Wale wa home made products, njooni hapa

mzalendo namba moja

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
390
476
Kwa namna maarifa yanavyozidi kuongezeka kuna bidhaa nyingi zinaweza tengenezwa ukiwa nyumbani tu kikubwa ujikusanyie malighafi Kwanza. Mimi binafsi nmejifunza vitu vingi na nisingependa kuwa mbinafsi, naweza kushare baadhi ya maarifa niliyonayo hapa, najua wengi wanajua pia, ukiona yafaa waweza weka maarifa yako hapa from scratch au hata video ikiwezekana.

Mfano wa maarifa hayo ni pamoja na utengenezaji wa:- sabuni zote kwa formula zote, shampoo, mishumaa, tomato soes, maji ya betri, mchanganyo wa dawa za kuprintia t-shirts, dawa za viatu, dawa za meno, mafuta ya kujipaka, lotion, spray, dawa za kusafisha malumalu, cake, pombe, wine, spirits, soda n.k, najua wengi wana wengi

Karibuni wana jukwaa

NITAANZA NA SABUNI YA MAJI

Ni sabuni nzuri kwa ajili ya matumizi ya kufulia, kudekia na kufukuzia wadudu.

Mahitaji yote yanapatikana kwenye maduka ya vjfaa vya wajasiliamali au waweza tafuta ofisi za Allied Chemicals au SIDO na kwa wale wa Mwanza tuwasiliane ili nikuelekeze..

MAHITAJI
kwa sabuni lita 25

✓chumvi yeyote kilo 1
✓ sulphonic acid ½ lita
✓Siles kilo 1
✓Rangi (uipendayo) vijiko viwili vya chakula
✓perfume (uipendayo) Mili-lita
50
✓maji lita 25
✓diaba la plastic (sio chuma)
✓mti mkavu wa kukorogea

HATUA ZA UTENGENEZAJI
Tanabahi: hii ni formula mpya, kama ipo nyingine nzuri zaidi na rahisi utaweka.

¶ baada ya kuweka maji kwenye diaba hizo lita 25 weka chumvi yote (kilo 1) kisha koroga dkk 5 na uhakikishe imeyeyuka yote

¶ Kisha tia sulphonic Acid {hakikisha umevaa gloves au kilinda mikono chochote ili tu sulphonic isikumwagikie (ni hatar ikikumwagikia)} kisha koroga kwa nusu saa nzima mpaka uone povu jeupe limeshamiri kwenye maji

¶ kisha weka Siles na koroga vizuri kwa nusu saa nyingine mpaka sabuni iwe nzito kabisa na baada ya hapo funika diaba lako na liache kwa masaa kumi na mbili kuruhusu mchanganyo ukae sawa

¶ Baada ya hapo waweza funua na kutia perfume kisha koroga dkk 5 na kisha weka rangi then koroga tena dkk 5, na sabuni itakuwa tayr kwa matumizi

tanabahi: usiache wazi muda mrefu ili kutunza perfume yako na usiiache juani, karibuni kwa maswali.
 
Asantee Sana bosi Mimi nipo mwanza ningependa kujua bei za material hayo , nahakika nitayapata pale sido yote
Kweli mkuu, pale kijereshi utawapata, lakini jengo la CCM mkoa utawapata Allied chemicals pia, sijui uko mtaa gani lakini huku mtaani kwetu kuna maduka zaidi ya matatu ya malighafi hizo.
 
Namna ya kutengeneza shower jelly
Hii sina hakika nayo mkuu, ngoja tungoje wanaojua vyema

Kwa kuongezea hapo juu, baada ya sabuni kupatikana kabla hujatia rangi, unaweza kuhit too in one (shampoo na sabuni), tenga litre nne za sabuni isiyo na rangi wala perfume( ambayo hujaimalizia hatua za mwisho alafu baada ya ya hapo tia rangi ya kijani(ndiyo rangi pendwa kwenye shampoo) koroga kwa dkk tano kisha ongezea GLYCELINE Mili-lita 200 (zinapatikana pia SIDO) kisha koroga na iache itulie nusu saa na shampoo itakuwa tayar, wakt huo upande wa sabuni utaendelea na mchanganyo uleule kwa kipimo kilekile (rangi na perfume) haitaleta tofauti yeyote
 
Kuna perfume za matunda zisizo na harufu kali ukipenda utaongezea lkn hata usipoweka ni murua kabisa inafaa.
 
JINSI YA KUTENGENEZA LOTION KWA NJIA RAHISI KABISA.

Tanabahi: mahitaji yote yanapatikana maduka ya vipodozi, maduka ya dawa (baadhi) na mengine ni kwa mazingira yetu ya kila siku

MAHITAJI

✓Mafuta ya nazi (yanapatikana)
✓Aloe Vera gel (duka la vipodozi)
✓Rose water (jaribu supermarkets)
✓Glycerin(inapatikana)
✓Vitamin e Capsule/oil (duka la vipodozi)

UTARATIBU

Weka kwenye bakuli safi kijiko kimoja cha chakula cha aloe vera gel (ya dukani iwe 100% natural)

Ongeza kijiko kimoja cha chakula cha mafuta ya nazi pamoja na glycerin na rose water kisha ongezea na vitamin e kama ngozi yako ya mafuta tumia capsule kama kavu unaweza kutumia vitamin e oil

Changanya vizuri mpaka ichanganyike na uone imekua na rangi ya kupendeza na ipo laini kisha hifadhi kwenye kichupa safi tayari kwa matumizi

utadouble au kutripple malighafi kulingana na mahitaji yako

Note: chukua mahitaji kwa ujazo mkubwa na utakuwa na unatoa kidogo kidogo kila mara lotion ikiisha.

Mfundishe mtoto na mkeo wajikomboe kwa suala la manunuzi ya lotion, sio muda ntaweka formula nyingine ya lotion ntaunganushia na ya mafuta ya mgando.
 
JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO (NATURAL)*

Chagua moja kati ya lotion zifuatazo

Mahitaji

✓Vitamin c powder (kijiko 1 cha chakula)

✓Vitamin e Capsule (kidonge 1)

✓Rose water (kijiko 1 cha chakula)

✓Glycerin (kijiko 1 cha chakula)

✓Shea butter au Vaseline lotion/Lotion yoyote uipendayo 100ml

HATUA ZA KUFUATWA

Tia rose water kwenye bakuli safi kisha tia kijiko kimoja cha unga wa vitamin C

Changanya vizuri na ukoroge kwa muda wa dakika 5 mpk vitamin c iyeyuke kabisa kisha ongezea glycerin na vitamin e na uchanganye vizuri

Tia lotion yako ya vaseline ujazo wa ml 100 ama shea butter ama cream yoyote uipendayo mwenyewe kisha changanya vizuri hadi ichanganyike

Weka kwenye chupa safi tayari kwa matumizi

Hii itafanya ngozi yako kua laini na kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuiacha ikipendeza zaidi na zaidi

Unaweza kupaka kwenye mwili hata usoni na ni salama kabisa haina sumu

Note: hapa huanzi from scratch kutengeneza lotion lakini unapata uhakika wa kung'arisha ngozi yako within a week, kwa viambata tajwa hapo ukichanganya na lotion yoyote, preferably Vaseline
 
Kama uso una mafuta sana naweza ongeza kidonge Cha vitamin E?
 
Back
Top Bottom