Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Hapo nyuma nimeagiza mizigo mingi sana ikiwemo simu kadhaa sikuwahi kukutana na tozo pale posta.
Lakini sasa imefika mizigo mitatu kila mzigo naambiwa niulipie Tsh 2350. Na ni small packages.
Na hata shipping mzigo miwili nimelipia shipping.
Lakini risiti inaonesha ni gharama za shipping.
Mizigo yote yenye tracking inayoanza na "R" (registered mail) huwa haulipii ila kama tracking no. Sio "R" wanakuchaji hiyo 2350.
 
Wale wanazingua sana..utendaji wao labda unazidiwa kiwango mana haiwezekani for 5 days mzigo umesimama tuu
Hawa sijui wanachanganya nini! Mfano cheki mzigo wangu ulitakiwa uje posta ya mbagala cheki ulivyozunguka
Screenshot_2019-09-10-10-10-59-688_com.android.browser.jpg
 
Angalia hizo tracking no. Ukiona no. Ya tracking imeanzia na "R" hapo hawatakulipisha hiyo 2350.
Fafanua manake kuna mda nilishaweka hiyo kitu hapa jukwaani . kuna wadau walibisha sana, na kwa kua sikua na ushahid wa kutosha nami niliaminishwa tu kua ni hivyo.
Kama kwa namna moja au nyingine unahusika na mamlaka husika tusaidie kwa faida ya jf
 
Fafanua manake kuna mda nilishaweka hiyo kitu hapa jukwaani . kuna wadau walibisha sana, na kwa kua sikua na ushahid wa kutosha nami niliaminishwa tu kua ni hivyo.
Kama kwa namna moja au nyingine unahusika na mamlaka husika tusaidie kwa faida ya jf
Wadau walibisha kwamba ni kodi, hiyo 2350 sio ile kodi ya TRA ni service charge ambayo posta wenyewe wanacharge. Import tax ukichajiwa huwa unalipa kama 21% ya bei ya kununulia bidhaa. Mara nyingi hawa wanaotutumia mizigo huwa kwenye package wanaandika bei ya chini ndio maana customs hawatucharge.
 
Back
Top Bottom