Walemavu wahoji: Serikali ya Magufuli ni katili hivi? Hatujawahi fanyiwa hivi na serikali yoyote

Haya CHADEMA, dili ingine hiyo. Sheria zinasema aeiou, wengine wanaganya babebibobu. Sheria inapochukua mkondo wake, hooo serikali dhalimu.
Hii serikali naijua vizuri ilivyokatili, lengo lilikuwa kuwaua ili ikusanye rambi rambi. Siku zao zilikuwa hazijafika. Naona sizonje kachukia sana huko
 
Naombeni tafsiri ya wanyonge.
Maana nilitegemea hao walemavu ndio wangekuwa sehemu sahihi ya neno hili
Wanyonge namba 1:Wabunge wa kijani 2:Wenye kadi za kijani na wale wanaovaa vitambaa, kofia, kanga na tisheti za kijani 3:Wale wanaosema ndioooooooooo kwa kila kitu kinachofanywa na Sizonje. Hatuna wanyonge wanaotambulika zaidi ya hao.
 
Tunaendelea kutengeneza taifa la watu wenye mioyo magumu na wasiokuwa na utu ndio maana kuna watu wanasifia vitendo vya kikatili na vya kitaahira walivyofanyiwa walemavu, kama tunda lilivyo mbegu tumeambiwa na chuki ni mbegu, itamea.
 
0d76827b9e6428f4f5156848d4d0eaf7.jpg
 
Inasikitisha sana kuwapiga watu wasioweza kujitetea! Polisi wetu inapaswa wafundishwe mbinu sahihi za kufanya kazi zao! Na hao ndugu zetu walemavu inabidi sasa waelewe kuwa ccm haina mahaba ya dhati juu yao ila hutumika tu kwa malengo maalum hasa wakati wa kampeni!
 
Mwenyekiti wa chama cha walemavu Dar Hamad Abdallah Komboza akiongea na waandishi wa habari amehoji polisi kutumia nguvu nyingi kuwapiga kiasi kile na kusema hii haijawahi kutokea awamu yoyote ile ila ni awamu hii na kusema watawaombea dua ili Mungu awape viongozi walionyanyasa walemavu nao wapate ulemavu pia.

Wamesema wanaomba wapewe eneo lao la kufanyia biashara kwa kuwa wao ni kundi maalumu na pia hata namna ya kushughulika nao ingekuwa maalumu na watangulize utu kwanza na sio sheria kwanza

Ameomba jeshi la polisi liwaombe radhi kwa kitendo walichofanyiwa
Wahanga wapewe fidia
Na askari waliofanya kitendo kile wachukuliwe hatua na iwe mwanzo na mwisho kufanyiwa hivyo



Mwenyekiti hajasikia tu mbona Waziri wa mambo ya ndani ameomba msamaha tayari?!
 
Back
Top Bottom