Walemavu wahoji: Serikali ya Magufuli ni katili hivi? Hatujawahi fanyiwa hivi na serikali yoyote

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,803
2,000
Mwenyekiti wa chama cha walemavu Dar Hamad Abdallah Komboza akiongea na waandishi wa habari amehoji polisi kutumia nguvu nyingi kuwapiga kiasi kile na kusema hii haijawahi kutokea awamu yoyote ile ila ni awamu hii na kusema watawaombea dua ili Mungu awape viongozi walionyanyasa walemavu nao wapate ulemavu pia.

Wamesema wanaomba wapewe eneo lao la kufanyia biashara kwa kuwa wao ni kundi maalumu na pia hata namna ya kushughulika nao ingekuwa maalumu na watangulize utu kwanza na sio sheria kwanza

Ameomba jeshi la polisi liwaombe radhi kwa kitendo walichofanyiwa
Wahanga wapewe fidia
Na askari waliofanya kitendo kile wachukuliwe hatua na iwe mwanzo na mwisho kufanyiwa hivyo

 

WILLIAM MARCONI

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,056
2,000
Inasikitisha sana.
Toka aingie Sizonje wanajisifu na kutamba wamerudishiwa 'heshima' yao ya 'kutumia nguvu pasipo na akili'

Poleni walemavu.
Haya CHADEMA, dili ingine hiyo. Sheria zinasema aeiou, wengine wanaganya babebibobu. Sheria inapochukua mkondo wake, hooo serikali dhalimu.
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,193
2,000
Yupo pwani anasema yeye ni wa wanyonge, sasa sijui hawa walemavu ni nani? Hivi unapomwambia mlemavu bajaji yake ni kero kuingia mjini lakini ma v8 200 si kero kuingia mjini hawa watu wanafundishwa nini?! Hawana uwezo wa kutembea zaidi ya kutumia bajaji basi wapewe na wao hayo magari au wasubiri zile Noah za ACCACIA? AIBU HII HAIWEZI KUFUTIKAWALA KUMUACHA SIZONJE SALAMA.
 

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,210
2,000
Waziri wa Home affairs Mwigulu Nchemba ameshaomba radhi kwa niaba ya jeshi la polisi ila kwa issue ya kulipwa fidia hao victims sina uhakika kama limezungumziwa.
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,409
2,000
Hivi aliposema, "I wish I could be IGP" kumbe hawakumwelewa? Vitendo huwa vinaongea zaidi kuliko maneno. Sasa ameeleweka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom