Wale wa madish ya ku-band na C- band pamoja na receiver pitia hapa

DIGE

Member
Apr 29, 2019
12
44
MAWASILIANO YA SATELAITI
Satelaiti ni nini?
Ni mwezi (moon), sayari (planet) au mashine inayozunguka sayari au nyota.

Satelaiti ya kwanza kutengenezwa na binadamu, kupelekwa angani na kuwekwa katika obiti kuzunguka dunia iliitwa SPUTNIK 1.

Ilitengenezwa na Urusi na kupelekwa angani tarehe 4 Octoba, 1957. Satelaiti hii ilisafiri kwa mwendo wa kilomita 29,000(km) kwa saa ikitumia dakika 96.2 kukamilisha mzunguko wa dunia. Ikiwa angani ilituma mawimbi ya mawasiliano katika masafa ya 20.002MHz na 40.002MHz ambayo yalipokelewa na mitambo ya redio za amateur “amateur radio” duniani kote. Iliendelea kutuma mawimbi kwa siku 22 baadaye nguvu ya betri za transmita hizo ziliisha nguvu tarehe 26 Octoba, 1957.

Satelaiti hiyo ilianza kudondoka toka katika obiti angani na kuungua tarehe 4 Januari, 1958 baada ya kuingia kwenye anga ya dunia (atmosphere). Ilikaa angani kwa muda wa miezi mitatu.

Kuna satelaiti za aina ngapi?
Kuna satelaiti za aina mbili:

· Satelaiti za asili (Natural satellites) mfano; Dunia (Dunia huzunguka Jua) na Mwezi (mwezi huzunguka Dunia).

· Satelaiti za kutengenezwa na Binadamu (Artificial satellites).
1084346


SATELAITI
Kuna aina ngapi za Satelaiti za kutengenezwa na binadamu?
Zipo satelaiti za aina nyingi na zimetengwa kwa matumizi mbalimbali.

· Satelaiti kwa ajili ya utafiti na uchunguzi sayari za mbali, galaxies na vitu vingine vinavyoelea angani (Astronomical satellites).
· Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufanya mawasiliano (Communications Satellites).
· Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kuangalia hali ya hewa (Weather Satellites).
· Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya matumizi ya Ki-intelijensia na Kijeshi (Intelligence and Military Operations Satellites).

· Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufanya utafiti wa dunia na vitu vingine vilivyoko angani mfano (Biosatellites ambazo hubeba viumbe hai kwenda angani kwa ajili ya utafiti).
· Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufuatilia mabadiliko ya dunia na mazingira (Earth Observational Satellites).

· Ofisi za uchunguzi wa anga zinazoelea angani (Space Stations).
· Vifaa (mitambo) vyote vinavyokuwa angani katika obiti (Manned Spacecrafts / Spaceships).
· Satelaiti ndogo zinazounganishwa katika satelaiti nyingine kwa waya mwembamba unaoitwa tether (Tether Satellites)

· Satelaiti kwa ajili ya kutambua (mahali/ sehemu) katika uso wa dunia (positioning satellites) mfano GLONASS ni mfumo wa Urusi, GPS(Global Positioning System) ni mfumo wa Marekani, GALILEO ni mfumo wa Ulaya (European Union), China mfumo wao COMPASS kwa sasa unaitwa BeiDou, IRNSS ni mfumo wa India. Mfumo wa GNSS (Global Navigation Satellite System) huunganisha mifumo niliyoitaja hapo juu.

Satelaiti zote hapo juu zipo katika obiti (orbit) zilizopo katika umbali tofauti kutoka katika uso wa dunia. Obiti hizo ni:
LEO (Low Earth Orbit) umbali kuanzia kilomita 0 hadi 2000km juu ya uso wa dunia; baadhi ya satelaiti zilizopo katika ukanda huu ni Kituo cha Kimataifa cha Satelaiti kilichopo umbali wa kilomita mia nne (400km) kutoka katika uso wa dunia kinachoitwa ISS (International Space Station), satelaiti za uchunguzi wa dunia (earth observation satellites), satelaiti za upelelezi, Satelaiti zinazotumika katika "Remote Sensing"

KITUO CHA KIMATAIFA CHA SATELAITI (INTERNATIONAL SPACE STATION - ISS)KINACHOZUNGUKA DUNIA KATIKA UMBALI WA KILOMITA 400km (umbali kati ya 330km na 435km kutoka ardhini) KUTOKA ARDHINI.

Taarifa nyingine:
Kilirushwa angani tarehe 20 Novemba, 1998
Kinazunguka dunia. Spidi yake inafika hadi 28,800km/saa. (Leo tarehe 30 Desemba, 2017, kati ya saa 1:00 hadi saa 1:10) usiku (Muda wa Afrika Mashariki); ((19:00 to 19:10) PM GMT + 3) kimesafiri kwa spidi kati ya 27,613km/saa hadi 27,617km/saa) katika umbali wa kati ya kilomita (400)km na (406)km juu ya uso wa dunia).

DOKEZO:
Kilomita 400km na 406km ni umbali kutoka ardhini hadi kilipopita kituo hicho (Altitude). Maana yake kituo hicho kilipanda kwenda juu katika muda huo kutoka kilomita 400km hadi kilomita 406km.
Kiligharimu dola za Kimarekani Bilioni 150 (150 Billion Us Dollar).
Kilitengenezwa kwa ushirikiano wa Marekani, Urusi, Japan, Canada na baadhi ya nchi za Ulaya.
.
MEO/ICO (Medium Earth Orbit/Intermediate Circular Orbit) umbali kati ya kilomita 2000km na 35786km juu ya uso wa dunia; baadhi ya satelaiti zilizopo katika ukanda huu ni satelaiti za utambuzi wa mahali katika uso wa dunia namaanisha za GPS (kilomita 20,200km), GLONAS (19,100km), GALILEO (23,222km), satelaiti zinazotumika kutuma na kupokea mawasiliano kaskazini mwa dunia (northern pole) na kusini mwa dunia (southern pole).




1084352



MIFUMO MBALIMBALI YA SATELAITI
GEO (Geostationary Earth Orbit): Umbali wa kilomita 35,786km juu ya uso wa dunia katika Ikweta. Satelaiti zilizopo katika umbali huu huzunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia.

Mfano wa satelaiti zilizopo katika umbali huu ni zile za mawasiliano ya Televisheni, Data (intaneti), redio, mawasiliano ya simu (mfano Thuraya ambayo hutumia satelaiti mbili ambazo ni Thuraya 2 na Thuraya 3 ambazo hutumika kutoa huduma za mawasiliano ya simu za satelaiti "satellite phones" katika bara la Asia, Afrika, Ulaya na Australia ), mawasiliano ya kiintelijensia, mawasiliano ya kijeshi, satelaiti za uchunguzi wa hali ya hewa, satelaiti za kurekebisha data katika uso wa dunia (mfano OmniSTAR).

Dokezo: Satelaiti zote zilizopo katika umbali wa kilomita 35,786km juu ya uso wa dunia katika Ikweta (latitudo 0) huzunguka sawa na kasi ya dunia. Satelaiti zilizopo katika umbali huo juu ya uso wa dunia nje ya mstari wa Ikweta haziwezi kuzunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia.

HEO (High Earth Orbit): umbali zaidi ya kilomita 35,786km. Satelaiti zilizopo katika umbali huu huzunguka kwa kasi ndogo kuliko kasi ya dunia. Mfano wa satelaiti iliyoko katika ukanda huu ni VELA 1A.

Satelaiti tunazozitumia kupokea mawimbi ya televisheni / redio zipo katika kundi la Satelaiti za Mawasiliano (Communication Satellites). Satelaiti hizi za mawasiliano tunazozitumia kupitisha mawasiliano ya televisheni na redio (zipo katika Geosynchronous Orbit) umbali wa kilomita 35,786km kutoka ardhini katika Ikweta na husafiri kwa kasi sawa na kasi ya dunia.

Mawasiliano kutoka katika satelaiti za mawasiliano zilizopo katika "Geosynchronous Orbit"(GSO).
KUTAFUTA CHANELI MBALIMBALI ZA TELEVISHENI / REDIO KUTOKA KATIKA SATELAITI MBALIMBALI ZA MAWASILIANO ZILIZOPO KATIKA GEOSYNCHRONOUS ORBIT (GSO); OBITI AMBAYO KWA MAJINA MENGINE HUITWA (PARKING ORBIT au CLARKE BELT au GEOSYNCHRONOUS ARCH).

Kwa kuwa dunia ina umbo la duara si rahisi watu wote tulioopo katika uso wa dunia (namaanisha mabara yote) tukatumia satelaiti moja kupokea mawasiliano toka katika satelaiti. Kusema hivi namaanisha mfano satelaiti tunayoitumia sana (IS 906 @ 64.2E (nyuzi za longitudo 64.2 Mashariki mwa Greenwich) katika ukanda wetu Tanzania ikiwemo haiwezi kufikisha mawimbi yake Marekani kwa sababu Marekani wanakuwa upande mwingine wa uso wa dunia (they are below the horizon of the reach of this satellite) hii ni vile vile kwa satelaiti zinazoimulika Marekani hata sisi hatuwezi kupata mawimbi yake.

Mfano baadhi ya satelaiti za Intelsat (IS 902, IS 906, IS 904, IS 10, IS 17, IS 907 na nyinginezo zilizoko juu ya usawa wa Afrika na bahari ya Hindi na wao wakitaka kupokea mawasiliano yake wanatumia kituo chao kilichopo Afrika Kusini au vituo vingine.

Baadhi ya satelaiti ambazo nilishazifanyia utafiti na mawimbi yake yanafika hapa Tanzania zipo kati ya nyuzi za longitudo 27 Magharibi mwa Mstari wa Greenwich na nyuzi za longitudo 85 Mashariki mwa Mstari wa Greenwich. Dishi linalozunguka (horizon to horizon) linaweza kupata chaneli mbalimbali kutoka satelaiti hizi kwa kuzunguka kupitia satelaiti moja baada ya nyingine (from 27 West to 85 East). Kadri unavyoelekea Magharibi ya dunia ndivyo utakavyozidi kupata satelaiti zilizopo Magharibi ya dunia huku ukipoteza za Mashariki ya dunia; na kinyume chake (and vice versa).

Baadhi ya satelaiti ambazo zinazunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia; ambazo zipo katika "Geosynchronous Orbit or Parking Orbit" zinazopatikana katika eneo letu (Tanzania na nchi za jirani zimeorodheshwa chini. Satelaiti hizi hutumika kwa mawasiliano mbalimbali mfano Data /Internet, Televisheni, Radio, Mawasiliano ya Ki-intelijensia, kijeshi na mawasiliano mengine.

Intelsat 907 @ 27.5W: VoA TV, Alhurra TV Iraq, Alhurra TV Europe, RTG (Guinea),
Intelsat 905 @ 24.5W: Nile Drama, Syria 1,
SES 4 @ 22W: Bolivia Mux, Truth TV, TV Universal,
NSS7 @ 20W: CNN, TBN, Emmanuel TV, MBC (Malawi), Lesotho TV, TPA, Trinity Broadcasting
Intelsat 901 @ 18W: Ethiopia Educational Media Agency
Telstar 12 @ 15W:

Nilesat 201 @ 7W: DW Arabia, BBC Arabic, Abu Dhabi, Abu Dhabi Sport 1, Dubai Sport 2, DM, TV, National Geographic Channel,
Intelsat 10 - 10W @ 1W: BBC World Service, RTS1 (Senegal)
Rascom QAF 1R @ 2.8E: Libya Satellite TV, Libyan Mux, RTNC, Digital Congo (Congo)
SES 5 @ 5E: ZUKU, SABC 1, SABC 2, SABC 3, ETV, STARTIMES

Eutelsat 7A @ 7E: Record Mozambique, MBC 1, MBC 2, CRTV, RTS 1 (Senegal), BBC Persian, ORTM, Raha Tv, TPA Internacional, VoA TV Persian, Azam TV,
Eutelsat 10A @ 10E: Startimes, Agape TV Network,
Amos 5 @ 17E: Zambia Mux, Reuters Live, Doordarshan, Kingdom Africa TV, Bible Exploration TV, Fashion TV Europe, TING (Tanzania), Continental, (Amos 5@ 17E ilipoteza mawasiliano na ardhini (duniani) tarehe 22/11/2015).

Eutelsat 36A @ 36E: TING Channels (Tanzania), NTV Plus, Afrique TV,
Eutelsat 36B @ 36E: CCTV News, CCTV 4 Europe, Multichoice DStv channels
NSS 12 @ 57E: ZUKU, KBC- Kenya, Family TV - Kenya, ETV (Ethiopia), VoA TV Africa, American Embassy tv Network etc.),

Intelsat 904 @ 60E: Uganda Mux, Kenya Mux, NTV (Kenya), KBC Channel 1 (Kenya), TBC 1, NTV, Uganda (Kenya), Swazi TV, ZNBC,
Intelsat 902 @ 62E: NTV (Kenya), Citizen TV (Kenya), SABC 1 - 3 (South Africa), Sky International,
Intelsat 906 @ 64.2E: ITV, EATV, CAPITAL, TBC, STARTV, TVM (Mozambique), UBC (Uganda), Chanel 10,

1084353


Picha hapo juu ni Intelsat 906 @ 64.2E inakofikisha Mawimbi yake katika masafa ya C Band (Hemi, Zonal & Global Beams)
Intelsat 17 @ 66E: HMTV, Captain TV, ABN (India), V6 News, DStv, Bunge la Jamhuri ya Tanzania

Picha chini ni sehemu duniani ambapo mawasiliano ya satelaiti hii (IS 17) yanafika.

1084356

Picha hapo juu ni sehemu mawasiliano ya satelaiti hiyo yanapofika katika masafa ya C Band (C Band Landmass Coverage)
1084357

Picha hapo juu ni sehemu mawasiliano ya satelaiti hiyo yanapofika katika masafa ya Ku Band (African Ku Band Beam); (Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawasiliano yao yapo katika "beam" hii).
1084359


Picha hapo juu ni sehemu mawasiliano ya satelaiti hiyo yanapofika katika masafa ya C Band (C Band Western Hemisphere Coverage).
1084360


Picha hapo juu ni sehemu mawasiliano ya satelaiti hiyo yanapofika katika masafa ya C Band (Global C Band Coverage).

1084368


Picha hapo juu ni sehemu mawasiliano ya satelaiti hiyo yanapofika katika masafa ya Ku Band (Europe and Middle East Ku Band Coverage)

1084371



Picha hapo juu ni sehemu mawasiliano ya satelaiti hiyo yanapofika katika masafa ya Ku Band (Russian Ku Band Coverage).

Intelsat 20 @ 68.5E: Indiasign, NHK World TV (Japan), Peace TV Bangla, India TV, South Korea Mux, CTS (South Korea), Hope TV India, YTN World, VTV (India), Peace TV, God TV Africa, Africa Unite TV, ABN (Nigeria), Messiah TV, Citizen TV (Kenya), UB (South Africa), Emmanuel TV, CTV, 3ABN International, Press TV, CCTV, EWTN, DStv South Africa,

Eutelsat 70B: Canadian Forces Radio & TV,

Intelsat 22@72.1: Family TV (Kenya), KBC Channel 1, Citzen TV, GBS

ABS 2 @ 75E:

Apstar 7 @ 76.5E: ERT World, Channel 9 (Bangladesh), God Asia,

Thaicom 5 @ 78.5E: Somalia National TV, TV5 Cambodia, T Sports Channel, Shop Thailand, Spring TV News, MRTV, na nyinginezo.

Thaicom 6@78.5E:

Express MD1 @ 80E:

Dishi linaloweza kufanya kazi hii vizuri katika C Band ni la kipenyo kuanzia futi sita 6ft, 8ft, 10ft, 12ft na kuendelea (hasa kuanzia futi kumi 10ft na kuendelea kutegemea na nguvu ya mawimbi unayoyapokea.).
Kwa madishi ambayo hayazunguki (fixed satellite dishes) inabidi ufunge madishi mengi kila dishi liwasiliane na satelaiti yake. Ndio maana ukienda katika vituo vya televisheni/ redio mfano ITV, Startimes na vingine unakuta madishi mengi ya kupokea mawasiliano (chaneli) mbalimbail kutoka katika satelaiti tofauti tofauti.

Masafa ya Mawimbi ya Televisheni / Redio kwenda (uplink frequencies) katika satelaiti katika eneo letu ITU Region 1 (Afrika, Ulaya, Uarabuni na Urusi).

Masafa yanayotumika kupeleka mawimbi katika satelaiti toka vituo vya Televisheni/Redio vinavyotumia Ku Band katika ukanda wetu (ITU Region 1) ni kati ya 14.0GHz - 14.5GHz.

Masafa yanayotumika kupeleka mawimbi katika satelaiti toka vituo vya Televisheni/Redio vinavyotumia C Band katika ukanda wetu (ITU Region 1) ni kati ya 5.850GHz - 6.425GHz.

Masafa ya Mawimbi ya Televisheni / Redio toka katika satelaiti (downlink frequencies) katika eneo letu ITU Region 1 (Afrika, Ulaya, Uarabuni na Urusi)

Mawasiliano ya Televisheni na Redio tunazozipokea toka katika satelaiti yapo katika "Electromagnetic Spectrum" kati ya 3GHz - 30GHz.

Kwa C Band masafa yanayotumika kutuma mawasiliano toka katika satelaiti hadi kwenye madishi tunayoyatumia ni 3.7GHz - 4.2GHz.

Kwa Ku Band masafa yanayotumika kutuma mawasiliano toka katika satelaiti hadi kwenye madishi tunayoyatumia ni 10.7GHz hadi 12.75GHz.

a) CHANELI ZA MULTICHOICE/ DSTV
Kutafuta chaneli za Multichoice/ Dstv kutoka katika satelaiti Eutelsat 36B iliyopo nyuzi za longitudo 35.9 (Mashariki mwa Mstari wa Greenwich) wanayoitumia kutupatia chaneli zao. Hii ni kwa sehemu ambazo satelaiti hii inafikisha mawimbi yake Tanzaniaikiwa mojawapo.

Eutelsat 36B iliyopo nyuzi za longitudo 35.9 Mashariki mwa mstari wa Greenwich.

Satelaiti hii iko wapi?

Satelaiti hii ipo katika nyuzi za longitudo 35.9°E Mashariki mwa Mstari wa Greenwich.

Ni satelaiti inayomilikiwa na kampuni ya Eutelsat; ilitengenezwa na Kampuni inayoitwa Thales Alenia Space iliyopo katika bara la Ulaya (ina ofisi Ufaransa, Italia, Ubelgiji, Hispania na Califonia - Marekani). Ilipelekwa angani na kuwekwa katika obiti 36,485.7km toka ardhini (ipo katika nyuzi za longitudo 35.9°E) juu ya Ikweta tarehe 24/11/2009 na kifaa kinachoitwa Proton Rocket. Muda wake wa kutumika ikiwa angani ni miaka kumi na tano (miaka 15) maana yake mwaka 2009 + miaka 15 = mwaka 2024.

Kwa hiyo muda wa kuitumia satelaiti hii ni hadi mwaka 2024. Eutelsat 36B imeambatanishwa na Eutelsat 36A ambayo ipo katika nyuzi za longitudo 36 Mashariki mwa mstari wa Greenwich (zilivyowekwa ni kama satelaiti moja.). Ikiwa katika obiti yake inafikisha mawimbi yake Afrika, Ulaya, Urusi, Maeneo ya Uarabuni na katikati ya bara la Asia.

Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Sub Saharan Beam"


1084372


Picha hapo juu inaonesha maeneo ambayo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake; pembeni ni kiwango cha mawimbi "signal power" toka katika satelaiti (nguvu ya mawimbi haiko sawa kwa maeneo yote ambayo satelaiti hii inafikisha mawimbi yake. Sehemu nyingine mawimbi yana nguvu sana na sehemu nyingine nguvu ya mawimbi ni ya kawaida.

Eneo katika bara la Ulaya ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Central European Beam"

1084373


Eutelsat 36B Central European Beam
Eneo katika bara la Asia na Ulaya ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Eutelsat 36B Eurasia beam"


1084377


Eutelsat 36B Eurasia beam

Eneo katika Urusi ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Eutelsat 36B Russia beam"

1084378


Eutelsat 36B Russia beam

Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Eutelsat 36B Southern Africa beam"


1084379


Eutelsat 36B Southern Africa beam

Vifaa muhimu vinavyohitajika wakati wa kutafuta chaneli kutoka katika satelaiti yoyote:

Spectrum Analyzer inayoweza kuonyesha mawimbi (electromagnetic radiations) hadi 15GHz, 20GHz au 30GHz (IF Range 950MHz to 2150MHz). Spectrum analyzer huonesha picha ya mawimbi, masafa yake, nguvu iliyoko katika mawimbi na hata kama mawimbi yanaingiliana yanaonekana. Kwa ufupi Spectrum Analyzer huonesha kila kitu (picha kamili ya mawimbi katika masafa mbalimbali).

Mitambo hapo juu inaitwa Spectrum Analyzer. Vifaa hivi hutusaidia kuona, kusikia, kupima na kuchunguza tabia za mawimbi katika "Electromagnetic Spectrum". Zipo Spectrum Analyzer za uwezo tofauti wa kuona mawimbi tokea 20Hz hadi 3GHz, 10GHz, 26GHz, 67GHz na kuendelea.

Field Strength meter (huonesha nguvu ya mawimbi husika).

Satellite Finder (zipo za digitali na analojia) baadhi ya mita za analojia hutoa mlio fulani ambao wakati unatafuta signal mlio huo huongezeka kadri mawimbi ya masafa unayoyatafuta yanavyoongezeka. Satellite Finder za digitali baadhi huonesha mawimbi kidijitali na nyingine huonesha mawimbi na picha. Satellite Finder za analojia hufungwa kati ya (LNB/ LNC (Low Noise Block) / Low Noise Converter respectively) na risiva/king'amuzi na za dijitali hufungwa moja kwa moja katika LNB/LNC.

Compass kwa ajili ya kuonesha uelekeo wa dishi (kuzungusha dishi kuelekea magharibi, kaskazini mashariki, kaskazini magharibi, mashariki, kusini mashariki, kaskazini mashariki, kusini, kaskazini, kutegemea sehemu ulipo duniani kutoka satelaiti unayoitafuta. Kwa lugha ya kitaalamu "Azimuth Angle". Dishi lazima lielekezwe satelaiti ilipo.

Mfano kama satelaiti ni Intelsat 906 (nyuzi 64) dishi linaelekea Kaskazini Mashariki (tukiwa Dar es Salaam) kwa sababu satelaiti hiyo ipo juu ya bahari ya Hindi jirani na maeneo ya India. Kwa maeneo mengine dishi linaweza kuelekea uelekeo tofauti kwa sababu inategemea anayefunga dishi alipo katika uso wa dunia kutoka katika satelaiti hiyo.

Inclinometer kwa ajili ya kupima ulalo au mwinuko wa dishi "elevation angle" (mzunguko wa dishi juu na chini).

Pimamaji (Spirit Level): Pimamaji ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba dishi linakaa katika msawazo; na kama unafunga katika bomba hakikisha bomba linasimama wima (upright) nyuzi 90).

TV ndogo kwa ajili ya kuonesha picha (kama unatumia Satellite Finder, King'amuzi au Risiva ya kawaida).

Vifaa vinginevyo (toolbox).

Angalizo:
Kama huna Spectrum Analyzer unaweza kutumia Field Strength Meter (Signal Strength Meter) kama huna vyote hapo unaweza kutumia Satellite Finder pamoja na King'amuzi au satelaiti risiva ya aina yoyote.

Kutafuta chaneli za Multichoice/Dstv.
Wakati wa kutafuta chaneli (signal) za Multichoice/ Dstv mafundi wengi hutumia ving'amuzi vya Multichoice/Dstv.

Ukifika site bila King'amuzi cha Dstv ufanyeje?

Wazo mbadala:
Unaweza kutumia satelaiti risiva yoyote; wakati wa kutafuta chaneli chagua satelaiti yoyote ambayo imesetiwa (satelite setup) katika Masafa ya LNB: Low Frequency 9750MHz na High Frequency 10700MHz. Haya ni masafa yanayotengenezwa na sakiti inayoitwa "local oscillator" iliyopo katika king'amuzi au risiva.

Kabla ya yote tuone hatua muhimu ambayo hufanyika katika LNB:

LNB ni nini?
Kirefu cha LNB ni "Low Noise Block".
Ni kifaa kinachofungwa katikati ya dishi (at the focus of the dish) kwa madishi yanayoitwa Prime Focus Dishes (Madishi ya C Band; madishi ya futi sita na kuendelea) na pembeni mwa dishi kwa madishi ya Ku Band (Offset dishes; madishi ya sentimita 60 na kuendelea). Kazi yake kubwa ni kupokea mawimbi kutoka katika satelaiti, kuyaongeza nguvu, kuyapunguza masafa (downconvert), na kisha kuyapeleka katika king'amuzi au risiva ambayo huyatengeza na kutoa RF (Radio Frequency), Video Baseband (Video Signal) na Sauti (Audio). Mawimbi yaliyopatikana katika king'amuzi au risiva yakiunganishwa katika televisheni tunapata picha na sauti.

Katika Ku Band masafa televisheni na redio yanayofika katika dishi ni kuanzia 10.6GHz au 10.7GHz hadi 12.75GHz.

Aina za LNB.
Zipo LNB za aina nyingi. Baadhi ya LNB zinazotumika katika mawasiliano ya televisheni kwa kuzitofautisha kutokana na Masafa.
1. LNB za Ku Band na
2. LNB za C Band.
3. LNB za Ka Band

a) LNB za Ku Band (LNB zilizoandikwa 10.7GHz hadi 12.75GHz); baadhi ya LNB za Ku Band
zimeandikwa 10.6GHz hadi 12.75GHz. Ni LNB zinazofanya kazi ya kupokea mawimbi ya
Televisheni / Redio kutoka katika satelaiti kuanzia 10.6GHz /10.7GHz hadi 12.75GHz.
Kuna aina mbalimbali za LNB za Ku Band baadhi yake ni LNB zinazotoa "output moja",
"output mbili", "output nne", "output nane", Quatro na nyinginezo. LNB za Quatro haziwezi kuunganishwa
moja kwa moja katika king'amuzi au risiva; inabidi ziunganishwe katika vifaa hivyo kupitia vifaa
vinavyoitwa "multiswitch"

Madishi yanayotumika kupokea masafa katika Ku Band (kwa madishi makubwa zaidi ya aina hii (offset ku band) mfano kuanzia 180cm unaweza kufunga LNB ya C Band





1084385


Picha hapo juu inaonesha dishi la kupokea mawasiliano ya televisheni katika Ku Band. Yapo madishi ya ukubwa tofauti kuanzia kipenyo cha sentimita 30, 45, 60, 90, 120,180 na kuendelea. Katika ukanda wetu (Tanzania na nchi za jirani) tunatumia zaidi madishi ya sentimita 90cm.

Ni vizuri zaidi kutumia Madishi ya kipenyo cha sentimita 120cm kwa sababu mawimbi katika masafa ya Ku Band huathiriwa sana na mvua (hunyonywa na matone ya mvua) na kusababisha picha kukatikakatika wakati na wakati mwingine picha kupotea kabisa wakati mvua zinaponyesha.
LNB za Ku Band

1084389

LNB ya Ku Band ya njia moja (Single output Ku Band LNB)

1084392

LNB ya Ku Band ya njia nane (Eight output octo LNB). Kila njia "Output" inajitegemea.

b) LNB za C Band:
Ni LNB zinazofanya kazi ya kupokea mawimbi ya Televisheni / Redio kutoka katika
satelaiti kuanzia 3.6GHz hadi 4.2GHz. Zipo za aina nyingi mfano
1. Single Solution C Band LNB. Hii ni LNB yenye output moja lakini inauwezo wa kugawa
mawimbi (satellite signal kwa zaidi ya risiva moja).
2. LNB za output moja, output mbili, output nne na kuendelea.
ITAENDELEA.....................................


 

Attachments

  • ddddddddddddddddddddjjjjj.jpg
    ddddddddddddddddddddjjjjj.jpg
    17.9 KB · Views: 131
  • duniaaaaa.jpg
    duniaaaaa.jpg
    12.4 KB · Views: 106
  • kifaa 1.gif
    kifaa 1.gif
    10.3 KB · Views: 125
Inaendelea sehemu ya pili ya ufafanuzi
LNB ya C Band inayotoa njia mbili (2 output LNB)

Kwa kawaida mawimbi yanayotoka katika satelaiti yana masafa makubwa sana kiasi kwamba ni shida kupita katika waya ( kadri masafa yanavyoongezeka ndivyo inavyozidi kuwa rahisi kwa mawimbi kupotea katika waya) hivyo lazima masafa hayo yapunguzwe ndio yaweze kupita katika waya.

LNB ya Ku Band (10.6GHz / 10.7 hadi 12.75GHz) hufanya kazi sawa na LNB za C Band tofauti yake ni kwamba LNB za Ku Band zinafanya kazi katika masafa makubwa ukilinganisha na LNB za C Band (3.6GHz hadi 4.2GHz).


Jambo muhimu sana la kuzingatiwa.
Mawimbi yanayotumwa katika satelaiti na kupokelewa na madishi majumbani na maofisini mwetu huwa yana namna yanavyokaa. Kuna yanayokuja katika mfumo wa koili (coil) na yanayokuja katika mstari myoofu ambayo yanakuja wima (Vertically Polarized) na mengine yanakuja yakiwa yamelala (Horizontally Polarized)

Mawimbi yanayokuja mfumo wa koili:

Yanakuja katika coil za aina mbili tofauti ambazo ni:
a) Right Circular na
b) Left Circular.

Hii inamaana vituo vya televisheni /radio hutuma katika satelaiti mawimbi ambayo husafiri katika mfumo wa:
a) Left Circular Polarized
b) Right Circular Polarized
c) Horizontal
d) Vertical

Mfano:
Tuchukue mfano wa chaneli za C Band ambazo tunazipata kutoka katika satelaiti inayoitwa IS 906 iliyopo nyuzi za longitudo 64.2 Mashariki mwa mstari wa Greenwich ambayo tunaitumia sana hapa kupokea mawasiliano ya televisheni na redio ya vituo vilivyoko hapa kwetu ambavyo ni:
Chaneli 10, TBC, Startv, ITV, Capital, EATV, TVM (Mozambique), na nyinginezo.

ITV, CAPITAL na EATV mawimbi yao yanabebwa na Frequency Moja (3641MHz) na yanakuja katika mfumo wa koili (coil) katika kundi la "Right Circular - R" na TBC (3891MHz), Startv (3884MHz) mawimbi yao ni "Left Circular (L)"

LNB hupokea mawimbi yote (Left Circular Polarized, Right Circular Polarized, Vertical Polarized na Horizontal Polarized) ila hufanyia kazi mawimbi ya aina mbili tu ambayo ni Vertical Polarized na Horizontal Polarized.


Kuna kifaa (kinafanana na kipande cha sabuni) mbacho wakati wa kufunga dishi lazima ukichomeke ndani ya LNB (ndani ya feedhorn) kwa kukatiza katikakati ya antena mbili zilizoko katika LNB ya C Band au unakichomeka kilale sambamba na antena mbili zilizoko katika LNB (antena moja ni kwa vertically polarized waves na nyingine ni kwa horizontally polarized waves). Kifaa hiki kinaitwa "Teflon Slab"

"Teflon Slab" hubadilisha mawimbi yanapokatiza katika feedhorn; Right Circular polarized waves hubadilishwa kuwa "Vertical" na Left Circular polarized waves hubadilishwa kuwa "Horizontal".

Kwa mawimbi ambayo ni "linear" (Vertical na Horizontal) hakuna haja ya kuweka Teflon Slab katika LNB.
Mfano chaneli za Asia tunazozipata toka satelaiti IS 10 iliyopo nyuzi za longitudo 68.6 Mashariki mwa mstari wa Greenwich haziitaji kuweka Teflon Slab katika LNB yake.
Mawimbi ya ITV, CAPITAL, EATV ambayo ni Right Circular hubadilishwa na Teflon Slab kuwa Vertical na Mawimbi ya TBC, Startv, ambayo ni Left Circular hubadilishwa na kuwa Horizontal.

Nini sababu kubwa ya kutuma mawimbi katika njia tofauti tofauti? Namaanisha kwa nini Left Circular, Right Circular, Vertical na Horizontal?

Sababu kubwa ya kufanya hivi ni "Frequency Reuse" mawimbi ya masafa katika frequency moja mfano 3642MHz - Right Circular ni tofauti na 3642MHz - Left Circular hivyo frequency moja inaweza kutumika zaidi ya mara moja bila kuingiliana kwa kutenganishwa na "Polarity".

Vertical na Horizontal
Katika LNB kuna antena mbili; moja kwa ajili ya kuyapokea mawimbi ya vertical na nyingine kwa ajili ya mawimbi ya horizontal. Antena ya Vertical hupokea mawimbi ambayo ni Vertical na kuyapeleka katika sakiti ya Vertical na Antena ya Horizontal hupokea mawimbi ambayo ni Horizontal na kuyaeleka katika sakiti ya Horizantal.
Sakiti ya Horizontal hutumia umeme wa Voti 18V na sakiti ya Vertical hutumia Voti 13V. Umeme huu hutoka katika risiva. Kwa hiyo waya unaounganisha risiva na LNB hupeleka umeme wa voti 13V kwa sakiti ya vertical na voti 18V kwa sakiti ya Horizontal na vilevile hubeba mawimbi (Intermediate Frequency) kutoka katika LNB kwenda katika risiva.

Unapochukua rimoti ya risiva ya satelaiti na kuweka chaneli mfano; CAPITAL televisheni risiva hupeleka voti 13V katika LNB kwa sababu Capital Televisheni mawimbi yake ni Right Circular ambayo hubadilishwa na Teflon Slab kuwa Vertical. Ukichukua rimoti na kuweka chaneli ya Startv (Left Circular ambayo hubadilishwa na kuwa Horizontal) risiva hupeleka voti 18V katika LNB.

Kwa wanaounganisha risiva zaidi ya moja:
Kama tulivyoona hapo juu Vertical ni Voti 13V na Horizontal ni Voti 18V. Ukiunga risiva zaidi ya moja na kutumia LNB ambazo si "Single Solution" (LNB zenye uwezo wa kugawa mawimbi na kuyasambaza kwa risiva mbalimbali) kuna wakati baadhi ya chaneli zitagoma kuonekana.

Kwa nini baadhi ya chaneli zitagoma kuonekana?
Hii ni kwasababu katika risiva ya kwanza mtu akichagua EATV (Right Circular - Vertical = 13V) risiva yake itapeleka Voti 13V katika LNB, na mwingine akichagua TBC (Left Circular - Horizontal = 18V) risiva yake itapeleka Voti 18V katika LNB hiyohiyo. Hii huichanganya LNB na wakati mwingine risiva.
Ukitaka kuunganisha risiva zaidi ya moja hakikisha unatumia LNB ya output mbili, au zaidi ambazo output zake kila moja inajitegemea au tumia "Single Solution LNB" kwa C Band. Kwa Ku Band hutakiwa kutumia LNB ambayo ina output zaidi ya moja (kila output inajitegemea) au Quatro LNB.

Kinachofanyika katika LNB ya Ku Band.
Ndani ya LNB kuna antena mbili ndongo ambazo hupokea mawimbi ya satelaiti na kuyapeleka katika sakiti ambayo huyakuza (amplify) na kuyaelekeza katika hatua nyinginezo. Baada ya kuyakuza hupelekwa katika sakiti ambayo hutengeneza mawimbi karibia sawa na yale yaliyotoka katika satelaiti; sakiti hiyo tunaiita "local oscillator". Mawimbi yaliyotoka katika satelaiti katika Ku Band 10700MHz - 12750MHz huchanganywa na mawimbi yaliyotengenezwa na "LNB Local oscillator" ambayo ni Low Frequency 9750MHz na High Frequency 10700MHz.

Intermediate Frequency (IF):
LNB hufanya hesabu (computes) ya kuchukua mawimbi yaliyotoka katika satelaiti na kutoa yale iliyotengeneza yenyewe katika hatua tunayoiita "Heterodyning". Hata TV, Radio risiva nazo hufanya hatua hizi wakati wa kuandaa picha na sauti. Baada ya hesabu hiyo kinachopatikana ni Intermediate Frequency (IF).

Hesabu yenyewe:

Mawimbi yaliyotoka katika satelaiti katika Ku Band 10700MHz - 12750MHz.
Mawimbi yaliyotengenezwa na LNB ya Ku Band - 9750MHz - 10700MHz.
Intermediate Frequency (IF) = 950MHz - 2050MHz

Kwa baadhi ya LNB za Ku Band:
Mawimbi yaliyotoka katika satelaiti katika Ku Band 10700MHz - 12750MHz.
Mawimbi yaliyotengenezwa na LNB ya Ku Band - 9750MHz - 10600MHz.
Intermediate Frequency (IF) = 950MHz - 2150MHz



Hii inamaanisha kwamba mawimbi yanayopita katika waya kutoka kwenye LNB ya Ku Band kwenda katika risiva ni kati ya 950MHz hadi 2050MHz au 950MHz - 2150MHz. Mawimbi haya yanaweza kupita katika waya na ukitumia "spectrum analyzer" inayoweza kuona hadi 15GHz , 20GHz au 30GHz unaweza kuyaona na kuyachunguza.

ANGALIZO:
Intermediate Frequency (IF) kwa C Band inapatikana kwa hesabu ifuatayo:

C Band:
C-Band: IF frequency = local oscillator frequency - received frequency

Local Frequency ya C Band ni 5150MHz.

Mpangilio wa Masafa tunayoyatumia kupata chaneli za televisheni/ radio katika Ku Band kwa undani zaidi.


Umeme unaokwenda katika LNB toka katika Risiva
Sauti ya kuiamsha LNB (Tone)
LO (Low Frequency) Masafa ya chini katika LNB
Ukaaji wa Mawimbi (Polarization)
Masafa yanayopokelewa
IF (Intermediate Frequency)
13 V0 kHz9.75 GHzVerticalLow Band (10.70-11.70 GHz)950-1950 MHz
18 V0 kHz9.75 GHzHorizontalLow Band (10.70-11.70 GHz)950-1950 MHz
13 V22 kHz10.60 GHzVerticalHigh Band (11.70-12.75 GHz)1100-2150 MHz
18 V22 kHz10.60 GHzHorizontalHigh Band (11.70-12.75 GHz)1100-2150 MHz


Baadhi za LNB za Ku Band hufanyakazi kuanzia 10.7GHz hadi 12.75GHz na nyingine hufanya kazi kuanzia 10.6GHz hadi 12.75GHz. Katika satelaiti hii Eutelsat 36B Multichoice / DStv wapo wanatumia High Band (masafa wanayotumia yanaanzia 11.7270GHz – 12.245GHz).

Angalia jedwali hapo juu:
Vertical High Band 11.70GHz – 12.75GHz
Horizontal High Band 11.70GHz – 12.75GHz


Jambo muhimu:
Kadri masafa yanavyoongezeka ndivyo mawimbi yanavyokuwa rahisi kupotea katika waya. Katika masafa makubwa tunahitaji kutumia waya bora; vinginevyo mawimbi yanayofika katika risiva au decoder yanakuwa madogo (mawimbi hupotea njiani). Kwa lugha ya kitaalam tunasema "signal attenuation along cables". Waya tunaotumia kusafirisha mawimbi toka katika antena kwenda katika decoder za; mfano Startimes, Ting, Easy TV, au antenna zinazoungwa moja kwa moja katika televisheni zinaweza kushindwa kupitisha vizuri mawimbi kutoka katika LNB ya dishi kwenda katika risiva au decoder kama wavu wa waya unaouzunguka waya wa katikati wa"COAXIAL CABLE" hauna waya nyingi (if the coaxial cable shielding is not well brided).


Ku Band ipo ndani ya "Electromagnetic Spectrum - 3GHz hadi 30GHz" katika masafa ya 10.7GHz (10700MHz) hadi 12.75GHz (12750MHz) kutoka katika satelaiti (Ku band Television downlink frequencies).

Au setup mwenyewe kwa kubadilisha (edit katika risiva); LNB Frequencies za C Band ambazo ni 5150MHz na kuweka za Ku Band kama inavyoonekana hapa chini.

Satellite setup (katika risiva):
LNB Frequency
Low Frequency: 9750MHz
High Frequency: 10700MHz

Katika channel search (kila risiva ina MENU yake tofauti na nyingine):
Ingiza masafa (frequency), Symbol Rate na polarization (polarization weka Auto) katika jedwali ifuatayo (chagua mojawapo). Anza kutafuta signal. Ukishapata unganisha kila kitu sawa (weka waya vizuri) alafu unganisha decoder ya Multichoice/Dstv; utapata picha.

Mfano:

Ingiza katika risiva au decoder:

Frequency : 11785
Symbol Rate: 27500
Polarization: Horizontal
FEC (Forward Error Correction): ¾ au Auto
Mambo ya kuzingatia wakati wa kutafuta chaneli za Multichoice / DStv yanayotoka katika satelaiti Eutelsat 36B.

Baada ya kutafiti sana mawimbi ya satelaiti hii yanaonekana kuwa imara (stable) kwa frequency zote ila kuna tatizo linalojitokeza ni upande wa dishi.

Tatizo lenyewe:
Kutokana na sababu za kijiografia sisi (Tanzania) tupo jirani na satelaiti hii (inakuwa kama ipo utosini). Madishi yanayotumika kwa wingi kupokea chaneli za Multichoice/ DStv ni ya kipenyo cha sentimita 90(cm). Mara nyingi wakati wa mvua kwa wanaotumia madishi ya ukubwa huu lazima mawimbi yakatikekatike. Kwa sababu kadri masafa yanavyozidi kuongezeka katika "electromagnetic spectrum" unavyozidi kwenda juu; ("SOMA ELECTROMAGNETIC SPECTRUM") ndivyo yanavyozidi kuathiriwa na mvua. Ili kupata mawimbi ambayo hayakatiki hata wakati wa mvua tunahitaji kutumia madishi ya ukubwa wa sentimita 120(cm) ambayo ni sawa na mita 1.2(m).
Madishi mengi ya Ku Band yaliyopo sokoni (satellite dishes on the market) yanasumbua wakati wa kutafuta satelaiti hiyo kwasababu hayazunguki sana (vertical movement). Yanaishia pale satelaiti ilipo hivyo inakuwa vigumu kurekebisha vizuri ilikupata mawimbi vizuri. Pia stand zake (dish bases) zinazokuja na madishi hayo ni fupi kiasi kwamba ukizifunga ukutani madishi yanagusa ukutani. Hili ni tatizo lililopo katika utengenezaji wa madishi ya Ku Band na Multichoice/ Dstv inabidi tatizo hili walitazame kwasababu linawahusu.

Uwekaji wa LNB.
Kitu muhimu cha kuangalia wakati wa kufunga dishi ni namna ya kuweka LNB (Ulalo wa LNB) ukiiweka vibaya inaweza ikakataa kutoa signal hata kama dishi limekaa vizuri (hii ni kwa dishi la Ku Band na C Band), kwa sababu katika LNB kuna antenna (probe) mbili ambazo moja kwa ajili ya chaneli ambazo ni “vertical” na nyingine kwa ajili ya chaneli ambazo ni “horizontal”. Katika kanuni za kurusha mawimbi lazima antenna inayorusha iwe imekaa sawa na antenna inayopokea.
Hii inamaanisha kwamba kama antenna iliyopo katika “transponder” ya satelaiti imesimama (vertical) na LNB ya dishi linalopokea mawasiliano hayo lazima antenna yake nayo iwe vertical. Vilevile kwa chaneli za Horizontal. Hatua ya kurekebisha LNB ili antenna yake ikae sawa na mawimbi inayoyapokea huitwa “LNB Skew Adjustment”.

Kufunga LNB ya Ku Band katika dish la C Band.
LNB ya Ku Band ukiifunga katika dishi la C Band inaweza kufanya kazi ikiwa dishi hilolinaelekea katika satelaiti yenye chaneli unazozitafuta. Katika hili ni muhimu kuangalia unapofunga LNB ya Ku Band katika dishi la C Band. Mawimbi yakiwa na nguvu sanayanaweza kuiharibu LNB.

Jedwali lililoko hapo chini linaonesha Masafa na Channel za Multichoice/ Dstv tunazozipokea nchini Tanzania na nchi nyingine ambazo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake.
Haya masafa huwasaidia mafundi wakati wa kufunga madishi (kutafuta signal za Dstv).

Masafa ya chaneli za Multichoice /DStv toka katika satelaiti Eutelsat 36B.

