Walemavu wafunga barabara makutano ya Uhuru na Kawawa wakipinga kuvunjiwa vibanda vya biashara

KISHINDO

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
2,108
1,798
Umati wa Walemavu wamefunga makutano ya barabara katika mataa ya Ilala na kusababisha magari kutokupita.

Madai yao makuu ni kwa serikali kwamba haiwajali, Bora iwaue tu kuliko kuachwa wakiishi kwa tabu huku vibanda vyao vilivyopo sokoni Karume vikibomolewa.

Naripoti toka eneo la tukio.
walemavu.png
1432205534179.jpg
 

Attachments

  • IMG-20150521-WA0019.jpg
    IMG-20150521-WA0019.jpg
    27.5 KB · Views: 410
  • IMG-20150521-WA0021.jpg
    IMG-20150521-WA0021.jpg
    26.8 KB · Views: 396
  • IMG-20150521-WA0022.jpg
    IMG-20150521-WA0022.jpg
    31.3 KB · Views: 402
Watu wenye ulemavu wameamua kuzuia njia kwa kulala barabarani katika makutano ya barabara ya Uhuru na Kawawa kupinga kuvunjiwa meza zao za biashara na askari wa jiji.

Magari mengi yamekwama, watu waamua kutembea kwa miguu. Jeshi la polisi linafanya nao mazungumzo kwa njia ya amani ili watoke, polisi hawatumii nguvu kuwaondoa.

Chanzo: ITV BREAKING NEWS.
 
Naisubiri kwa hamu sana hio siku ifike....itafika tu maana Wakati ni mwamuzi asiye na upendeleo!
 
Uzembe wa watu wachache unasabisha usumbufu mkubwa kwa wasio na hatia.
 
huu mwezi ni Special kwa migomo nini walianza wanafunzi vyuoni leo tena ndugu zetu hawa na kesho je nani atahusika????
 
JEshi letu ni mabingwa wa kuwamwangia watu maji washa.

Sasa tuone kama wanaweza kuyatumia na leo.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hawa Askari wa jijini wapuuzi sana mnavunja vibanda vya walemavu mnataka waishi maisha gani inabidi Jiji libebe majukumu yote kuwalipa fidia na kuwatafutia eneo maalumu hapo Karume.
 
Ni kweli serikali inashindwa kuwaondoa walemavu 20 wanaotesa raia na kuzorotesha shughuli za kiuchumi!
 
Wapigwe tu! / ulemavu sio kigezo cha kuvunja taratibu za nchi wana haki sawa na watu wengine / serekali iache ulegelege kwa mambo ya kipuuzi namna hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom