Wale wote tunaojianda kupeleka barua za Uchumba 2017/2018 karibuni

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Wadau Karibuni sana wale wote wenye Malengo na ambao tupo kwenye maandalizi ya kwenda kujitambulisha ukweni Karibuni tupeane maujuzi
1:Mavazi gani siku ya mahari
2:Umemjua vya kutosha mchumba
3:Mkoani au mkoa mmoja
Karibuni wote
 
hapo ngoja waje lakini pia nina swali ... kama unataka kwenda ukweni je ni lazima bint awepo nyumbani kwao au anaweza akapewa taarifa tuu
 
images-257.jpg

Kwenye mavazi, piga kama hivyo
 
hapo ngoja waje lakini pia nina swali ... kama unataka kwenda ukweni je ni lazima bint awepo nyumbani kwao au anaweza akapewa taarifa tuu
kuna stage mbili
1:Wazee wanapeleka barua ya uchumba ww auta kuwepo wala mchumba hata kuwepo labda wazee wamuombe kumuona
2:kupelela mahari hapa wote mtakuwepo pia vijana wa kisasa wa napenda kuvalishana Pete ila mm ctofanya mbele ya wazee
 
hapo ngoja waje lakini pia nina swali ... kama unataka kwenda ukweni je ni lazima bint awepo nyumbani kwao au anaweza akapewa taarifa tuu
Lazima binti awepo wakati wa posa.
Sababu kubwa ya binti kuwepo ni kwamba yeye ndie anae kufaham wewe, yaani kwalugha nyepesi binti ndie atakua mwenyeji wako pale nyumbani kwao
 
Lazima binti awepo wakati wa posa.
Sababu kubwa ya binti kuwepo ni kwamba yeye ndie anae kufaham wewe, yaani kwalugha nyepesi binti ndie atakua mwenyeji wako pale nyumbani kwao
mh sidhani ww utaenda sehemu bila kuandaa mazingila
 
mavazi simple tu
1:koti jepesi LA kubana
2:Cardet yako black au milk white
3:Simple shoes
4:Watch
 
Aisee mi nimeshapavuka hapo nipo hatua ya kupeleka mahari aisee nimepigwa parefu mbaya
 
mh sidhani ww utaenda sehemu bila kuandaa mazingila
Mkuu.....
Unadhani wewe ndie utaenda kujitambulisha kwao na mchumba wako pasipo uwepo wake?
Je hayo mazingira, niwewe ndie utakae yaandaa kwao na unae enda kumchumbia?

Kwenye kuoa lazima uwepo wako halisi uonekane.
1: Siku ya posa
2: Siku ya ndoa
 
posa unakuwepo ila siku ya kupeleka barua ya uchumba
 
ulijuaje kama wiki hivi niliitwa na dada wa mchumba angu mtarajiwa nilipofika huko nikabanwa na maswali ya ajabu lengo lilikua kujua msimamo wangu kabla sijachukua hatua ya kupeleka barua kwa mshua ake sasa sijui walikua sahii au laa.
 
walikuwa sahihi maana ni vizuri umepata MTU wa kukutetea Dada na mdogo MTU hata mm kabla ya kupeleka lazima nianze kujenga urafiki na dada yake kwanza
 
hapo ngoja waje lakini pia nina swali ... kama unataka kwenda ukweni je ni lazima bint awepo nyumbani kwao au anaweza akapewa taarifa tuu
Na kwa kuongezea kabla ya kutuma posa,,ni vizur ukawa unafahamika kwao,,yaan umeshatambulishwa kwao kwamba huyu ni mwenzangu then posa ndio inafuata,,maana posa ni kutoa taarifa ikiwezekana na mahar kabsa sasa haiwezekana ikaanza posa bika hata kujua nyumban kwao.. Hakuna mzaz anaweza anaejielewa anaweza kupokea posa bila kumwambia binti mlete kwanza huyu mwenzako nyumban wamjue ndipo posa inafuata.

Baadhi wanafanya family meeting kabla hta ya posa so wanakua wanaelewana vzr na familia zinafahamiana kwa mapana... Tchao
 
Back
Top Bottom