Wale wote ambao Waliishia tu kwenye Interview za kutaka kuingia JKT tusimuliane ilikuwaje

Okwanyo58

JF-Expert Member
May 3, 2020
1,554
2,000
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2016 Mkoani Ofisi ya Mkuu wa Wilaya nimeingia pale ndani nikiwa nimeshavaa kiheshima mpaka basi,

Nimekutana pale Wanajeshi tofauti wenye Vyeo wamezunguka Meza huku ya Veti vyangu Original vinazunguka Mikononi Mwao, Yani nilitegemea ntaulizwa Mambo kama Mkuu wa majeshi ni nani! Au mkuu wa mkoa/Wilaya jina lake, Nikawa nimejiandaa vya kutosha

Ila niliulizwa tu mwaka wangu wa kuzaliwa basi harafu nikaabiwa nikasubiri nje? Kipindi hicho Mkuu wa wilaya ni Polepole alitunaga vibaya sana kwamba huko mnaenda kulima bamia harafu mnarudi watupu,🤣

2017 nikajaribu pia ila nikaangukia pua, Tuambizane wewe pia ulishaishia kwenye interview tu au uliendelea mpaka mkoani.
 
Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,030
2,000
Nilipita kwenye interview mpaka mkoani nikachaguliwa kwenye depo then tulikaa sana home,siku tuliyopangiwa kwenye mafunzo nilikuwa tayari nimepata dili kuliko nilivyotarajia sikwenda na sikuwaza kabisa kuhusu JKT, wenzangu walioenda walirudishwa mtaani baada ya miaka 3.

Ahsante Mungu, huwa nakaa nakumbuka sana hili swala ningeenda ingekuwaje?
 
karue

Member
Oct 31, 2018
62
125
Hii habari inanitoa machozi sana,mwaka 2011 nikiwa mwanza wilaya ya Ilemela ofisi ya mkuu wa wilaya tulipewa interview ya kukimbia kilometa kama kumi hivi na watu tulikuwa wengi sana na waliitajika kama watu 40 hivi,namshukru sana mungu nilikimbia kwenye group letu nilikuwa wa 3 kati ya watu 100.

Tulivyo maliza mbio washindi tukasomwa tukaingia ukumbini wakaanza kukagua vyeti.
Ikafika zamu yangu yule kaimu mkuu wa wilaya alikuwa mama mmoja hivi jina limenitoka aliniambia ukuona fani nyingine hadi uje uku ? Kwanza sura yako na ya cheti haiendani nikajitetea hakunielewa akawambia mgambo Mara moja nitolewe nje na nisionekane pale na vyeti vyangu alinirushia nje nikaokotewa na watu wengine tu.

Kumbuka tumekimbia km 10 kwenda na kurudi miguu ilipasuka na ngozi ya chini imebanduka banduka

Nililia sana baba angu akanichukua kwenye baiskel tukaanza kurudi nyumbani.

Hadi Leo hii ninavyoandika ujumbe huu mkuu wa wilaya ya ilemela 2011 sitokuja kukusahau maisha yangu yote uliniumiza moyo wangu sana.

Mungu ni mwema alinipa kazi nyingine
 
Pole sana mkuu,
 
Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
319
500

Cheti kilikuwa na shida gani mkuu..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom