mipira. Inaaminika mhudumu huyo alipitisha ujumbe huo kwa mpishi mkuu
Inaelezwa kuwa Bw Evans mwenye umri wa miaka (42) alimfuata mpishi huyo hadi jikoni kwa ghadhabu na baada ya kujibizana kwa sekunde chache, mpishi akamrushia pilipili (masala) usoni iliyokuwa kwenye sahani
Akieleza matukio hayo kwa mashirika ya habari, mke wake alisema "Mpishi huyo mwenye asili ya Bara la Indi alikuja mezani kwetu kwa jeuri na hasira akatukashifu kwamba tunataka kuhepa kulipia chakula
Tulisema tutakula chakula kingine chote kilichokuwa mezani lakini nyama haiiliki,alianza kunitusi kwa hivyo Evans akamwambia" hakuna haja ya kumtusi mke wangu" lakini akaendelea kupiga kelele ndipo Evans akamfuata hadi mlango wa jikoni kumtaka aombe msamaha"
Picha zilizochapishwa na mashirika ya habari zilionyesha jamaa huyo akiwa amefura uso hasa macho yake ambayo yaligeuka mekundu na hangeweza kuyafungua