Wale waliofukuzwa na wengine kuhamishwa Tambaza Secondary 1993 mko wapi?

Nilihudhuria mechi ya Tambaza iliyofanyika Uwanja wa Taifa. Uwanja ulijaa pomoni. Nilikuwa nimevaa magwanda ya 'Kombati'. Sikuona askari yoyote mwingine uwanjani.

Mashabiki wa Tambaza walikuwa wakiimba nyimbo ambazo mashairi yake yanakinzana na T.O.S. za JamiiForums.

Timu yao ilipofungwa, walizidi kushangilia, mashairi yakiwa:

"Tutafungiwa!!!
Tutafungiwa!!!"

Niliondoka kurejea kambini kabla ya mechi kuisha. Baadae nikasikia palitukia tafrani.
 
Nashukuru baba angu hakuharibika japo nae alikuwa kweny kisanga cha kutupwa mkoani lol, alivokuwa anasimulia nkawaa nadhan utan kumbe n kweli duuuuuuh. So sad
 
nilisoma hapo miaka hiyo. Hii ilikuwa shule ya aina yake. Tulikuwa tunakula viazi maganda na mchuzi wa nyama. Halafu unakwenda summit kupiga shule. Ukitoka hapo ngoma Faya au Palm Beach unalamba Riziki kwa Mungu, Dau la Mnyonge, Simba Luwala, Kolombia,n.k. Konda akileta zake anachapwa. Walikuwepo kina Shetani, No Mbungi, DickPapa, hata Ndama Mutoto ya Ngombe maticha wetu Father K, Busianya,Haonga,Kaihula(sasa Mb Cdm), Savimbi,n.k Those old gooddays
Umenikumbusha Miaka 1985-87.Wakati huo niko F.5,PCM! Father Kalumuna(Headmaster),Mwaipopo(Physics),Kaihula(Siasa),Mama Shija(Chemistry),Mrs.Kilembe(Adv.Maths)!
Lak
 
Sisi wengine tulikuja kujiunga baada ya kufanywa kuwa Shule ya mchanganyiko na ikiwa “A” level tu yaani wavulana na wasichana ambapo zamani kabla ya huo uhamisho wa Babeli ilikuwa ya wavulana tu!

Mimi ilikuwa shule ya ndoto yangu , nilikuwa napenda wanavyovaa viatu vyeusi na soksi nyeusi ilikuwa inapendeza sana na wasichana walivyokuwa wanavaa zile skeets light grey kitambaa fulani amazing

Niliipenda sana Shule ile!
 
Tumesoma wote
 
Hakika tumesoma wote…ilikuwa ni shule ya ndoto yangu
 
Mimi kwakwel niliwaza kuja kusoma tambaza baada ya kusikia Habar zake…
 
Niliwahi ambiwa kuna Jamaa alikuwa anakuja na semi trela then daftar anazweka kule nyuma….anazfunga na Mpira kabsa
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom