Wale wenye hisa Tol Gas hivi mmeona gawio?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,095
2,000
Hii kampuni ya Tanzania oxygen Tol Gas hakika imekua pasua kichwa kwa wanahisa wake.

Ndio ya kwanza kuingia soko la hisa Dar es salaam ila hawajawahi kutoa gawio tangu wameingia soko la hisa hadi jpm juzi alipoanza kukaba mashirika na kampuni zenye hisa za serikali kutoa gawio ndio wametoa kigawio kiduchu Shs 17 kwa hisa.

Kampuni ina uwekezaji mkubwa kazi wakurugenzi na mameneja kujilimbikizia mafao wanahisa hawapati kitu utafikiri kampuni imekua yao. Hicho kigawio walichotangaza wanazungusha tu wanahisa wala hawatoi hadi sasa.

Inaelekea kama wajanja wamejibinafsishia Tol kiujanja, wanakula wao faida.
 

mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,314
2,000
Hiyo kusema ndio kwanza wameingia soko la hisa utakuwa hujui vizur TOL. Hongera kama umepata gawio kiongozi.
 

Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
26,896
2,000
Minimum shares 100x17=1,700. Mwenye 100,000 shares 100,000x17=1,700,000. Gawio dogo sana hili. Thamani ya hisa kwa sasa ni shs ngapi?

Nadhani soko la hisa bongo kwa sasa ni msiba.
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,504
2,000
Hisa haijawahi kumkwamua mtu kiuchumi katika nchi zetu hizi. Labda kama unataka pakutunzia pesa yako tu

Kuna jamaa anauza hisa zake za voda huko kwa bei yoyote na hajapata mteja
 

Einsten

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
589
250
Minimum shares 100x17=1,700. Mwenye 100,000 shares 100,000x17=1,700,000. Gawio dogo sana hili. Thamani ya hisa kwa sasa ni shs ngapi?

Nadhani soko la hisa bongo kwa sasa ni msiba.
Niendelee tu kutrade forex nikipigwa leo kesho napga . nitafute pesa kwa jasho alaf nmlishe mtu ns mkewe watoto zake wakasome ulaya kwa pesa yangu alaf mm niambulie patupu??? Nawashangaa sana wanaoendelea kuwekeza kwenye hisa Bongo.
 

t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
2,018
2,000
kama hukununua hisa nyingi ni vema ukakata tamaa
na gawio
 

t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
2,018
2,000
Hisa haijawahi kumkwamua mtu kiuchumi katika nchi zetu hizi. Labda kama unataka pakutunzia pesa yako tu

Kuna jamaa anauza hisa zake za voda huko kwa bei yoyote na hajapata mteja
kwa walionunua hisa za breweries na sugar pale mwanzoni zilisaidia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom