Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Kuna seller wako fasta sana
Sellers huwa wazito kukujibu, Ila wao sasa wakiwa na shida na wewe wanakuchangamkia balaa. Mi niliagiza Xiaomi Mi Store, yalibaki kama masaa 3 muda wa kuprocess kuisha na ye bado hajatuma mzigo, mbona nilipigiwa WhatsApp call saa 12 asubuhi.
 
Msaada bandugu....... Mwenzenu simu yangu ina Font type moja tu. Nikitaka kubadili ni lazima ni download kwa kununua. Inafanyikaje hii? Au kama kuna utundu mwingine naweza utumia. Natumia Redmi Note 7 Pro.
 
Kama ni kweli basi itakuwa ndio mwisho wa kuagiza vitu vidogo vidogo kama SD card na flash au ikibidii labda kuanzia 5pcs !!
Hii ni bei ya kutoa mizigo kule RDP (mizigo ya kodi) , mizigo ya DP unachukua kwa bei ile ile ya 2350 na mizigo ya FGN unachukua bure kabisa... Nimetoka huko Alhamis kuchukua mizigo yangu.
 
Shida namtafuta seller fantacy kupitia profile yake ya AliExpress ili nipate Bei aliyoandika ila hajajibu hadi sasa

Sasa sijui kuna njia nyingine naweza tumia kumpata
Mkuu tulia kidogo hadi tarehe 8 wakimaliza hii sikukuu yao fantacy tech atakuwa ameshakupa jibu, au pitia kwenye comments zile za wengine wenye order kama yako na unaweza kukuta mmoja wao kaandika declared value.
 
Asante mkuu ngoja nifatilie
Mkuu tulia kidogo hadi tarehe 8 wakimaliza hii sikukuu yao fantacy tech atakuwa ameshakupa jibu, au pitia kwenye comments zile za wengine wenye order kama yako na unaweza kukuta mmoja wao kaandika declared value.
 
Hii ni bei ya kutoa mizigo kule RDP (mizigo ya kodi) , mizigo ya DP unachukua kwa bei ile ile ya 2350 na mizigo ya FGN unachukua bure kabisa... Nimetoka huko Alhamis kuchukua mizigo yangu.
Kuna mdau aliomba ufafanuzi hizo DB, FGN RDP zinakuwaje vigezo gani hutumika kupewa hizo lebo?
 
Nimefanikiwa kupata declaration kwenye feedback
Ila sijajua kama nisubiri hadi wanitumie msg kama posta au niende nikachukue hivyo hivyo maana mzigo wameuteka tangu tarehe 4 mwezi huu
Mkuu tulia kidogo hadi tarehe 8 wakimaliza hii sikukuu yao fantacy tech atakuwa ameshakupa jibu, au pitia kwenye comments zile za wengine wenye order kama yako na unaweza kukuta mmoja wao kaandika declared value.
 
Nimeagiza Xiaomi wireless wearbuds kwa aliyewai kuzitumia vp quality zake na features zingine, please share jamvini hapa
 
Kuna mdau aliomba ufafanuzi hizo DB, FGN RDP zinakuwaje vigezo gani hutumika kupewa hizo lebo?
Mzigo kuwa FGN au DP inategemea na tracking number utakayopewa, nikimaanisha kama seller atakutumia mzigo kawaida au kama Regista.

Kwa uzoefu wangu mimi FGN inakuwa mizigo ile niliyolipia shipping na tracking number yake inakuwa inaanza na R (RP au RB kutegemea kama mzigo umetumwa na China Post au Singapore post) kuna ile ya LP pia nimepokea kama FGN.

DP inakuwaga sana sana ile mizigo yenye tracking number zinazoanza na U (UC/UN/UG) hii ndio ile mizigo yetu inayochukuwa miezi kuwasili. Na hapa kuna mawili kuna ile mizigo unapokea (kwa Dar pale posta makao makuu) kule counter number kumi na Private bag, sasa hapa sielewagi maana kuna mizigo nanunua kutoka eBay na shipping nalipa bei kubwa sana alafu napokea Private bag na bado natoa 2350.

RDP hii mara nyingi ni mizigo ile ya bei kubwa au ina vitu kama nguo, viatu, begi au electronics ambayo inaonekana taxable na TRA. Tracking number yake pia inakuwa inaanza na R. Kwa mimi mizigo yangu iliyoingia huku ilikuwa na tracking number ya (RF, RY, RV) <--- sijui kama ni wote inawakuta, lakini kwa mimi hizi tracking number hazijawahi kukosekana na "customs" zikifika.
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom