Wale wanaouza mabegi, vitenge kwa mnada na kurusha pale Ilala na Karume ni matapeli

Wale wanaouza mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha pale Ilala na karume ni matapeli

Unanunua kitenge unapewa begi bure na rubega 3 bure kwa elfu 5 tu Ngoja niwape taarifa mchukue tahadhari

Kwanza sipo hapa kuharibu biashara za watu. Ni hivi katika ya karume na ilala njiani pale kwenye kibao cha shule ya michikichini kunakuaga na wakaka wanauzaga nguo,mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha juu

Mtu ananunua Tisheti moja anapewa zawadi ya begi kubwa bure, Vitenge vya wax kigoma anapewa pair tatu bure, na rubega aka mkorori mbili bure hapo kanunue tishert ya 3000.....huu ni utapeli

Ngoja niwaambie wanachofanyaga Wanatafutaga kinadada ambao ni watu wao na kina kaka wanawachanganya katika ya watu kwahiyo wakiwa wanauza wanatupa ofa kama hizo wanawatupia wale wanawake wao kwamba eti ionekane kanunua kitenge kwa buku kapewa begi bure, mashuka bure na mashuka ya kimasai bure.

Wakishawarushia watu wao utaona wale wadada mmoja mmoja kwa wakati wake akijifanya anaondoka akifika huko ndani ndani anaenda kumkabidhi mtu wao maalum ambaye naye huzirudisha stoo then watazitoa kwa njia nyingine na kuzirudisha hapo mnadani.

Wanaopigwa na wapita njia ambao watavutiwa jinsi watu wanavyozawadiwa vitu basi wewe mpita njia utajiunga, watakuambia ununue tishet kwa elfu kumi then wanakwambia utulie watakupa zawadi ya bure, utaendelea kusubiria huku ukiona wenzako (wale watu wao) wakiendelea kuzawadiwa vitu kibao, wakiona una wasiwasi watakuambia nunua sasa upate mabegi mawili bure, utanunua utaambiwa mwishoni utapewa zawadi mwisho wa siku watafunga mnada na kusema usubiri wanakuja then watapotea wote mmoja mmoja.

Hao wadada na wakaka ambao ni watu fatilia kwa makini hata wakinunua wakitupiwa hizo zawadi ukiangalia kwa makini anayekusanya pesa za wanaolipa akiwasogelea wanajifanya wanatoa pesa lakini hawalipi anamsogelea masikioni na kumpa maelekezo kwamba ninini cha kufanya

Cha ajabu utakuta hao wadada wanaojichanganya na wanunuzi ni wao tu ndo hurushiwa hayo mabegi na mavitenge na zawadi halafu baadae wanarudisha kimya kimya hadi wanapoendaga kuviweka ili virudishwe mnadani napajua

Halafu hao hao wadada wanaojifanyaga wanunuz nawakutaga hapo kila siku kingine kama jioni au giza linaingia ili muuza mnada mtu wao aweze kuwatambua wadada wote hufunga vilemba, mitandio au vitambaa au kanga kichwani ili waweze kuwatambua.

Huo ni utapeli unaoendeleaga hapa ilala kwetu nimewapa taarifa mapema msanuke maana kila siku watu hulizwa hapa hubaki wakilia, yaani kila siku ni lazima nikute watu wakilia hapo na wengine wanaondokaga nyumbani na hela au kabeba hela kwa ajili ya mambo ya msingi akifika hapo anamalizia kwa hao matapeli anabaki bila hata nauli

Juzi kuna mama kalizwa kama elfu 90 hivi na alikopa Kwenye kikundi yule mama ilibidi aombe nauli, mwingine ni mtoto wa shule mpita njia aliona tishet kali akajichanganya elfu 50 aliyopewa na mzazi ikaliwa na wahuni akabaki akilia na kusaga meno.

Kuweni makini na hao matapeli wa mnada hapo njia ya kuelekea kati ya ilala na karume na huo mnada mara nyingi hufanyikia pale kilipo kibao cha shule ya michikichini Wapita njia kuweni makini
Hata wangetoa ofa ya lamborghini nisingeshawishika asee,.
 
Hao wapo nchi nzima na si matapeli wana usajili wao wako hapo kihalali kufanya mnada wao. Tz wanapenda vya bure kwa bei Chee! Sasa hao wanachofanya ni kuuza bidhaa za low quality kama Ni t-shirt Ni zile za kchovya vitenge unaambiwa ni wax lkn Ni teleza ya Kenya au laknan zawadi Ni wanazotoa kweli ni pipi tu.
Makao makuu yao Ni Arusha lkn wana matawi nchi nzima mpk vijijini na huo Ni ubinifu wa vijana acha wapige pesa.
 
Wale wanaouza mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha pale Ilala na karume ni matapeli

Unanunua kitenge unapewa begi bure na rubega 3 bure kwa elfu 5 tu Ngoja niwape taarifa mchukue tahadhari

Kwanza sipo hapa kuharibu biashara za watu. Ni hivi katika ya karume na ilala njiani pale kwenye kibao cha shule ya michikichini kunakuaga na wakaka wanauzaga nguo,mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha juu

Mtu ananunua Tisheti moja anapewa zawadi ya begi kubwa bure, Vitenge vya wax kigoma anapewa pair tatu bure, na rubega aka mkorori mbili bure hapo kanunue tishert ya 3000.....huu ni utapeli

Ngoja niwaambie wanachofanyaga Wanatafutaga kinadada ambao ni watu wao na kina kaka wanawachanganya katika ya watu kwahiyo wakiwa wanauza wanatupa ofa kama hizo wanawatupia wale wanawake wao kwamba eti ionekane kanunua kitenge kwa buku kapewa begi bure, mashuka bure na mashuka ya kimasai bure.

Wakishawarushia watu wao utaona wale wadada mmoja mmoja kwa wakati wake akijifanya anaondoka akifika huko ndani ndani anaenda kumkabidhi mtu wao maalum ambaye naye huzirudisha stoo then watazitoa kwa njia nyingine na kuzirudisha hapo mnadani.

Wanaopigwa na wapita njia ambao watavutiwa jinsi watu wanavyozawadiwa vitu basi wewe mpita njia utajiunga, watakuambia ununue tishet kwa elfu kumi then wanakwambia utulie watakupa zawadi ya bure, utaendelea kusubiria huku ukiona wenzako (wale watu wao) wakiendelea kuzawadiwa vitu kibao, wakiona una wasiwasi watakuambia nunua sasa upate mabegi mawili bure, utanunua utaambiwa mwishoni utapewa zawadi mwisho wa siku watafunga mnada na kusema usubiri wanakuja then watapotea wote mmoja mmoja.

Hao wadada na wakaka ambao ni watu fatilia kwa makini hata wakinunua wakitupiwa hizo zawadi ukiangalia kwa makini anayekusanya pesa za wanaolipa akiwasogelea wanajifanya wanatoa pesa lakini hawalipi anamsogelea masikioni na kumpa maelekezo kwamba ninini cha kufanya

Cha ajabu utakuta hao wadada wanaojichanganya na wanunuzi ni wao tu ndo hurushiwa hayo mabegi na mavitenge na zawadi halafu baadae wanarudisha kimya kimya hadi wanapoendaga kuviweka ili virudishwe mnadani napajua

Halafu hao hao wadada wanaojifanyaga wanunuz nawakutaga hapo kila siku kingine kama jioni au giza linaingia ili muuza mnada mtu wao aweze kuwatambua wadada wote hufunga vilemba, mitandio au vitambaa au kanga kichwani ili waweze kuwatambua.

Huo ni utapeli unaoendeleaga hapa ilala kwetu nimewapa taarifa mapema msanuke maana kila siku watu hulizwa hapa hubaki wakilia, yaani kila siku ni lazima nikute watu wakilia hapo na wengine wanaondokaga nyumbani na hela au kabeba hela kwa ajili ya mambo ya msingi akifika hapo anamalizia kwa hao matapeli anabaki bila hata nauli

Juzi kuna mama kalizwa kama elfu 90 hivi na alikopa Kwenye kikundi yule mama ilibidi aombe nauli, mwingine ni mtoto wa shule mpita njia aliona tishet kali akajichanganya elfu 50 aliyopewa na mzazi ikaliwa na wahuni akabaki akilia na kusaga meno.

Kuweni makini na hao matapeli wa mnada hapo njia ya kuelekea kati ya ilala na karume na huo mnada mara nyingi hufanyikia pale kilipo kibao cha shule ya michikichini Wapita njia kuweni makini
polee kwa kupigwa...sisi ndio watoto wa mjini..UTAJIITAJE MTOTO WA MJINI NA HUJAWAI KWENDA JELA?..
 
Hizo ni technics za kuwafanyia watu wa kuja kama wale wa kutoka Mwakaleli.
Nimezaliwa Manzese, kukulia Manzese, kusoma Manzese! Uniingize mjini a ujanja huo?
 
Usisahau mtoa uzi hawa jamaa wana connection na polisi na wanalipa bill kila ijumaa ndio maana kila siku wanaendelea kutapeli watu,wala hawabuguziwi .

Dawa yao ni kwenda na mshikaji wako ambaye ni mjeda depo jipya tu ,then mnaenda kukichafua hii niliina Ubungo Darajani pale,waliyakanyaga kwa mjeda wakapoteana.
Kumbe
 
Wale wapo kila mkoa na mikoa yenye mavuno huwa wanawahi kufika wanasafiri kwa upepo wa mikoa saivi wapo singida, babati, arusha na moshi wapo, wanasafiri kwa upepo. Matapeli nimewashuhudia hapa moshi juzi stand ya vumbi karibu na polisi hapa, yaani begi la 30,000 wao wanatangaza 2000 afu kaja chokoraa katoa 2000 kapewa begi afu kazunguka nyuma karudisha begi lao kwenye kile kiota chao wanawekeaga vitenge na buku mbili karudisha.

Ishu ni kwamba mpaka wanapiga hii biashara eneo la polisi kabisa, huwa wanawapa polisi pesa kuwatuliza wao polisi wanasemaga tupate maji ya kunywa ndiyo mfanye kazi. Alafu wa wanaingia kutapeli mambwiga.

sasa kisanga kilianza pale jamaa hawakutoa maji ya kunywa kwa polisi wacha jamaa wabebwe na defenda mpaka cero hii ilikuwa moshi hapo 😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom