Wale tunaovaa Barakoa tupeane experience jinsi ya Kuvaa, mwenzenu inaniletea matatizo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Salaam wakuu,

Huu Ugonjwa wa Corona umekuja na mengi ikiwemo kuvaa Barakoa kuziba mdomo na Pua ili ili majimaji ya Korona yasikupate au hata kama na wewe una Corona usiweke kuambukiza wengine pale unapo piga chafya.

1587970803270.png

Ila mimi nikiivaa naona ni Mateso makubwa. Wenzangu mnawezaje kuvaa Barakoa asubuhi hadi jioni?

Mimi nikivaa Barakoa muda mrefu, kichwa kinaniuma, nasikia kizunguzungu, macho yanakua hayaoni vizuri, na saa nyingine najisikia homa pae nivaapo Barakoa kuliko siku ambazo Sivai.

Imefika kipindi hata kuvaa najishauri naiweka mfukoni tu. Tena bora ya Kitambaa hizi za kushona, lakini nikivaa vile Special ndo najisikia kufa kabisa.

Nimekuja hapa kuuliza kama ni mimi tu au kila mtu anajisikia kama mimi? Kama vipi tushinikize Shirika la Viwango Tanzania Bureau of Standards (TBS) lifanyie uchunguzi hizi barakoa Zilizoingia Nchini. Naamini hazina viwango. Sababu ukiwa umeivaa ukipumua hewa haitoki nje, ukivuta unavuta hiyo hiyo. Nahofia Barakoa zinaweza niletea maradhi hivyo nina panga kufanya kinyume labda nishauriwe namna nzuri ya kuvaa.

Tangu nianze kuvaa Barakoa Macho yangu yamekua mekundu kama navuta Kaya. Ni mateso kwa kweli, Mungu tuokoe.

Nakosa uhuru wa kuvuta hewa safi. Pumzi ninayo ivuta hainitoshi. Kama nilikua navuta pumzi ya kujaza lita moja, sasa navuta kikombe kimoja tu nikiwa nimevaa Barakoa aka Mask

Leo nmeona idadi ndogo ya watu walovaa Barakoa, nahisi wamekiona cha moto.

Waziri wa Afya alikataza tusivae Barakoa namba N95 sababu ni chache na tuwaachie wahudumu wa afya. Kwakuwa hili swala linahusu uhai, imebidi nitafute hizi kwani nahisi zitakuwa na ubora zaidi.

1587971108290.png
1587971586818.png
 
Haya madude yamekuwa kero sana yananipunguzia hewa, navaa kwenye daladala tu, nkifika kazini navua. Mabossi washasema sana hadi wameamua kuniacha. Uzuri DAHRM wangu mwoga sana nikiamua job siendi napiga simu tu kama naumwa, najilalia zangu home.
 
Back
Top Bottom