Masafa katika Megahertz (MHz)
Symbol Rate
Polarization
FEC (Forward Error Correction)
1172727500Vertical (V)¾ (au Auto)
1174727500Horizontal¾ (au Auto)
1176627500Vertical¾ (au Auto)
1178527500Horizontal¾ (au Auto)
1180427500Vertical¾ (au Auto)
1182327500Horizontal¾ (au Auto)
1184327500Vertical¾ (au Auto)
1186227500Horizontal¾ (au Auto)
1188127500Vertical¾ (au Auto)
1190026480Horizontal¾ (au Auto)
1191927500Vertical¾ (au Auto)
1194027500Horizontal¾ (au Auto)
1195827500Vertical¾ (au Auto)
1197727500Horizontal¾ (au Auto)
1199627500Vertical¾ (au Auto)
1201527500Horizontal¾ (au Auto)
1203427500Vertical¾ (au Auto)
1205427500Horizontal¾ (au Auto)
1207327500Vertical¾ (au Auto)
1224527500Horizontal¾ (au Auto)

ANGALIZO:
Masafa katika jedwali yapo katika Megahertz na Megahertz 1000MHz (Megahertz elfu moja) ni sawa na Gigahertz moja (1GHz).

b) CHANELI ZA C BAND TOKA KATIKA SATELAITI MBALIMBALI.

Kuna aina ngapi za madishi ya C Band:
Kuna aina tatu za madishi ya C Band kutokana na utengenezaji.

1. Madishi ya Bati (Aluminium alloyed satellite dishes)
2. Madishi ya Wavu (Mesh Satellite dishes).
3. Madishi yanayotengenezwa kwa vioo (enforced glass fibre satellite dishes).

Madishi ya bati na madishi ya wave (Mesh) hayana tofauti sana katika utendaji (upokeaji wa mawimbi kutoka katika satelaiti).

Matatizo yanayoyakumba Madishi katika ukanda wetu:
Tatizo kubwa katika ukanda wetu hasa maeneo ya mwambao mwa Bahari ya Hindi (Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Tanga, Mtwara, Mogadishu, Mombasa, na maeneo mengine kusini, kaskazini, Mashariki na Magharibi mwa Afrika na Mabara mengine ni mvuke wenye chumvi kutoka baharini ambao husababisha madishi ya bati yapate kutu na kuharibika haraka.

Madishi ya Bati.
Madishi mengi ya bati yanayoletwa nchini Tanzania ni mchanganyiko aluminium, chuma na madini mengine na hivyo kusababisha yapate kutu kiurahisi. Ukifunga dishi kuelekea satelaiti 906, IS 10 katika maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi na baadhi ya sehemu za Tanzania Bara lazima maji yatuame (kwa madishi ya bati) baada ya mvua kunyesha kwa sababu ziilipo satelaite hizi nyuzi 64.2 na 68.6 Mashariki na sisi hapa kwetu mfano Dar es Salaam tunapofunga dishi halilali sana na kumwaga maji badala yake maji hutuama na kuliharibu dishi baada ya muda mfupi.Jaribu kuangalia madishi yenu baada ya mvua kunyesha mtaona hili. Tatizo la kutuamisha maji huzidi kupungua kadri tunavyozidi kuingia ndani (Magharibi ) mwa Bara la Afrika; mfano mtu aliyeko Kigoma, Ngara au Kagera dishi lake linaweza lisituamishe maji kwasababu tunavyozidi kwenda mbali na satelaiti ndivyo dishi inabidi lilale sana kuipata satelaiti hiyo
View attachment 1084393

Picha hapo juu niliipiga jijini Dar es Salaam. Inaonesha Satellite dish la upana wa futi 8 lililofungwa kuelekea satelaiti Intelsat 906, Intelsat 10 na Intelsat 20 likiwa limetuamisha maji baada ya mvua. Kwa kuwa madishi haya hayatengenezwi kwa kutumia aluminium peke yake (aluminium huwa haipati kutu) huwa yanapata kutu haraka na kutoboka.

View attachment 1084394



1084395

Picha hapo juu inaonesha dishi madishi mawili ya bati kwa ajili ya kupokea masafa ya C Band au Ku Band



Madishi ya Wavu.
Madishi mengi ya Wavu yametengenezwa kwa aluminium (pure aluminium) hivyo si rahisi kupata kutu. Pia kwa kuwa madishi ya wavu (Mesh dishes) yana Matundu; huwa hayaruhusu maji ya mvua kutuama na hivyo kuyanusuru yasipate kutu kwa urahisi. Sehemu za dishi la wavu zinazopata kutu kiurahisi ni bolts na nut zake, na mihimili ambapo madishi yanafungwa (dish bases, dish poles). Ni muhimu kuyapaka Grease ili kuzuia kutu

1084396


Picha hapo juu inaonesha Dishi la Wavu la linalozunguka (moving Mesh dish) kwa ajili ya C Band na Madogo kwa ajili ya Ku Band
1084397

Picha hapo juu inaonesha Dish la Wavu linalozuzunguka (moving mesh dish) kwa ajili ya C Band na Madishi modogo Mawili ya Ku Band

Ufungaji wa dish la C Band hauna tofauti kubwa na Dish la Ku Band. Dish la C Band ni kubwa kuliko la Ku Band. Madishi ya C Band huanzia futi 6ft, 8ft, 10ft, 12ft na kuendelea.

Satelaiti tunazopata chaneli za C Band katika ukanda wetu.
Katika ukanda wetu tunaweza kuona chaneli nyingi toka katika satelaiti kwa kufunga madishi ya C Band. Baadhi ya satelaiti tunazoweza kupata katika eneo letu kwa kufunga madishi kuanzia futi nane (8ft) na kuendelea ni NSS 12, NSS7, IS901, IS902, IS904, IS905, IS906, IS 17, IS907, NSS806, IS10, Apstar 7, Thaicom 5 na nyinginezo.

Matatizo katika mawasiliano.
Matatizo yanayosumbua wakati wa kutafuta satelaiti hizo ni mwingiliano wa mawasiliano kati ya Masafa ya satelaiti katika C Band 3.6GHz - 4.2GHz na mawasiliano ya kawaida (terrestrial transmissions) katika baadhi ya sehemu na baadhi ya miji.
Mfano maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam tatizo hili ni sugu kutokana na kuwa na vifaa vingi vinavyofanya kazi katika C Band 3.6GHz - 4.2GHz (there are many devices transmitting within the Frequency Range 3.6GHz - 4.2GHz).

Tatizo jingine ni baadhi ya chaneli kuwa na mawimbi ambayo hayana nguvu na hivyo kuyafanya yasipatikane katika madishi. Kwa sasa kuna tatizo la mawimbi yanayobeba chaneli:
TBC (Tanzania) Transponder No. 93, Masafa 3.891GHz - Left Circular
Startv (Tanzania) Transponder No. 93, Masafa 3.884GHz - Left Circular
UBC (Uganda
) Transponder No. 11, Masafa 3.721GHz - Right Circular
Channel Ten (Tanzania) Transponder No. 93 Masafa 3.905GHz - Left Circular
Agape TV Network (Tanzania) Transponder No. 93, Masafa 3.900GHz - Right Circular

kutoka katika satelaiti inayoitwa Intelsat (IS906 iliyopo nyuzi za longitudo 64.2 Mashariki mwa Mstari wa Greenwich) kutokuwa na nguvu nahivyo kushindwa kupatikana katika madishi ya yenye kipenyo (diameter) cha futi sita (6ft) na kupatikana kwa tabu katika madishi ya futi nane (8ft).

Nini kinaweza kuwa chanzo cha kutopatikana kwa chaneli hizo hapo juu?
Kutokupatikana kwa chaneli hizo hapo juu kunaweza kusababishwa na:

Sababu ya kwanza:
Nguvu ya mawimbi yanayopelekwa katika satelaiti kuwa ndogo (low satellite uplink power).
Kwa kawaida huwa kuna makubaliano (mikataba) kati ya wamiliki wa vituo vya redio na televisheni vinavyotumia satelaiti na wamiliki wa satelaiti. Mikataba hiyo huonesha nguvu ya mawimbi yanayopelekwa katika satelaiti. Mamlaka zinazodhibiti mawasiliano katika nchi mbalimbali hupewa nakala za mikataba hiyo. Nguvu ya mawimbi (uplink power) yanayokwenda katika satelaiti inaweza kuongezwa au kupunguzwa katika vituo vya redio/ televisheni vinavyotumia satelaiti ila haitakiwi kuzidi kiwango walichokubaliana.
Ukiongeza nguvu ya mawimbi yanayokwenda katika satelaiti yakazidi kiwango cha makubaliano na mmiliki wa satelaiti (above contract power) unaweza kusababisha mwingiliano na chaneli nyingine katika satelaiti; chaneli ambazo masafa yake yanakaribiana na chaneli yako. Wakati wa kuongeza nguvu ya mawimbi yanayokwenda katika satelaiti katika vituo vya televisheni/ radio lazima yawepo mawasiliano kati ya pande mbili ili nguvu isizidi kiwango au isipungue kiwango.
Vituo vingi husaini mikataba ambayo power level ni ndogo kwa sababu ya gharama (kadri unavyopeleka nguvu kubwa katika satelaiti ndivyo unavyolipa zaidi). Kumbuka kulipia Transponders gharama yake si mchezo.
Wengine husaini mikataba ambayo nguvu ya mawimbi yake ni ndogo kwa kukosa wataalam wa kuwashauri vizuri juu ya hilo.

Sababu ya pili:
Katika satelaiti kuna kifaa kinachoitwa "Transponder".

