Nichumu Nibebike
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 8,658
- 15,784
Siku moja nikiwa nimetoka Tegeta (Wazohill) kwa bebi angu nikafika mahali nikawakuta vijana kama watatu hivi wa Kiarabu wakiwa wameharibikiwa na gari yao. Nikasimamisha gari na kuanza kuwahoji, mafuta yapo, wakajibu yapo, nikawauliza mmeangalia oil ipo wakasema ipo. Nikawauliza sasa ni kwanini gari haiwaki, wakasema hata wao hawajui maana limezimika ghafla na wamejaribu kiwasha lakini wapi.
Kwa mda ule walionekana kukata tamaa maana mda ulikuwa umeenda na ilikuwa ni kama saa nne za usiku... Wakaniomba nishuke niwasaidie kuangalia shida ni nini. Nikawaambia hapana sishuki. Nikamwambia dereva wao aingie ndani awashe gari, wakasisitiza nishuke niwasaidie kuwangalia. Mimi nikawaambia tu wawashe gari maana haina haja ya mimi kushuka.
Mwishowe dereva wao akaingia kwenye gari akapiga stata. Gari hiyooo ikawaka. Wale vijana walibaki wamepigwa na butwaa wasiamini kile kilichokuwa kinatokea. Ile gari limewaka, wote wakarukia kwenye gari. Sikutaka stori nao zaidi na mimi nikaondoka zangu. Ila kwa tukio lile lilivyotokea, wale vijana watakuwa wamewaza sana juu yangu na kudhani labda nina nguvu za ziada...
Mpaka leo najiuliza ni nini kilitokea hata mie mwenyewe sijapata majibu... Its alomst three years ago na hili tukio bado nalikumbuka...