Wale wenye 35+yrs na hawajaanza kuota mvi mkuje hapa...

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,373
6,756
Jamani!
Mbona naona vijana wa siku hizi wanazeeka haraka?
Yani nikiangalia wazee wengi wana nywele nyeusi tii labda na vimvi vichache tu. Ila vijana sasa... Vichwa vimejaa mvi... Tena wengi ni below 35.
Nini kimekikumba hiki kizazi chetu?
Embu ambao mmevuka 35 na hamjaota mvi mkuje hapa mshee lifestyle yenu...
 
Kuna changamoto ya vyakula tunavyokula sometimes hata mafuta tunayojipakaa miilini mwetu,ukitaka kuamini hili sogea vijijini utakutana na vijana waliojaa stress ana familia ya watoto wanne hajui watakula nini watavaa nini au atawaachia nini ila mvi hana njoo sasa humu mijini kijana hana mtoto hata mmoja kichwani nywele nyeupe!

Pia wengine ni maumbile tu,unakuta wana mvi za kurithi.
 
Ninachofahamu mvi za kichwani zipo hadi za kurithi, lakini za kidevuni ni utu uzima umepiga hodi.
 
Vyakula vya mafuta mengi,
Chipsi
Chapati
Mandazi
Sambusa
Soseji
Kachori
Na kuzidisha mafuta mengi kwenye chakula sasa hivi ni fashen hasa mijini.

Lazima uote mvi mapema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom