Wale wanaosemaga China wanatupenda hawajui hawa watu vizuri

Kuna watu wanafikiri kule China tunaheahimiwa kuliko sehemu nyingine Duniani kama US . Huu sio ukweli tofauti ni kwamba kwasababu US vyombo vya habari viko wazi tunasikia matukio mengi lakini wa China ni wabaguzi mara 100 zaidi


Wode maya anafanya kazi nzuri sana kuwafichua hawa watu maana jamaa kwanza anajua kichina fluently na amaeshatembelea nchi nyingi tu ila china ndo sana hupendelea kwenda .

All ina all tumejifunza nini kama africa? Badala ya kulalamika?
 
Nashangaa watu wanajustify huu ushenzi wa wachina.

Anachokifanya huyu mama anafundisha mtoto HATRED dhidi ya mtu yeyote mweusi bila kujali kuwa mtu huyo mweusi ni mtu mzuri au la!

Tabia za kujidharau kisa tu uko frustrated kwa mambo mabaya nchini mwako ni tabia za kijinga kwa sababu adui anazitumia kukudharau zaidi maana wewe tayari ni self hating

Wachina walinyanyaswa sana na Wajapani lakini hakuna mchina anayeweza kusema kuwa "Well tulistahili kunyanyaswa kwa sababu tulikuwa wajinga wakati huo"

STOP BEING SELF HATING!
 
Wachina ni wafyonza rasilimali tu na mabeberu uchwara.
 
The only way to survive in this world, make sure una pesa. Pesa ndio itaamua heshima yako, huwezi kuwa masikini hapohapo unataka ule pamoja na wakubwa 😅😅
Ukitegemea pesa ndio upate heshima hautakuja kuheshimika kwasababu pesa ni namba zisizo na mwisho.

Ili uheshimike dhibiti NJAA na usiwe MSUKULE wa mtu yeyote.

Maisha ni kutegemeana. Ukiona mtu anakudharau mdis-connect kwenye maisha yako. Period
 
Enzi za Mao Zedong ambaye alikuwa mkomunisti na rafiki yake na mkomunisti mwenzake Nyerere, Wachina wasingethubutu kutukana weusi. Walilazimishwa mpaka kuja huku kujenga reli ya TAZARA. Siku hizi Wachina wako huru kidogo ndiyo maana unaona wanatukana na kukashifu weusi.
 
Wachina ni wabaguzi sana... Na tena wanabaguana hata wenyewe Kwa wenyewe...
 
Kubaguliwa,mbaya sana ila inategemea na wewe utaichukuliaje!
Ila ukikutana na hali kama hiyo we wachukulie kama wapumbv fulani

Ova
 
Hakuna undugu na heshima kati ya tajiri ya masikini, rafiki wa tajiri ni tajiri na rafiki wa masikini ni masikini... ukitaka uwe na urafiki na matajiri na watu wenye uelewa inakupaswa nawe uwe tajiri pamoja na uelewa..

tusilazimishe kuheshimiwa wakati hatuna kitu na hatuna msaada wowote duniani na hatufanyi lolote la maana kuendeleza mataifa yetu zaidi ya kuyabomoa kila siku....

WaAfrica tuache ujuaje tupambane kuijenga Africa kutengeneza heshima kwa vizazi vyetu vya baadaye...tukiendelea kuwa ombaomba na kujipendekeza kwa weupe tutaendelea kudharauliwa na kubaguliwa milele...
Well said! Dhambi ya kuombaomba inatutafuna, akili za viongizi wetu wa zinawaumiza waafrika
 
Back
Top Bottom