Transponder ni nini?

Transonder ambayo kwa mara nyingi huitwa kwa kifupi XPDR, XPNDR, TPDR or TP maana yake kwa jina la kitaalam ni "Transmitter - Responder".
Ni kifaa ambacho kipo ndani ya satelaiti ambacho kazi yake ni kupokea mawimbi katika masafa makubwa toka ardhini (mfano katika vituo vya redio na televisheni katika C Band 5.850GHz - 6.425GHz, katika Ku Band 14.0GHz - 14.5GHz kuyakuza (amplification) na kuyapunguza masafa (downconvert) kwa C Band 3.6 - 4.2GHz na kwa Ku Band 10.7GHz - 12.75GHz na kuyarusha tena ardhini katika uso wa dunia ambapo tunayapokea majumbani mwetu na maofisini mwetu kwa kutumia madishi. Satelaiti moja inaweza kuwa na idadi ya transponder hadi 70.
Satelaiti huwa zina muda wa kukaa angani. Zikianza kuchoka Transponder zilizoko katika satelaiti hushindwa kufanya kazi vizuri na wakati mwingine kusababisha matatizo kama haya.

Anayeweza kutoa jibu kamili juu ya kupotea kwa mawimbi au mawimbi kuwa madogo katika satelaiti husika ni vituo vya televisheni / radio husika, mmiliki/operator wa satelaiti husika na Mamlaka zinazotumika kudhibiti Mawasiliano katika nchi husika. Mfano IS 906 inamilikiwa na kampuni inayoitwa Intelsat iliyoko na makao yake makuu Atlanta, Marekani.
Ni wajibu wa Mamlaka zinazosimamia Mawasiliano katika nchi zao kuhakikisha hayo mawasiliano ambayo wanatoa leseni kwa waendeshaji wa vituo vya Televisheni na Radio kupitia satelaiti yanapatikana. Katika Tanzania anayetakiwa kusimamia hili ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kenya Tume yao ya Mawasiliano inaitwa CCK, Uganda - inaitwa UCC, Rwanda - inaitwa RURA, Burundi - inaitwa ARCT, Zimbabwe - inaitwa POTRAZ na nchi nyingine (kila nchi ina Mamlaka/Tume yake ya udhibiti wa Mawasiliano.
Tatizo tulilonalo katika nchi nyingi juu ya kubaini matatizo haya ni kutokuwa na vifaa vya kutosha hasa katika upande wa kudhibiti mawasiliano yanayokwenda au yanayotoka katika satelaiti.

Tatizo la Tatu:
Ukifunga dishi sehemu ambayo ina mitambo inayorusha mawimbi sawa na unayoyapokea toka katika satelaiti dishi linaweza lisifanye kazi au nguvu ya mawimbi unayoyapokea itakuwa ndogo kwa sababu kunakuwa na mwingiliano wa mawasiliano. Kiwango cha madhara ya mwingiliano wa mawasiliano ya satelaiti toka mitambo iliyopo jirani (nearby terestrial transmissions) hutegemea nguvu ya mawimbi yanayotoka katika mitambo hiyo. Ila ukifuatilia ukaona tatizo la kutopatikana kwa mawasiliano lipo sehemu nyingi; mikoa mingi au nchi nyingi ujue tatizo hilo linatokana na sababu nilizozitaja hapo juu.

Mwingiliano wa Mawasiliano katika jiji la Dar es Salaam.
Kumewahi kuwepo kwa matatizo makubwa ya mwingiliano wa mawasiliano katika C Band kati ya mwaka 2007 hadi 2008 katika jiji la Dar es Salaam matatizo yaliyofanya baadhi ya chaneli za televisheni/radio toka katika satelaiti zisipatikane kabisa. Tatizo hili lilisumbua sana.
Tatizo la mwingiliano wa mawasiliano hukumba zaidi madishi yanayofungwa juu ya maghorofa kuliko madishi yanayofungwa chini kwa sababu mawasiliano kutoka mitambo ya jirani huwa yapo katika mstari mmoja (line of site) na madishi yanayofungwa juu ya maghorofa.

1084398


Picha/ grafu hapo juu imetokana na kipimo nilichofanya kwa kutumia Spectrum Analyzer tarehe 24 Februari, 2008 katika jiji la Dar es Salaam katikati ya Kijitonyama na Mikocheni. Kipimo hiki nilikichukua nikiwa chini tu. Kama ingekuwa juu ya maghorofa ambapo mawasiliano yanakatiza kiwango cha mawimbi yanayoingilia mawasiliano kingekuwa juu sana. Wakati huo kulikuwa na mwingiliano mkubwa wa mawasiliano kutoka katika satelaiti na kusababisha baadhi ya mawasiliano kutoka katika satelaiti mbalimbali kuwa magumu sana. Nilianza kulifuatilia suala hili kwa karibu na kugundua kulikuwa na vifaa/ transmitter (vifaa vingi vilikuwa vinatumika kwa mawasiliano ya data) zilizokuwa zikifanya kazi katika masafa ambayo yametengwa kupokea mawasiliano kutoka katika satelaiti. Hili tatizo lilikuwa kubwa na liliharibu mawasiliano ya data na chaneli za televisheni/ redio (mfano ITV, CAPITAL, EATV, CHANNEL TEN na nyinginezo) kutoka katika satelaiti mbalimbali.

Maelezo ya Picha / Graph:
Katika grafu kuna X na Y Axis.
X Axis: Katika grafu kutoka kushoto kwenda kulia ( masafa), kati ya mstari na mstari ni Megahertz 100MHz. Kutoka Mwanzo wa grafu hadi mwisho (Span) ni 1GHz.Maana yake kutoka 3.5GHz - 4.5GHz. Katikati ya grafu ni 4GHz.

Y Axis: Katika grafu kuanzia chini hadi juu huu inaonesha nguvu ya mawimbi (power levels).

Picha ilipigwa (scanning) kutoka 3.5GHz - 4.5GHz.
Kutoka 3.5GHz hadi 3.6GHz kuna mawasiliano ya internet/data.
Masafa 3.6GHz - 4.2GHz yametengwa kwa ajili ya kupokea mawasiliano kutoka katika satelaiti katika C Band mfano ITV, EATV, CAPITAL (3.641GHz), TBC 3.891, Startv 3.884GHz, Channel Ten 3.905GHz)
Matuta yanayoonekana katika grafu ni mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika katika masafa hayo.

Katikati ya 3.6GHz - 4.2GHz hakukutakiwa kuwa na Matuta (transmissions):
Katika Grafu:
Mark 1: 3.764GHz
Mark 2: 3.817GHz
Mark 3: 4.025GHz
Mark 4: 4055GHz

Ukiangalia katika grafu kuanzia 3.6GHz hadi 4.2GHz kuna matuta ambayo ni mawasiliano (local terrestrial transmissions) zilizosababisha kukoseka/ kupotea baadhi ya mawasiliano.

Nini kinachotakiwa kufanyika endapo mawasiliano yanaingiliwa.
Ni wajibu wa Mamlaka/Tume zinazosimamia na kudhibiti Mawasiliano katika nchi husika kuhakikisha masafa yanatumika kama yalivyopangwa.
Na ikitokea hivyo hao watu wanaofanya hivyo lazima wanyanganganywe masafa hayo kwa sababu wanakuwa wanayatumia kinyume na utaratibu. Kwa kufanya hivyo husababisha mwingiliano au kupotea kwa mawasiliano ya watu wengine.

Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kurusha mawasiliano kati ya 3.7GHz hadi 4.2GHz katika Afrika, Ulaya na Urusi (Region 1) kwa sababu masafa hayo yametengwa na ITU (International Telecommunications Union) kwa ajili ya kupokea mawasiliano ya televisheni/ redio na data kutoka katika satelaiti.
Tazama ukurasa wa ITU katika blog hii.


Masafa ya C Band kwa Undani:

Masafa ya C Band Duniani​
Band
Masafa ya Kupeleka mawimbi katika satelaiti Masafa ya Kupokea Mawimbi kutoka katika satelaiti
Standrd C - Band5.850–6.4253.625–4.200
Extended C - Band6.425–6.7253.400–3.625
INSAT / Super – Extended C - Band6.725–7.0254.500–4.800
Urusi C - Band5.975–6.4753.650–4.150
LM C - Band5.7250–6.0253.700–4.000


Ufungaji wa LNB zaidi ya Moja katika Madishi ya C Band.
Inawezekana kufunga LNB za C Band katika dishi la futi 6 (6ft), 8ft, 10ft na kuendelea.

Madishi yote ya C Band (kuanzia kipenyo cha futi 6ft, 8ft, 10ft na kuendelea) yametengenezwa kwa ajili ya kupata chaneli kutoka katika satelaiti moja ila kuna utundu/ubunifu wa kuliwezesha dishi moja lipokee chaneli toka satelaiti zaidi ya moja ambazo zipo karibu karibu. Hii inawezekana kufanya hivyo kwa kufunga LNB zaidi ya moja (mara nyingi LNB 2, 3 na wengine hata LNB 4). Kufanya hivi kuna faida na hasara zake:

Faida zake:
Mfumo huu hutuwezesha kupata chaneli nyingi kutoka katika satelaiti tofauti tofauti. Mfumo ulioenea hapa mjini ni ufungaji LNB mbili, tatu au nne katika madishi ya futi 6ft na futi 8ft.
LNB ya 1 ni ya C Band na hupokea chaneli kutoka satelaiti IS 906 (Intelsat 906).
LNB ya 2 ni ya C Band na hupokea chaneli kutoka satelaiti IS 10 (Intelsat 10) na Intelsat 7 @ 68.6E
LNB ya 3 ni ya Ku Band na hupokea chaneli kutoka satelaiti NSS12 (ili kupata chaneli za Zuku, KBC (Kenya) n.k.
LNB ya 4 ni ya Ku Band na hufungwa juu ya LNB ya C Band ili iweze kupokea chaneli zinazotumwa katika masafa ya Ku Band kutoka katika satelaiti IS 10 @ 68.5 Mashariki mwa Greenwich. LNB ya Ku Band hufungwa hapo kwa kuitoboa LNB ya C Band (inayopokea chaneli kutoka IS 10) au hufungwa pembeni kidogo (kwenye mkono wa dishi).

Wengine hufunga hadi LNB 4 au 5 katika dishi la futi 6ft au 8ft kupata chaneli kutoka satelaiti nyinginezo kama IS902 na satelaiti nyinginezo.

Jambo muhimu la kuzingatia:
Kuna baadhi ya satelaiti ambazo hufanya kazi katika masafa ya C Band tu, nyingine masafa ya Ku Band tu na nyingine hufanya kazi katika masafa ya C Band na Ku Band.

Hasara zake:
Kufunga LNB nyingi katika dishi moja ni kulilazimisha dishi lifanye kazi ya ziada (kulitumia kikamilifu). Faida zake nimezitaja hapo juu (kupata chaneli nyingi toka satelaiti tofauti tofauti).
Kwa kuwa dishi linakuwa limelazimishwa ; baadhi ya chaneli hasa ambazo mawimbi yake kutoka katika satelaiti hayana nguvu huwa zinakatika katika na wakati mwingine huwa hazipatikani kabisa kwa sababu dishi linakuwa halijalenga katika satelaiti moja (linakuwa katikati).

Mfumo mzuri wa kupata chaneli mbalimbali toka katika satelaiti tofauti tofauti ni kufunga madishi zaidi ya moja kila dishi likilenga satelaiti yake au dishi moja lilenge satelaiti mbili (kwa ambazo zipo karibu karibu na ambazo mawimbi yake yana nguvu sana).

JAMBO LA MUHIMU KUZINGATIWA:
Hakuna madhara yoyote ukisimama mbele ya dishi linalopokea mawasiliano kutoka katika satelaiti (downlink satellite dish) kwasababu mawimbi yanayotoka katika satelaiti yanakuwa yamesafiri umbali mrefu na hivyo nguvu yake inakuwa ndogo.

Unaweza kupata madhara ukisimama kwa muda mrefu mbele ya satelaiti dishi (parabolic reflectors) za VSAT hasa zinazofungwa chini na antena bapa (flat antenna) mfano antena zinazotumika kwa ajili ya mawasiliano kama INMARSAT, antena za RADAR, antena za SNG (Satellite News Gathering) ambazo hupeleka mawasiliano katika satelaiti. Pia ukisimama karibu na antena za GSM/CDMA, antena za microwave links kwa muda mrefu unaweza kupata madhara (hasa mafundi wanaozifunga).

Minara ya kurusha matangazo ya redio na televisheni hurusha mawimbi yenye nguvu zaidi hewani kuliko ya mitambo ya simu ingawa masafa yake yanakuwa madogo kuliko ya mawasiliano ya simu. Hata ukifungua muziki kwa sauti ya juu unapata madhara (hasa kwa watoto wadogo ambao ngoma ya masikio - "diaphram" ni rahisi kutoboka). Madhara mengine yanatokea baada ya muda mfupi na mengine baada ya muda mrefu.
Kila kitu duniani kina athari zake kwa viumbe hai; hata mimea, miti, majani ya miti hutoa mionzi ingawa kwa kiwango kidogo (chukua dishi lizungushe kama unatafuta mawimbi ya televisheni fulani kutoka katika satelaiti mfano katika C Band badala ya kulielekeza dishi juu katika satelaiti lielekeze katika miti utaona mawimbi (signal) ikiongezeka. Kama hutumii Spectrum Analyzer unaweza kutumia hata risiva ya satelaiti.

Si rahisi kukwepa athari zinazotokana na mionzi iliyopo katika mawimbi hapa duniani kwa sababu duniani tumezungukwa na mawimbi ambayo mengine yanatokana na ulimwengu huu (natural radiations) na mengine yanatokana na vifaa / mitambo ya kutengenezwa na binadamu (manmade radiations). Tunachoweza kufanya ni kujitahidi kujiepusha kuishi karibu na sehemu au na vifaa/mitambo inayotoa mionzi yenye nguvu sana. (Mitambo isifungwe karibu sana na makazi ya watu: kuna antena za minara ya simu zinafungwa katika maghorofa jirani kabisa na madirisha ya nyumba).
Mionzi mbalimbali iliyopo hapa duniani (mionzi ya asili) na ya kutengenezwa na binadamu (man made) hupunguza muda wa binadamu kuishi hapa duniani

Shukrani sana kwa hii elimu ndogo niliyo nayo naamini wapo wengi wanao fahamu zaidi na ukitembelea mitandao mbalimbali wameeleza kwa undani zaidi
 
umenikumbusha ile satellite iliyopotea kwenye mzunguko wake na kwenda kusikojulikana. AMOS5, hii kwa hapa tz kinga'muzi cha Ting ndo walikua wamejiunga nayo sasa ilivyopotea tu mawasiliano yakakata palepale. Mpaka leo wanaitafuta kwenye system hawaioni sijui imepoteaje na imeenda wapi
 
Kwanza Heshima kwako mkuu DIGE,huwa napenda sana kujua mambo haya ya madish ila leo umeniongezea elimu zaidi ,pamoja sana mkuu.
 
DIGE iko poa sana hii article.

Hivi nikiwa LNB za ku-band naweza pata channel za c-band?

Satellites gani ambazo beam zake zinafika tz ambazo naweza pata FTA channels?

Na dish la size gani ambalo linaweza punguza noises wakati wa mvua au kupata beams za satellites zinazofika kwa shida tz.
 
DIGE iko poa sana hii article.

Hivi nikiwa LNB za ku-band naweza pata channel za c-band?

Satellites gani ambazo beam zake zinafika tz ambazo naweza pata FTA channels?

Na dish la size gani ambalo linaweza punguza noises wakati wa mvua au kupata beams za satellites zinazofika kwa shida tz.
Licha ya uzi kuwa na nondo kali lakini bado kuna maswali..
 
Dah nmekuwa fund kwa zaid a miaka 10 xx ila haya uliyoyaeleza ndo nmeyaelewa leo maana yake maana nlikua nkifanya kinamazoea yaan utundu bila elimu na mambo huwa yanaenda vzr tu
Heshima kwako mkuu
Pamoja sana tunajulishana hata kidogo tukicho nacho
 
Hayo yote uliyoyaeleza sisi tuliosoma HKL zinatusaidia vipi kuelewa? ungetuambia lugha rahisi kabisa kama una uwezo wa kuuza na kuunganisha dish ili zikamate bure bila kulipia kwa viwango vya juu sisi tutatoa pesa tunachotaka ni maisha rahisi hayo madude magumu uliyoyaeleza mka discus kwenye vipindi vyenu madarasani
 
DIGE iko poa sana hii article.

Hivi nikiwa LNB za ku-band naweza pata channel za c-band?

Satellites gani ambazo beam zake zinafika tz ambazo naweza pata FTA channels?

Na dish la size gani ambalo linaweza punguza noises wakati wa mvua au kupata beams za satellites zinazofika kwa shida tz.
Ukipitia vizuti nimeeleza kila kitu unaweza pata itategemea na receiver unayo tumia pamoja na uelekeo wa dish jaribu kurudia juu nimeweka sawa yote
 
Hayo yote uliyoyaeleza sisi tuliosoma HKL zinatusaidia vipi kuelewa? ungetuambia lugha rahisi kabisa kama una uwezo wa kuuza na kuunganisha dish ili zikamate bure bila kulipia kwa viwango vya juu sisi tutatoa pesa tunachotaka ni maisha rahisi hayo madude magumu uliyoyaeleza mka discus kwenye vipindi vyenu madarasani
Naamini hata wa HKL ulikaa darasani ukasoma lengo langu ni kwa yule ambae anaweza akajifunza anaweza akapunguza gharama za kuita mafundi kwakuwa kuna vitu vichache unaweza fanya bila fundi
 
Naamini hata wa HKL ulikaa darasani ukasoma lengo langu ni kwa yule ambae anaweza akajifunza anaweza akapunguza gharama za kuita mafundi kwakuwa kuna vitu vichache unaweza fanya bila fundi
real no one who is born a craftsman. Tusifike sehemu tukajidanganya kuwa kitu fulani ni kwa ajili ya watu tuu kumbe tukiweka juhudi na kutenga muda wa kujifunza utakielewa tuu.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom